Ushauri wa bure haswa kwa vijana ambao hawajaoa. Kama unatafuta mke, kwa kuanzia chagua tuu iwe sura au umbo, uzuri wa mke ni tabia.
Kwa ajili ya starehe na raha zako kama unapenda sura bomba ukiipata utajiona tuu ka unafaidi na mengine yote kwa sababu moyo wako ushapenda hiyo sura uliyoipenda.
Wapenda body ni wwatu wa shughuli, akiipata bodi anayoipenda atajiona anafaaidi kwa vile moyo hicho ndicho upendacho.
Kwa uzoefu wangu ambao una long expirience ya uzowefu wa muda mrefu,ukifanikiwwa kupata kimojaa, kingine kinapungua. Hivyo ni uamuzi binafsi uko radhi kucompromise nini. Kuna watu wanafuraha machoni mbele za watu. Kumbe wakifunga tuu mlango wa chumbani, ni kituo cha polisi!. Ndio maana hutashangaa kuona watu wa heshima na ndoa zao, tena wake zao bomba, lakini utawakuta wanakuja Jolly Club, Bills na Kona Bar kuhangaikia mazagazaga. Unaishia kujiuliza huyu jamaa vipi!?.
Nikiwa kijana mdogo, nilipenda sana sura, nywele na miguu. Nikapata nikakuta idara nyingine hazijatimia. Kuna kipindi nilikula sambamba na mamiss wa mchujo kuelekea miss Tanzania, ohh.. Unapata sura bomba na vifiga vikali vikali mbele ya watu unatamba na kusifiwa, tatizo ni hukoo.. Hakuna kitu.
Nilipojikuta nimedondokea mahali hakuna sura, hakuna figure, hakuna nywele wala mguu ila ni asali!. 'penye asali ndio penye ulimbo', nilinasa na nilifanya uamuzi wa kuchukua jumla japo baadae uamuzi huo ulinitokea puani... nimekuja kuishia uamuzi wa busara kuwa 'kama ni mke, tafuta tabia na hayo mengine yote yatajiseti'.