Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,183
- 10,921
Kumekuwepo na fununu za muda mrefu juu ya kuwepo kwa wapiganaji wa kikundi cha Wagner kilichohusishwa na kiongozi wa Urusi,Vladmir Putin.Hii ilikuwa ni kabla hata ya kuanza kwa vita vinavyoendelea sasa baina ya Ukraine na Urusi.
Katika kipindi kifupi fununu hizo ziliongezeka baada ya kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi kwenye nchi za Afrika magharibi na kati kama vile Mali na Burkinafaso. Mapinduzi hayo mara zote yameambatana na kufukuzwa kwa majeshi ya Ufaransa ambayo ni mwanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO. Hali hiyo ilipelekea Ufaransa kuhamishia shughuli zake Niger ambako tayari Marekani ina kituo chake kikubwa cha kuongozea droni za kupambana na inaowaita wanamgambo wa ISIS na Alqaeda na Bokoharam.
Wiki iliyopita mapinduzi mengine yameendelea nchini huko ambako ilikuwa kama ni ngome kubwa ya washirika wa NATO kwa magharibi ya Afrika.Kilichoshangaza ni kutokea waandamanaji wengi wakiunga mkono mapinduzi hayo na kupeperusha bendera za Urusi.
Nchi ya Ufaransa na nchi nyengine zimehamisha wananchi wake lakini inaonekana ni kwa shingo upande huku ikitafuta mwanya wa kubaki.Kitu kilichowapa moyo kutokutoa tamko la kuondoka moja kwa moja ni tangazo la ECOWAS la kuwataka wanajeshi waliopindua kumrudisha kiongozi wa kidemokrasia,raisi Bazoum ambaye wanasema alichaguliwa kidemokrasia.
Kwa upande mwengine majirani wa Niger,Burkinafaso na Mali na nchi ya Guinea nao wametoa onyo iwapo ECOWAS itatumia nguvu kama walivyotangaza za kumrudisha madarakani raisi Bazoum basi na wao watakuwa pamoja na Niger.
Maamuzi ya ECOWAS ni kama kwamba yanaonekana kuwaunga mkono NATO na kwa upande mwengine NATO nao wameamua kuunga mkono uamuzi huo kwa maslahi ya kubaki Niger hapo.
Jana kiongozi Kuonesha kuwa ECOWAS imedhamiria kufanya kweli hapo juzi mwanachama mkubwa wa umoja huo Nigeria iliizimia umeme Niger ambayo inapata nguvu za nishati ya umeme zaidi ya asilimia 70 kutoka nchini humo.
Kwa upande wa kuonesha Niger nayo imedhamiria kweli kulinda mapinduzi yake hapo jana mmoja wa viongozi wa juu wa mapoinduzi ya kijeshi General Salifou Mody alikwenda Mali kukutana rasmi na wawakilishi wa Wagner kupanga namna ya kuyalinda mapinduzi hayo ambayo yakikamilika na kufanikiwa itakuwa na faida kubwa kwa taifa la Urusi kiuchumi na kisiasa.