Suprise nyingine hazifai...

Mbilimbili

Senior Member
Mar 17, 2012
172
19
Habari za hapa: kwenye mahusiano hasa kipindi cha urafiki wa kimapenzi, kila mtu huwa anajitahidi kufanya mambo kwa kushtukiza (suprise). Hii imenitokea weekend iliyopita lakini imeniweka kwenye wakati mgumu, mpenzi wangu wa kike alinizimia sim Ijumaa jioni hadi kesho yake saa tatu asubuhi. Baada ya kumbahatisha hewani alinieleza kuwa ni "Suprise" alinifanyia, nilikasirika ila sikumwambia chochote nikakata sim. Tokea hapo hadi jumapili asubuhi hatukuwasiliana kabisa, nilipokwenda kanisani tukawa tumefundishwa juu ya msamaha. Ndipo nilipotoka tu nje nikamtumia txt kwamba "suprise zimekwisha" hakunijibu chochote. Niliamua kumpigia baada ya nusu saa hivi, akanijibu Nashukuru. Lakini tokea hapo mawasiliano sio mazuri, nikipiga sim wkt mwingine haipokelewi wala baadhi ya txt hazijibiwi. Nifanyeje kwa hili? Roho inaniuma kwa kuwa ninampenda sana huyu binti!
 
kwani huyo binti njia pekee ya kuwasiliana nae ni kupitia simu tu, mtafute physically kama una wasiwasi
 
na wewe mchunie halafu cheki reaction yake... ukimshobokea sana atakusumbua; pia fanya ushushushu kidogo kujua alikuwa wapi siku ya 'surprise' usije ukawa even more surprised...
 
Pole....ushaumia hapo. Khaa tunavyopenda mawasaliano sisi. Khaa siku nzima sijajua uko wapi unafanya nini, uko na hali gani? Haloooo oh sorry to say Ukiona manyoya............................................
 
Jina lako linafanana na visa unavyofanyiwa,akaa! afunge cm ndio suprise ndio kwanza nisikie tangu nizaliwe,nilidhani kama kwako usiku wa manane bila kukujulisha kumbe hilo! babu jinga inama ufikiri mali yako inaliwa...
 
labda anaendelea na surprise.huyo dada hiyo kwake nio njia ya kukuacha,inabidi ukubali matokeo.mapenzi mengine ni ya kimjini mjini,wewe unaweza ukampenda sana,ila yeye mwenzako ana mahesabu mengine kabisa
 
am very sapraizid ofu yua posti ofu sapraiz on hau yua GF sapraizid yu... usishangae siku akaamua kukaa mwaka mzima bila mawasiliano wala kuonana afu akaja kusema amekusapraiz.
 
hii suprise mpya jamani.........
suprise ya kuzima simu?
ndo naisikia..............

mmmmmh bado sitaki kuamini............... na wewe ukaridhika kuwa kuzima simu ni suprise? nia na madhumuni yake ni nini? uwe suprised? then what?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom