Sumu inayowaua wanaume

Sumu inayowaua wanaume

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,392
Reaction score
7,863
Hapo zamani za kale, msichana mrembo alichoka na maisha yake ya ndoa na alitaka kumuua mume wake.
Siku moja asubuhi alikimbilia kwa mama yake na kumwambia:

"Mama, nimechoka na mume wangu, siwezi kuvumilia upuuzi wake tena. Nataka kumuua lakini ninaogopa sheria ya nchi itanihukumu. Tafadhali, unaweza kunisaidia mama?"
Mama yake alijibu:

"Ndiyo binti yangu, naweza kukusaidia, lakini kuna kazi ndogo unayopaswa kufanya."
Binti akasema: "Kazi gani? Niko tayari kufanya lolote ilimradi nimpate mume wangu aondoke."
Mama akasema:

1. Lazima uishi naye kwa amani ili watu wasikushuku wakati atakapokufa.
2. Lazima ujipambe na ujitunze ili uonekane mrembo na mwenye mvuto kwake.
3. Lazima umtunze vizuri, uwe mwema kwake na umshukuru kwa kila jambo.
4. Lazima uwe mvumilivu, mwenye upendo, usiwe na wivu kupita kiasi, uwe msikivu, na uwe mnyenyekevu kwake.
5. Tumia pesa zako kumsaidia na usikasirike hata kama hatakupa pesa.
6. Usimpigie kelele, badala yake himiza amani na upendo ili usitiliwe shaka baada ya kifo chake.
"Je, unaweza kufanya haya yote?" Mama aliuliza.
"Ndiyo naweza," binti alijibu kwa msisitizo.
"Sawa," mama akasema.

"Chukua unga huu na uweke kiasi kidogo kwenye chakula chake kila siku, itamuua taratibu."
Baada ya siku 30, binti alirudi kwa mama yake akiwa na huzuni na kusema:
"Mama, sina nia ya kumuua mume wangu tena. Sasa hivi nimeanza kumpenda sana kwa sababu amebadilika kabisa, sasa ni mume mzuri zaidi ya nilivyowahi kufikiria. Naweza kufanya nini kuzuia sumu hii isiendelee kumuua? Tafadhali nisaidie mama!"
Mama alitabasamu na kumwambia:

"Usijali, binti yangu. Kile nilichokupa siku ile kilikuwa tu ni unga wa manjano (Tumeric Powder). Hakitamuua kamwe."
"Kwa kweli, wewe ndiye ulikuwa sumu iliyokuwa inamuua mume wako taratibu kwa msongo wa mawazo na kutokumjali."
"Lakini ulipoanza kumpenda, kumheshimu, na kumthamini, ulimwokoa.
 
Attachments

  • mke.jpg
    mke.jpg
    40.9 KB · Views: 19

Ok
 
Back
Top Bottom