Rais Magufuli afungua kiwanda cha Ace Leather kinachomilikiwa na Rostam Aziz mjini Morogoro

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
43,475
2,000
Rais Magufuli anafungua kiwanda cha ngozi kinachomilikiwa na tajiri maarufu nchini Dr Rostam Aziz Kihonda mkoani Morogoro.

Tukio liko mubashara TBC Channel ten na ITV


Up dates;

Rais Magufuli amemtaja Mbunge wa Mororogo Mjini, Aziz ABood kuwa alipewa kiwanda cha Canvas na Moproco tangu mwaka 1996 ambavyo alivishindwa hadi aliponyang'anywa mwaka 2020. Ambapo kwa sasa wamepewa watu wengine

Aidha ametaka atafutwe muwekezaji kupewa kiwanda cha mafuta cha Moproco ili kutoa mafuta kwa ajili ya watanzania.

Magufuli amwambia Rostam Aziz aende kugombea ubunge Morogoro ili amtoe Aziz Abood.

----
Magufuli amsema Abood kuwa alimilikishwa viwanda ambavyo alitumia kuchukua mikopo ambayo alitumia kununua magari na sio kuendeleza viwanda vya Moproco na Canvas

Kiwanda cha Rostam Aziz kinatarajia kuajiri watu 1000

=====

Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameagiza Serikali kuchukua viwanda kutoka kwa wawekezaji ambao wamepewa na kushindwa kuviendeleza

Amesema, "Waziri wa Viwanda usichelewe wala usiulize, inawezekana hata wapo viongozi wengine wa CCM walijimilikisha kwa chini chini, nyang'anya"

Ameagiza hayo Mkoani Morogoro wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha Ngozi cha Ace Leather Tanzania Limited akisema Serikali inataka Watanzania wapate Ajira. Vilevile amesisitiza Tanzania ni sehemu bora zaidi kufanya uwekezaji

Rais John Magufuli amesema Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdul - Aziz Aboud amekaa na viwanda, akakopea fedha na kununua mabasi huku viwanda vikifa. Ameongeza kuwa, hata Wafanyakazi wakawa wanakufa na yeye anawabeba kwenye mabasi kwenda kuwazika

Ameeleza hayo mapema leo wakati akizindua Kiwanda cha Ngozi ambapo amesema "Ninampenda sana Aboud lakini kwenye Viwanda hapana. Kwa Morogoro aliviua Mbunge wetu"

Amesema Mbunge huyo ameshindwa kuendesha Viwanda viwili vikubwa ambavyo amekaa navyo kwa zaidi ya miaka 25.
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
11,087
2,000
Rais Magufuli amemtaja Mbunge wa Mororogo Mjini, Aziz ABood kuwa alipewa kiwanda cha Canvas na Moproco tangu mwaka 1996 ambavyo alivishindwa hadi aliponyang'anywa mwaka 2020. Ambapo kwa sasa wamepewa watu wengine


Magufuli amwambia Rostam Aziz aende kugombea ubunge Morogoro ili amtoe Aziz Abood.
Huyu ndio Rais John Pombe Joseph Magufuli ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ
Mwenyekiti wa Chama cha mapindunzi chama tawala
Abood ajitafakari na kuchukua hatua๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom