Rais Magufuli: Mbunge wa Morogoro ndugu Abood alikaa na viwanda viwili bila kuviendeleza

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Rais Magufuli amesema mbunge wa hapa ndugu Abood alichukua viwanda viwili bila kuviendeleza.

Amesema kuwa Mbunge wa Morogoro alichukua viwanda viwili Moprocco na Calvaly,amesema kiwandacha Moproco kilikuakinahusisha na utengenezaji wa mafuta ya kula hapo Morogoro.

Amesema Abood amekaa na viwanda hivyo kwa muda wa zaidi ya miaka 25 bila kuviendeleza mpaka kimoja kilipouzwa na kununuliwa na CRDB, nao CRDB nao wamekaa nacho bila kukiendeleza.

Rais Magufuli amesema anataka kiwanda hicho CRDB wakiendelezena si kukaaa nacho, ameagizwa wizara ya viwanda kufatilia viwanda hivyo ili siku moja aende kufungua kiwanda cha Moproco kitakachozalisha mafuta hapo Morogoro.

Rais Magufuli amesema anamsema hadharani mbunge huyo kwa kuwa kukaa na kiwanda bila kukiedeleza ni kuwanyima fursa ya ajira watanzania.

Rais Magufuli amemwagiza Waziri wa viwanda kuwanyang'anya wale wote ambao wamekaa na viwanda bila kuviendeleza. amesema huu ndi wakatiwa kutekeleza agizo hilo maana yeye bado yupo kwani akiondoka yatarudi yaleyale.

=======
Mororgoro ilikuwa ni source ya emplyoment ya watu wengi kwenye miaka ya 1999 ndipo ubinafsishwaji wa viwanda sera hiyo ilipokuja viwanda vingi vikabinafsishwa.

Na ndio maana leo nampongeza sana mh. Rostam kweli nakupongeza kwa sababu ndugu yako mbunge wa hapa alichukua viwanda viwili akashindwa kuviendeleza na mimi huwa ni mkweli nazungumzaga uwazi.

Ndugu Rostam alichukua viwanda vikubwa viwili cha Calvary pamoja na kingine kilikua kinatengeneza mafuta ya kupikia cha Moprocco mafua ya awali yalikua yanatengenezwa hapa.

Mbunge wetu na mimi nakusema hadharani huu ndio ukweli na mimi nitabaki kusema ukweli nasema uongo ndugu zangu amekaa na viwanda vya Calvary pamoja na Moprocco kwa zaidi ya miaka 25 kile kingine kikaja kikauzwa na CRDB nataka kuyasema haya kwa sababu niko Morogoro CRDB nao wamekaa nacho.

Waziri wa viwanda na Naibu Waziri wa viwanda nataka CRDB nao wahahakikishe kiwanda hiki cha Calvary eidha wanawapa mtu bure au wakiendeshe wao kianze nacho kufanya kazi kama hiki cha Rostam kinavyofanya kazi.

Na kile kiwanda cha Moprocco ambacho ndugu Abood ulinyang'anywa najua kiko mikononi mwa hazina wizara ya fedha wasihangaike hata kuleta waraka kwenye cabinet watafute muwekezaji nije niitwe kufungua kiwanda kitengeneze mauta kwa ajili ya kutoa ajira kwa watu wa Morogoro na watanzia, nilifikiri hata uje ugombee ubunge hapa umtoe huyu aliewanyima ajira watanzania.

Lakininajua ndugu Abood hili liwe funzo kwake viwanda vile vimeniuma mno kukaa navyo miaka zaidi ya 24 bila kuviendelezana vimekufa na wewe ni mbunge wa CCM, kwa hiyo leo Ndugu Rostam nakupongeza huyu leo simpongezi japo jana nilimpongeza ingawaje jana nilimpongeza ya kwenye viwanda ndugu Abood hujafanya vizuri, nikiondoka Morogoro bila kusema hili nitakuwa mnafiki.

Abood amekaa na kiwandaa wee akaenda kukopamabasi amekaa nacho wee kinakufa na sasa tunaagiza mafuta nanchi hii si ya kwenda kuagiza mafuta lakini viwanda tuliviua sisi wenyewe na kwa Morogoro aliviua Mbunge Abood.Kwa leo Mbunge utanivumiliajana ulikua vizuri lakini kwa leo ni mabaya.






 
Balaa
1613134967681.png
 
Bilioni 10 alizozitoa Obama kuvisaidia viwanda kama canvas hawajapewa,ulikuwa karibu na uchaguzi zilienda wapi?kiwanda kimeshindwa kwa sababu asilimia 90 ni export, wenzetu wa india, pakistan wanapewa ruzuku ya asilimia 50 huku kwetu ujitegemee,utaweza kweli kushindana?
 
Rais Magufuli amemwagiza Waziri wa viwanda kuwanyang'anya wale wote ambao wamekaa na viwanda bila kuviendeleza. amesema huu ndi wakatiwa kutekeleza agizo hilo maana yeye bado yupo kwani akiondoka yatarudi yaleyale.
Hapa ndipo tunakwama na kujikwamua lazima viongozi wetu wajifunze wajenge mfumo endelevu. Rais wa China akiondoka leo, bado dira ya taifa hilo haitabadilika kitachoweza badilika ni mikakati tu ya utekelezaji.
 
Morogoro, Arusha, Tanga, Kilimanjaro viwanda vilikuwepo, vijana hawakuwa idle kama Sasa walikua na mambo ya muhimu ya kufanya.

Ila kwa sasa bongo fleva ndio kiwanda kipya kwa vijana.

Ni mwendo wa sukari tu na nyinginezo.
 
Bilioni 10 alizozitoa Obama kuvisaidia viwanda kama canvas hawajapewa,ulikuwa karibu na uchaguzi zilienda wapi?kiwanda kimeshindwa kwa sababu asilimia 90 ni export ,wenzetu wa india,pakistan wanapewa ruzuku ya asilimia 50 huku kwetu ujitegemee,utaweza kweli kushindana?

Hivi viwanda wamevichukua vinafanya kazi. Vimekufa mikononi mwao. aibu sana. Tunaagiza kila kitu bila sababu ya maana
 
Amenena vizuri mheshimiwa rais

Kuchukua kiwanda toka serikalini na kutokitumia ni tamaa mbaya isiyo na kichwa wala miguu
 
Tangu lini Mbunge ndiye anayehusika kuendeleza viwanda? Anaogopa nini kulaumu Serikali ambazo yeye alikuwemo ya tatu na ya nne na miaka sita yeye kafanya lipi zaidi ya ngojera zake tu zisizo kichwa wala miguu!? 😳
 
Amenena vizuri mheshimiwa rais

Kuchukua kiwanda toka serikalini na kutokitumia ni tamaa mbaya isiyo na kichwa wala miguu

..serikali walitakiwa wakae pamoja na Aboud ili kujua ni changamoto gani zimemkuta mpaka akashindwa kufufua viwanda alivyouziwa.

..Aboud siyo mjinga mpaka aache kuchangamkia fursa ya kufufua kiwanda na badala yake akajikite kwenye biashara ya usafirishaji.

..vilevile mfanyabiashara kubadilisha aina ya biashara siyo jambo la ajabu. wafanyabiashara na wawekezaji wakiona biashara fulani hailipi huamua kufanya biashara nyingine.
 
Huyo Rais atujuze , ninani aliye sababisha kiwanda cha kusindika tumbaku na kile cha kutengeneza jezi morogoro vikafungwa awamu ya uongozi wake kama siyo Sera mbovu za kodi za serikali awamu ya tano. Na aondoke tu aje mwingine atengeneze uchumi
 
Kwani namba zake za simu alikuwa hana ampigie na kumwambia sasa kuja kujiongelesha mbele za watu ndo alichobakia nacho no reasoning skills at all anaona wabongo ni wale wa zama za mawe
 
Kwani namba zake za simu alikuwa hana ampigie na kumwambia sasa kuja kujiongelesha mbele za watu ndo alichobakia nacho no reasoning skills at all anaona wabongo ni wale wa zama za mawe
Ile ni mali ya Uma na sisi kama wenye nchi tunapaswa kupewa taarifa kuhusiana na mali zetu.

Rais ndio custodian wa mali za nchi hivyo ana mamlaka ya kuaccount kwa Kila moja wapo.

Kama wewe hutaki sikia hizo taarifa, achana nazo tu wengine tunahitaji kusikia.
 
Tangu lini Mbunge ndiye anayehusika kuendeleza viwanda? Anaogopa nini kulaumu Serikali ambazo yeye alikuwemo ya tatu na ya nne na miaka sita yeye kafanya lipi zaidi ya ngojera zake tu zisizo kichwa wala miguu!?
Mkuu hata huna unalolijua kwenye huu mjadala zaidi ya mihemko yako ya uchadema na uccm.

Hapa abood alaumiwi kama mbunge wa jimbo ila analaumiwa kama mmiliki wa hivyo viwanda ambavyo alivichukua toka serikalini na kushindwa kuviendeleza.
 
Wacha ujinga wewe! Hiyo miaka yote Serikali ilikuwa wapi hadi ikafika miaka 25? 😳😳😳
Mkuu hata huna unalolijua kwenye huu mjadala zaidi ya mihemko yako ya uchadema na uccm.

Hapa abood alaumiwi kama mbunge wa jimbo ila analaumiwa kama mmiliki wa hivyo viwanda ambavyo alivichukua toka serikalini na kushindwa kuviendeleza.
 
Back
Top Bottom