Sutco Dar - Iringa Badilikeni, acheni kiburi

Sutco Dar - Iringa Badilikeni, acheni kiburi

Kaudunde Kautwange

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2011
Posts
1,698
Reaction score
1,783
Nimekuwa mteja wa basi la Sutco la Dar - Iringa kwa muda sasa, lakini naona kama hawa Sutco wameanza kulewa sifa ya kujiona wameteka soko.

Kuna basi la saa moja, hili likitoka Dar, kuna kuwa na yule wa kukagua tiketi, ambaye ni bonge fulani hivi, siku ya kwanza nilikata seat mbili, mimi huwa napandia njiani, gari kufika kituo nilichopo naingia ndani nakuta seat zangu zimeuzwa tena, tena muuzaji ni huyu bonge.. maana yeye ndio anawapanga abiria wa njia wasio na tiketi.

Sikukubali, nilipambana naye hadi nikapata seat zangu, maana alianza kuleta habari za kutaka kunitafutia seat zingine.

Leo tena, nimekata tiketi toka Ijumaa, safari ya Jumapili.. tena mimi ndio nilikuwa wa kwanza kuzindua hiyo chati.

Kama kawaida yake huyu Bonge, nikakuta seat yangu ameuza tena, eti ananiambia huyu dada ni mgonjwa ndio maana tumempa hii seat, aisee.. Jamaa alinikera sana.. imebidi niwe mstaharabu maana mule ndani nilikutana na watu ambao nafahamiana nao na tunaheshimiana sana, nikawa mpole, nikapewa seat ya nyumaa kabisa.

Sasa wewe Bonge na Sutco yako, hii ni mara ya mwisho, next time aisee itakuwa ishu nyingine.

SUTCO DAR - IRINGA BADILIKENI, TABIA YA KUUZA SEAT ZA WATU WAKIO WAHI KUKATA TIKETI SIO NZURI..
 
Angalia kwenye tiketi zao kuna mawasiliano yao ni vema ukawapa hii taarifa itawasaidia sana SUTCO kuboresha huduma zao.
 
Hiyo route kwani ina Basi moja tu?
 
Angalia kwenye tiketi zao kuna mawasiliano yao ni vema ukawapa hii taarifa itawasaidia sana SUTCO kuboresha huduma zao.


Unaweza kuona unayempigia ndiyo huyohuyo Bonge, sidhani kama zile namba ni za wamiliki wa hayo mabasi, niliwahi kulalamikia kero nyingine lakini kamwe haikufanyiwa kazi,

Kwa wingi wa kadhia hizi kwa wasafiri nadhani SUMATRA walitakiwa kuwa na page ya kupokelea malalamiko ya abiria na waweke mrejesho wa namna walivyoshughulikia kero za walalamikaji husika

Kadhalika hapa JF kungekuwa na forum maalumu ya wasafiri ili kuzirahishia mamlaka zenye kigugumizi kama SUMATRA
 
Namaanisha hiyo route haina Kampuni ingine?


Zipo ila mabasi yenyewe yapo hoi bin taaban, kelele za muziki ndiyo burudani pekee na kero ya upepo fukuto nk, hiyo sutco ndiyo yenye unafuu, unaweza kusema ndiyo Scandinavia ya sasa japo haiwafikii hata kwa theruthi 1
 
Kama kawaida yake huyu Bonge, nikakuta seat yangu ameuza tena, eti ananiambia huyu dada ni mgonjwa ndio maana tumempa hii seat, aisee.. Jamaa alinikera sana..


Usishangae alikariri jina lako kwenye ugomvi wa kwanza na mara hii akaamua kukuonyesha kwa style nyingine, fuatilia mkoa anaotokea husianisha na alichokifanya utajifunza kitu
 
Mbona magari yapo mengi jombaa kwani ni lazima upande hilo hilo
 
Back
Top Bottom