Swali fikirishi. Kwanini Rais Magufuli hakugusia viwanda cha tumbaku na cha Hezi Mazava vilivyofungwa kwenye utawala wake?

kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,638
5,139
Niliwahi andika humu nikionya kwamba Sera mbovu za kodi na viwanda inaenda kusababisha kufungwa kiwanda cha Tumbaku Moro na hivyo kupelekea kupoteza zaidi ya ajira 1000 za moja kwa moja.

Wapiga pambio humu walinishambulia. Kiwanda kikafungwa mwaka Jana na wale jamaa kuondoka.

Baadaye kidogo kiwanda cha jezi mazava nacho kikafungwa. Hivi vyote Rais Magufuli hakuongelea . yeye ka focus kumshambulia Abood kwa viwanda alivonunua vikiwa vimejifia.

Simtetei Abood. Ninachoshangaa hapa ni unafiki wa Rais kutogusia hivi viwanda viwili vilivokufa ndani ya awamu ya utawala wake.
Je Rais Magufuli anachuki binafsi na Abood?

Sisi weusi ni wanafiki sana. Siipendi CCM lakini nasema hivi ukilinganisha wabunge rangi nyeusi na wale wabunge wenye Asili ya Asia , kuna tofauti kiutendaji majimboni. Hawa weusi hujitokeza majimboni kwa nadra kama sio wakati wa kuomba kura. Wabunge asili ya Asia at least hufanya vitu tangible. Atleast.

Upande wangu naamini Abood angeweza kufanya mengi morogoro ,tatizo Rais amekua akimshambulia kila akipita morogoro mbele ya umma.
 
Anashindwa nini kufanya hayo mengi? Kwani anamfanyia Rais au wananchi aliowaomba kura wakamchagua? Kama hakufanya eti kwa sababu Rais anamsemasema basi Hana sifa za kuwa kiongozi na hawafai watu wa Morogoro.
 
anashindwa nn kufanya hayo mengi??? Kwani anamfanyia rais au wananchi aliowaomba kura wakamchagua??? Kama hakufanya et kwa sababu rais anamsemasema basi Hana sifa za kuwa kiongozi na hawafai watu wa morogoro.
Kwani huyo Magu angeshambuliwa hivyo angefanya kazi gani?Jimboni kwake alifanya nn?Acha unafiki na wewe.
 
Inahitaji akili ndogo sana kuangalia tu ajira zilizopotea ama zitakazopokea kama kigezo cha kufanya ya maamuzi ya kufunga kiwanda ama kutokukufunga? pita mtandaoni jifunze kitu kinaitwa "Cost and Benefit Analysis " itakusaidia.
 
Rais amesemea viwanda Moproco na canvas alivyonunua Abood kwa nia ya kuvifufua na hakufanya hivyo! Je! Anaonewa? Japo kiwanda cha tumbako kimefungwa, hakisaidii Abood kuona kama hakutimiza ahadi yake - bado amekosea na kusemwa lazima asemwe. Hapa rais hamchukii.
 
Tumbaku kilifungwa kwa sababu malowezi Zimbabwe wamerudi kulima tumbaku so cheap tumbaku plus utawala wa jk pinda alidanganywa na wezi wakachukua tenda ya pembejeo, yaani kwa ufupi mchawi ni serikali iliyopita na siyo jpm
 
Inahitaji akili ndogo sana kuangalia tu ajira zilizopotea ama zitakazopokea kama kigezo cha kufanya ya maamuzi ya kufunga kiwanda ama kutokukufunga? pita mtandaoni jifunze kitu kinaitwa "Cost and Benefit Analysis " itakusaidia.
CBA inam msaidiaje mwananchi kibarua chake kilichoota Nyasi?
 
Mmiliki wa kiwanda cha tumbaku amekimbilia Malawi kuendesha biashara hiyo. Bongo haieleweki.
Na kule amefungua kiwanda Cha kuchakata bange,sio tumbaku.malawi bange ndo dili kwa sasa,serikali ya Malawi iliruhusu watu kulima zao la bange tangu mwaka juzi.na bange yote ya Malawi inapelekwa nje.
 
Tumbaku kilifungwa kwa sababu malowezi Zimbabwe wamerudi kulima tumbaku so cheap tumbaku plus utawala wa jk pinda alidanganywa na wezi wakachukua tenda ya pembejeo, yaani kwa ufupi mchawi ni serikali iliyopita na siyo jpm
Mtamtetea lakini ukweli utabakia pale pale, muuaji mkuu wa uchumi wa Tanzania ni Magufuli.

Ameua kuanzia biashara, kilimo, viwanda, utalii mpaka uwekezaji.

Sahizi amebakia kukimbizana na wafuga kuku, wanunua vocha, wachimba visima na wamiliki wa nyumba vijijini ili kupata kodi. Watu ambao alistahili kuwainua yeye ndiyo anawamalizia kabisa.
 
Tumbaku kilifungwa kwa sababu malowezi Zimbabwe wamerudi kulima tumbaku so cheap tumbaku plus utawala wa jk pinda alidanganywa na wezi wakachukua tenda ya pembejeo, yaani kwa ufupi mchawi ni serikali iliyopita na siyo jpm
Mkuu hivi awamu iliyopita ilikuwa chini ya Chadema?

Kama ilikuwa chini ya chama hicho hicho ambacho kinaongoza sasa mtakwepa vipi lawama?!
 
Ila abood amekuwa aklishambuliwa mara nyingi sana kila mkuu akipita moro sijui kuna nini nyuma ya pazia! lazima kuna kitu. Au jamaa alikuwa upande wa Lowasa kipindi kile?
 
Back
Top Bottom