Sumu ya kuua kunguru ni ipi?

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,627
Naomba msaada wa haraka wadau. Hivi ni sumu gani ya kuua huyu ndege mweusi kama lami na mwenye laana kubwa?

Hawa ndege ni wasumbufu sana kupita maelezo na wanakiburi sana kisicho na mashiko yoyote. Yote kwa yote ni ndege wenye kisasi sana pale wanapogundua umejaribu kuwadhuru au kuwashambulia.

Changamoto ni hapa kwenye eneo ninaloishi upande wa pili kuna mnazi wameweka kiota hapo sasa wamekuwa wasumbufu sana kwa fujo za kuchafua mazingira wanaweza toka na matakataka wameokota huko wanakuja kutupa eneo hili. Au wanaweza parua mtu bila sababu. Tunashindwa kuanika vitu kwa amani kama nguo nyeupe wanazichafua kusudi kabisa.

Wanaweza anzisha fujo juu ya paa asubuhi wakiwa wengi. Ni kero juu ya kero.

Nani anayefahamu sumu ya haraka. Maana nimejaribu kuharibu kiota chao zaidi ya mara tatu ila wanatengeneza kipya. Na nimeona wapo jike na dume ndio wamekomaa.

Sasa muda huu ni kama wamenijua wakiniona tu wanaanza kuitana kwa kelele na kujazana as if kuna mkutano wa kijiji na kufanya fujo.

Sasa nadhani natakiwa kuweka sumu niuwe huyu bibi na bwana kwenye kiota ili biashara ife. Ningeweza kukata mnazi ila sasa upo kwa jirani na jirani mwenyewe ni wale wa mama sio waelewa. Atasema mnazi unamsaidia nazi na madafu.

Naombeni ushauri wa haraka sana.
 
Changamoto ni hapa kwenye eneo ninaloishi upande wa pili kuna mnazi wameweka kiota hapo sasa wamekuwa wasumbufu sana kwa fujo za kuchafua mazingira wanaweza toka na matakataka wameokota huko wanakuja kutupa eneo hili. Au wanaweza parua mtu bila sababu. Tunashindwa kuanika vitu kwa amani kama nguo nyeupe wanazichafua kusudi kabisa.
Duuuh hao ni hatari. Maana mi ninavyowajua kunguru hata kumsogelea binadamu ni waoga.
 
Kikuweli kunguru ni changamoto. Hao viumbe wanakera mpaka basi.

Kuna mtu aliwahi kuniambia eti hata ujaribu kuwategea sumu kwenye vyakula kama maandazi, nk! Wakila na kugundua tu kama ni sumu, basi wakiwahi kunywa maji sumu yote inapoteza nguvu! Halafu unawakuta wanadunda tu.
 
Kuna siku mwaka 2016 nikiwa na jamaa yangu maeneo ya Kinondoni, sina hili wala lile nashangaa kunguru katoka huko akaja akatua begani paaa kushtuka nikampiga na mkono akaanguka chini kumbe alikotka inaonekana alidhuriwa maana akawa hawezi tena kupaa, nikaendelea na mambo yangu ila kwa haraka niliwaza asije akawa katumwa na wazee wa kazi Kiafrika zaidi. Kunguru kumanyiokooo

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Hao ni viumbe watu walio katika vazi la kunguru. Hapo cha muhimu ni dua kwa sana.
Mmmmmmhmn kwamba ni watu wanafanya ushirikina?! Hapana boss. Hii kero haipo kwangu tu kuna sehemu zaidi ya kwangu nimekutana na hii kero ya hawa ndege. Wanausumbufu sana.

Na wamefikia hatua wamezoea watu sababu wanakaa kwenye makazi yao. Unaweza mfukuza anakutazama tu kama mnachezeza mpira wa marede.
 
Duuuh hao ni hatari. Maana mi ninavyowajua kunguru hata kumsogelea binadamu ni waoga
Hawa wameshazoea sana watu kunguru wa Dar hawana discipline hata kidogo. Anaweza kukaa juu ya bati akakukatia gogo kichwani au mgongoni, unashangaa tu paaaah kitu cha moto moto amekudondoshea wao wanahisi maisha ni mchezo mchezo hawa ndege choko sana.
 
Kikuweli kunguru ni changamoto. Hao viumbe wanakera mpaka basi.

Kuna mtu aliwahi kuniambia eti hata ujaribu kuwategea sumu kwenye vyakula kama maandazi, nk! Wakila na kugundua tu kama ni sumu, basi wakiwahi kunywa maji sumu yote inapoteza nguvu! Halafu unawakuta wanadunda tu.
Nadhani ipo sumu ambayo inaweza kuwakomesha tena wakinywa maji ndio inazidi kukolea. Hiyo sumu haiwezi kukosekana ndio maana nikasema niweke hapa uzi mnisaidie ushirikiano wa kuwatokomeza .
 
Naomba msaada wa haraka wadau. Hivi ni sumu gani ya kuua huyu ndege mweusi kama lami na mwenye laana kubwa?

Hawa ndege ni wasumbufu sana kupita maelezo na wanakiburi sana kisicho na mashiko yoyote. Yote kwa yote ni ndege wenye kisasi sana pale wanapogundua umejaribu kuwadhuru au kuwashambulia.

Naombeni ushauri wa haraka sana.
TAFUTA CHUMVI YA MAWE WAPIGE NAYO WATAKIMBIA UTAKUJA KUNISHUKURU
 
Kwa sumu ni vigumu kuwaua, hata ukiuwa wachache has a wadogo wengine watastuka tu.

Kuna miaka walikuwa kero kwa Da es salaam na pwani nzima mpaka ''Kunguru wa Zanzibar'' likawa sasa ni suala la kitaifa na serikali ndio ikawa inadeal nao

Kuna Mzee mmoja alikuwa anawatega zaidi ya 300 kwa siku kwa wavu mpaka akawa analipwa na serikali

Njia pekee ya kuwamudu ni kwa kuwatega na wavu
 
Kwa sumu ni vigumu kuwaua, hata ukiuwa wachache has a wadogo wengine watastuka tu.

Kuna miaka walikuwa kero kwa Da es salaam na pwani nzima mpaka ''Kunguru wa Zanzibar'' likawa sasa ni suala la kitaifa na serikali...
Mmmmmmhmn. Aiseee hawa ndege wanalaana na ni wazi wanatakiwa kutokomezwa maana sio wastaarabu. Nadhani haijashindikana kuwatokomeza ila ni vile hatujaamua kwapamoja wakazi wa Dar kuwamaliza.
 
Mmmmmmhmn. Aiseee hawa ndege wanalaana na ni wazi wanatakiwa kutokomezwa maana sio wastaarabu. Nadhani haijashindikana kuwatokomeza ila ni vile hatujaamua kwapamoja wakazi wa Dar kuwamaliza.
Sasahivi wamepungua sanaaa, kuna wakati walikuwa kero mpaka kwenye vibanda vya chips wananyakua watu misosi

Ifanyike kampeni tokomeza kama miaka ile ya 2000's

Na ni Mzee Ruksa ndio aliwaleta huko pwani kutoka India
 
1668602210927.png

Ni hao hapo juu au wa kwako wapo vipi ?...,

Mimi huku wapo wachache na wanafanya kazi yao katika ecosystem ipasavyo kwa kula mizoga ya hapa na pale..., wala hawana shida..

Unajua sometimes nawaza labda binadamu ndio virusi..., kuna mdau alikuja eti tumbili wanamsumbua kwenye shamba lake na nyumba yake, nilivyofanya research kumbe yeye ndio kawavamia kwenye makazi yao...

Nadhani hawa viumbe wengine kama wangeweza kukaa na kujadili mustakabali wa maisha yao wangetuona sisi binadamu kama virusi tu (yaani mchanyato wa Corona na Ukimwi)
 
Umeharibu kiota zaidi ya mara 3 wakatengeneza tena hapohapo?
Yeah ni kwenye mnazi. Wanafanya kuhama upande wa kuweka kiota. Mara ya kwanza nimeuwa makinda matatu. Mara ya pili na tatu nimepasua mayai. Naona wamejenga tena na watakuwa wametaga.
 
View attachment 2418563
Ni hao hapo juu au wa kwako wapo vipi ?...,

Mimi huku wapo wachache na wanafanya kazi yao katika ecosystem ipasavyo kwa kula mizoga ya hapa na pale..., wala hawana shida..

Unajua sometimes nawaza labda binadamu ndio virusi..., kuna mdau alikuja eti tumbili wanamsumbua kwenye shamba lake na nyumba yake, nilivyofanya research kumbe yeye ndio kawavamia kwenye makazi yao...

Nadhani hawa viumbe wengine kama wangeweza kukaa na kujadari mustakabali wa maisha yao wangetuona sisi binadamu kama virusi tu (yaani mchanyato wa Corona na Ukimwi)
Sio aina hii. Hao wastaarabu na hawana noma kwanza hawapo Dar.

Ni wale weusi mwili mzima. Wale ni wakorofi na hawana faida mazingira yetu haya. Ni wakorofi hata wakitokomezwa hakuna wa kuwamiss.
 
Aaaah yaani CCM wana mambo ya kiwaki sana. Kila wanalofanya linageuka kuwa mikosi kwa raia.
Hao kunguru weusi wa Pwani wasio na baka jeupe asili yao ni India.

Wakati wa awamu ya pili Mzee Ruksa alienda India na kuonana na Aidha Rais au Prime Minister....sasa kule India kuna population kubwa sana mijini na jijini na wakawa wanawatumia hao kunguru kusafisha miji kwa kula mizoga na uchafu

Wakamshauri na Mzee Ruksa awalete jijini Dsm ila kaskazini na kanda zingine hawapo hao, wapo wale wenye baka jeupe shingoni ambao hata kuwaona ni nadra sana mpaka kuwe na mzoga.
 
Back
Top Bottom