Niliwai ona kwa wafugaji magereza wakiwategea kenge mayai ya kuchemsha. Kwa maelezo yao kuwa kenge anapokula mayai hapasulii mdomoni, ulimeza na kulivunjia shingoni, sasa atapomeza yai lililochemshwa na kupoa atapojaribu kuvunja atashindwa. In short litamkaba had kufa.
😌😌 ila umenikumbusha mbali. Mzee wetu enzi zake alikuwa anapambana nao sana. Tulikuwa na mabwawa ya samaki na kuku, kenge na fisimaji walikuwa wasumbufu, basi anawategea usiku sana na mkuki, anawaua. Asubuhi anawatundika kwenye mti, basi watu wanajaa kushangaa yeye kichwa hichoooo 😌
Yani mtu saa 6 usiku katega mtoni kutegea kenge na mkuki na rungu. 🤓🤓 mabanda ya kuku yalizungukwa na kunguru aliowatundika baada ya kuwaua kwa manati.