Swali: CCM ni Chama Cha 'Mapinduzi' Yepi?

Hujui mbona unauliza swali rahisi. CCM ni Chama Cha Mapinduzi, Mapinduzi ya Demokrasia na kuwa Mapinduzi ya MAFISADI. Ndiyo maana Kipo kwa masilahi ya MAFISADI. Hivyo imepindua Demokrasia.
 
Wadau,

Nimekuwa nikijiuliza na sijapata majibu murua yenye kunikidhi juu chama kinachotutawala hapa TZ.
  • Ya kwamba sioni tafsiri halisia juu ya 'mapinduzi' kutumika kwa chama hicho kinachotawala.
  • Ya kwamba je, iliwahi kutokea mapinduzi Tanganyika kupelekea neno 'mapinduzi' kuwepo kwenye alama ya bendera yao tangu enzi za mwalimu mpaka sasa?
  • Iwapo hatukuwa na mapinduzi...kwa nini neno hilo liwepo tangu enzi ya chama kimoja? Je kuna siri gani imefichika?
  • Ama neno hilo limeibeba Zanzibar na ni kielelezo cha alama ya muungano na kutambua kiitwacho mapinduzi 'MATUKUFU' ya znz?
  • Iwapo nchi yetu inatambulika ki-ngonjera kuwa ni kisiwa cha amani...kwa nini neno mapinduzi/revolution litumike kwa chama tawala toka enzi za mwalimu?
Naomba nisaidiwe ili niondoe ukungu na tongotongo waungwana, NAOMBA KUWASILISHA.
 
Good question!

Tusubiri wenye chama watasemaje, tatizo la zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama!

kwa kebehi za kisiasa tunasema; mapinduzi yaliyofanyika ni kumtoa mkoloni mweupe na wao KUTAWALA kama wakoloni weusi....mapinduzi mengine ni kundoa mfumo wa vyama vingi uliokuwepo tangu 1961 na kuleta mfumo wa chama kimoja......
 
Waberoya, ahsante. Lakini bado hatujajua kwa nini 'chama cha mapinduzi'. Kilipindua nini? ASP na TANU si viliungana ndio kikazaliwa? Kuna wenye umri ambao watatusaidia.
 
Good question!

Tusubiri wenye chama watasemaje, tatizo la zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama!

kwa kebehi za kisiasa tunasema; mapinduzi yaliyofanyika ni kumtoa mkoloni mweupe na wao KUTAWALA kama wakoloni weusi....mapinduzi mengine ni kundoa mfumo wa vyama vingi uliokuwepo tangu 1961 na kuleta mfumo wa chama kimoja......

Aya hebu tusubiri matusi na kejeli
 
Aya hebu tusubiri matusi na kejeli

Chama cha Demokrasia na Maendeleo-
1. Kuna demokrasia gani chadema kwani wanawake viti maalumu wanachaguliwa kwa formula aliyo iandaa dr Kitila,Zitto alipogombea Uenyekiti wa Chama ikabidi Mtei na Wazee wengine wakatishia kumvulia nguo!
2. Maendeleo yepi kama Chama kinajiita kikubwa kwa Upinzani kina ruhusu wabunge wake wachukue milion 90 wakati wakijua maisha ya mtanzania yako hoi!
 
Kwa hali ya kisiasa Tanzania ya leo, inabidi uwe mwendawazimu kujaribu kuelezea haya mambo ya sisiemu.
Hayo mapinduzi yalikuwepo wakati ule na wazee wenzangu tuliocheza HALAIKI na CHIPUKIZI watakubaliana nami.
 
Guys, I just told you so..... hawatajibu hoja, hawana uwezo huo na hawajazoea
 
Good News ni kuwa hawa waliomo kwenye Chama hiki na huko historia inavyojionyesha ni cha kupigania uhuru, leo hatukihitaji tena kwani tumeshajikomboa na sasa tupo Nchi huru. Muda wake wa kuwepo madarakani umekwisha kama hakitaki kujiuzulu ni lazima kwa hali yeyote ile kiuzuliwe na kuwajibishwa, wanaotaka kuendeleza siasa za kujenga nchi ambao wamo katika chama hicho kilichotukomboa kutoka kwa mkoloni wajiunge na vyama vya siasa ya kujenga nchi. Mwisho wa CCM ulikuwa ni siku ile ilipopita sheria ya kuruhusu vyama vingi vya siasa.

Hiki Chama Cha CCM ni Chama ambacho wengi wa WaTanzania walikuwa nacho na ilikuwa ndio Chama chao, habari zake zikisomeshwa hata mashule, kwa leo hakina umuhimu na kimeshafulia, kinaongoza kama kinafanya harakati za kugombea uhuru kwa mtutu wa bunduki.

Mali zote za Chama hiki ni za WaTanzania wote, kumbuka baada ya kuanzishwa kwa Vyama vingi, ilitakiwa maliza zake zote zikabidhiwe kwa serikali kwani ni mali za WaTanzania wote.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-
1. Kuna demokrasia gani chadema kwani wanawake viti maalumu wanachaguliwa kwa formula aliyo iandaa dr Kitila,Zitto alipogombea Uenyekiti wa Chama ikabidi Mtei na Wazee wengine wakatishia kumvulia nguo!
2. Maendeleo yepi kama Chama kinajiita kitikubwa kwa Upinzani kina ruhusu wabunge wake wachukue milion 90 wakati wakijua maisha ya mtanzania yako hoi!

swali ni nini maana ya CCM? mapinduzi ya nini? unachosema Zitto, Kitila si wako chadema?
 
Mwiba, umeokoka?

Kweli uko vizuri kamanda. Katika watu nilikuwa najua ni wavaa mashati ya kijani ni wewe. Ila nimekukubali.
 
Ni heri kipindi cha mwalimu mambo yalikuwa yanaenda na kiongozi aliyekuwa mkt wa ccm wananchi walikuwa wanamwamini hata akiwa anaongea wanamuelewa lakini hivi sasa,wanaccm weneyewe hawamwamini kiranja mkuu wa ccm

kunasababu ya kumfanyia mapinduzi kiranja mkuu.
 
Kwa hali ya kisiasa Tanzania ya leo, inabidi uwe mwendawazimu kujaribu kuelezea haya mambo ya sisiemu.
Hayo mapinduzi yalikuwepo wakati ule na wazee wenzangu tuliocheza HALAIKI na CHIPUKIZI watakubaliana nami.

Mkuu,
Ndio maana ukiwa ni kijana wa zamani...chonde tujulishe kwa nini 'mapinduzi'? Kipi kilifanyika mpaka ifikie kuwepo neno mapinduzi? Nchi iliyo ni 'kisiwa cha amani' katu hakuna chembe za lakabu ya mapinduzi katika utambulisho wa kitaifa. KULIKONI?
 
bado wana jamvi mimi kama mwanaharakti na kufikilia baada ya mwalimu kuhakikisha kua nchi na kisiwa vianungana na kwa kua katika article of union kulikua na makosa kwanza kuungana kwa vyama kulikuja ili kupata sehemu moja ya kushika ila upande wa pili walitaka heshima yao isife hivyo wazee ili kuitiliza zanzibar wakaamua histpria isifutike ya mapinduzi na hivyo kuamua kua chama kitakacho undwa lazima kiwe na neno hilo kama moja ya masharti ya muungano na kwa kua mwalimu alitaka alilazimika kuwakubalia ila hakuna zaidi ya kukubali maombi ya zanzibar rejea kitabu cha kwa heri ukoloni na kwa heri uhuru na baada ya hapo nini kilitokea kabla ya muungano na kwa nini mwalimu alisafili usiku baada ya kua amemtuma AG na mkataba uko kwa kizungu wakati karume hakujua lugha hiyo na hata mwanasheriia wake hakuingia
 
Well, nilipitia Chipukizi miaka hiyo - bado ninazielewa itikadi za CCM. Mapinduzi yako ya aina nyingi na siyo lazima yawe ya kuuondoa uongozi fulani na kuweka uongozi mwingine kwa nguvu.
Chama cha Mapinduzi ni chama kilichoanzishwa ili kuleta mapinduzi ya kilimo na viwanda nchini (jembe na nyundo). Tulianza kuongeza nguvu za kupambana na adui zetu watatu wa maendeleo na kujenga viwanda ikiwa ni pamoja na kuimarisha mashirika ya umma kama MECCO, ATC, TTCL n.k Katika kipindi hicho tulijenga viwanda vingi na kuongeza tija ya kilimo na mazao yatokanayo na kilimo au mifugo kama ngozi n.k
Kwa ujumla mapinduzi yanayoelezwa katika chama (CCM) ni mapinduzi ya kifikra na kiutendaji kwa maana ya kuweka misingi sahihi ya kujitegemea kama nchi. Tulikuwa na dira, dhamira na nia safi ya kuleta maendeleo ya haraka kwa jamii. " Wenzetu wako mbali hivyo kama wanatembea sisi inabidi tukimbie" - J.K Nyerere. Tuliangalie neno mapinduzi kwa maana hiyo ... kuwa ni chama kitakachotuongoza katika kubadili mfumo tuliourithi toka kwa wakoloni na kuweka mfumo mpya wa haki, usawa na maendeleo ya kisayansi na Teknolojia kwa mwelekeo wa kujitegemea. Hayo ndo mapinduzi yanazozungumzwa na chama (CCM).

Well, naomba nisiulizwe maswali tena kuwa nini kimetokea katika hizo dhamira, nia n.k.... Chama kilibadili haya mambo mwaka 1992 katika azimio la Zanzibar. Sijui kinachoendelea maana si mwanachama tena baada ya mabadiliko hayo!!
 
bado wana jamvi mimi kama mwanaharakti na kufikilia baada ya mwalimu kuhakikisha kua nchi na kisiwa vianungana na kwa kua katika article of union kulikua na makosa kwanza kuungana kwa vyama kulikuja ili kupata sehemu moja ya kushika ila upande wa pili walitaka heshima yao isife hivyo wazee ili kuitiliza zanzibar wakaamua histpria isifutike ya mapinduzi na hivyo kuamua kua chama kitakacho undwa lazima kiwe na neno hilo kama moja ya masharti ya muungano na kwa kua mwalimu alitaka alilazimika kuwakubalia ila hakuna zaidi ya kukubali maombi ya zanzibar rejea kitabu cha kwa heri ukoloni na kwa heri uhuru na baada ya hapo nini kilitokea kabla ya muungano na kwa nini mwalimu alisafili usiku baada ya kua amemtuma AG na mkataba uko kwa kizungu wakati karume hakujua lugha hiyo na hata mwanasheriia wake hakuingia

Safi sana mkuu,
Swali langu jipya...je ni wapi ulipo UWAKILISHI wa m-Tanganyika katika chama hicho tawala ambacho kimeshika hatamu bara & visiwani?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-
1. Kuna demokrasia gani chadema kwani wanawake viti maalumu wanachaguliwa kwa formula aliyo iandaa dr Kitila,Zitto alipogombea Uenyekiti wa Chama ikabidi Mtei na Wazee wengine wakatishia kumvulia nguo!
2. Maendeleo yepi kama Chama kinajiita kikubwa kwa Upinzani kina ruhusu wabunge wake wachukue milion 90 wakati wakijua maisha ya mtanzania yako hoi!

Mkuu,

Mbona unajaribu kupindisha hoja? Jibu issues ambazo mtoa hoja ameleta halafu na wewe ukitaka uje na post yako ya hayo uliyoyasema. We need to be consistency my dear!!!!

Tiba
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom