Sumaye: Msichague mafisadi mwaka huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumaye: Msichague mafisadi mwaka huu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzalendo, Oct 11, 2010.

 1. Mzalendo

  Mzalendo Senior Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Monday, 11 October 2010 07:48

  Daniel Mjema,

  Same

  WAZIRI mkuu mstaafu, Frederick Sumaye jana aliibuka hadharani na kutoa hotuba kali ya kukemea wagombea wanaotoa rushwa, akisema kuwa njia pekee ya kuwadabisha ni kuwanyima kuta Oktoba 31.

  Sumaye, ambaye alijaribu karata yake kwenye urais mwaka 2005 na kuangushwa, alisema tatizo kubwa linaloikabili nchi kwa sasa, hasa wakati wa uchaguzi ni rushwa, na hivyo akashauri wananchi watumie silaha yao ya kura kuwashikisha adabu wote wanaotaka uongozi kwa kutoa rushwa.

  Sumaye, ambaye hotuba hiyo ni kali ya kwanza kwake tangu astaafu uwaziri mkuu mwaka 2005, alisema: “Rushwa ni tatizo kubwa Tanzania hasa nyakati za uchaguzi.. lazima sote kama taifa tupige vita tukatae utaratibu wa watu wanaotaka uongozi kwa kutununua kama njugu sokoni na tuanze katika uchaguzi huu.”

  Sumaye alitoa kauli hiyo katika ibada ya kuwekwa wakfu na kuingizwa kazini kwa askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Pare, Charles Mjema na msaidizi wake, Mchungaji Timothy Msangi.

  Sherehe hizo zilihudhuriwa na maaskofu 25 kutoka ndani na nje ya nchi, wakiongozwa na mkuu wa kanisa hilo, Dk Alex Malasusa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe na viongozi wa serikali na wananchi.

  Sumaye alisema watu wanaochaguliwa kwa kutoa rushwa huwa hawawathamini wananchi wanapopata uongozi na kwamba hutumia kipindi chao cha miaka mitano kukusanya fedha nyingine kwa ajili ya kuhonga tena wananchi ili warejeshwe madarakani.

  "Hivi sasa inaonekana huwezi kushinda uchaguzi bila kuhonga wapigakura. Kwa staili hiyo mshindi anakuwa kiongozi si kwa sababu anapendwa na watu bali kwa sababu ya kununua uongozi," alisema mbunge huyo wa zamani Hanang, ambaye alikumbwa na tuhuma nyingi za kashfa wakati akielekea kuwania urais.

  “Kiongozi anayepatikana kwa njia ya rushwa yeye mwenyewe lazima ni mwizi na ni fisadi, vinginevyo hizo fedha za kuhonga angezipata wapi. Kiongozi mtoa rushwa ni mali ya watu fulani, yaani wale waliompa fedha.”

  Waziri mkuu huyo mstaafu alisema kiongozi wa aina hiyo hawezi kuwa na huruma kwani anawaona wananchi wake kama bidhaa sokoni.

  “Mimi nasema hivi; hata kama mgombea ni wa chama chako lakini unajua alihonga; hata kama na wewe hizo fedha zilikufikia na ukazila, usimpigie kura Oktoba 31. Hivyo ndio njia pekee tutakayowashikisha adabu.”

  Sumaye ambaye hotuba yake ilikuwa ikikatishwa mara kwa mara kwa makofi ya kumshangilia, alisema kiongozi anayeingia madarakani kwa rushwa atatumia miaka yake mitano kutafuta fedha za kuwahonga wananchi kwa kipindi cha pili.

  Naye Askofu Mjema alisema KKKT haishabikii chama chochote cha siasa wala mgombea lakini linao wajibu wa kuwahimiza waumini wake kuchagua viongozi watakaoweka mbele maslahi yao.

  “Tunahitaji kupata viongozi waadilifu na waaminifu. Ni aibu kwa Mtanzania kurubuniwa kiasi cha kuuza haki yake ya msingi ya kuchagua kiongozi anayefaa. Tumesikia ipo minong’ono ya watu kununua shahada hii ni dhambi,” alisema.

  Askofu Mjema alisema moja kati ya mambo yanayotoa dalili mbaya nchini ni namna neno “wapinzani’ linavyotumika kiasi kwamba wapo walioko upinzani ambao biashara zao zimehujumiwa, kutishwa maisha au kubambikiwa kesi.

  “Hii ni ishara tosha kuwa na tunaweza kufikia mahali tukakifanya kisiwa cha amani duniani (Tanzania) kikawa kisiwa cha vurugu duniani. Ni vyema Watanzania, vyombo vya dola na wanasiasa tukawa makini na jambo hili,” alisema.

  Askofu Mjema ametoa wito kwa wataalamu wa Kiswahili kutafuta msamiati mbadala wa neno “wapinzani” ambao utatumiwa na Watanzania kutambuana katika uwanja wa siasa kuliko wa sasa unaoibua hisia za mgawanyiko.

  Alipendekeza mwaka ujao uwe mwaka wa kutimiza ahadi na kurudisha mambo katika mstari na kuitaka serikali kuutumia mwaka kesho kujitathmini na kanisa linapeleka serikalini mambo ambayo hawajayakamilisha.

  Askofu huyo alisema zipo taarifa hivi sasa kuwa wawekezaji mbalimbali wanaoikimbilia Tanzania kwa ajili ya kuchukua malighafi mbalimbali wataliachia taifa hili mashimo matupu na jangwa kwa kizazi kijacho pasipo kuwaachia urithi.

  “Matatizo makubwa ya nchi za Afrika ni ukosefu wa viongozi watumishi. Wengi wa viongozi wanaoibukia katika rushwa na ufisadi kwa hiyo wanajitajirisha wenyewe na kuwaacha wananchi wao masikini,” alisema.

  Alitumia mkusanyiko huo kuzipongeza serikali za rais mstaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete kwa namna walivyojituma katika kushughulikia mgogoro wa dayosisi hiyo uliodumu kwa miaka 12.

  Askofu Mjema alisema anatumia siku hiyo ya jana kuutangazia ulimwengu kuwa mgogoro uliokuwepo sasa umekwisha na hiyo jana wachungaji wa Dayosisi ya Pare na ile iliyokuwa ikijiita ya Mwanga waliingizwa kazini kwa pamoja.

  Alihidi kutumia nafasi yake kama askofu, kusimamia na kulinda upendo na amani miongoni mwa wachungaji, waumini na wazee wa kanisa katika wilaya za Same na Mwanga na akaomba ushirikiano katika kufikia malengo hayo.  Source: Mwananchi

  Jamani mwenye macho aambiwi Tazama

  TANZANIA KWANZA
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ukitaka kujua CCM si chama cha wananchi tena utawasikia muda si mrefu CCM hao hao wakipingana na kauli hii!
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hongera Sumayi kwa kutoa mwongozo kwa wapiga kura nini cha kuzingatia wakati wa kupiga kura.Hii ni elimu nzuri ya uraia na hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi!
   
 4. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  anataka kujikosha...fisadi fisadi tuu!!
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,416
  Likes Received: 22,301
  Trophy Points: 280
  Sumaye, tunajua kuwa wewe si fisadi, lakini tunaomba uturudishie rasilimali zetu ulizotunyang'anya ulipokuwa Waziri Mkuu.
   
 6. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sumaye ni Jasiri, tunawaomba na wengine waliokuwa madarakani wasiogope kusema ukweli maana historia itawaenzi kwa kuutumikia Utaifa kuliko kujiweka kama wasiopenda kuonekana kama wanakerwa na hali hii mbaya ya rushwa wakati mioyoni mwao wanaugulia hali hii ya hatari. Tunawaomba waheshimiwa wanaoaminika kitaifa nao watoe kauli kwa wananchi kama dira kwa kuwaondolea kovu hili la rushwa ktk kupiga kura Octoba 31, wapige kura ya ushindi dhidi ya mafisadi na wala-rushwa.
  Tunawaomba akina Msuya, Warioba, Butiku, Malecela na Mzee Mwinyi watoe kauli. Wanzania wanahitaji sana kujua kama nao wapo mstari wa haki au wa uovu? Wanakaa kimya wakati vizazi vinaangamia kwa dhuluma na rushwa wao wakiona au wanageuza nyuso zao wasione au wanaziba masikio wasisikie vilio vya wamama wanaozalia manjiani na watoto wanaoangamia kwa kukosa matibabu? Wananchi watakuja kucheza juu ya makaburi yenu, na historia itawahukumu kwa ukimya wenu, na dhambi hiyo haitawaisha hata mbele za muumba wenu. Ni afadhali uwe baridi kabisa au moto kabisa kuliko kuwa vuguvungu, maana unawapeleka na wale ambao wangeokoka na laana unawapeleka katika mkondo usiowakomboa....Tunaomba kauli toka kwa Waheshimiwa hawa wastaafu na waaoaminika ili taifa lijenge imani zaidi tota katika tunu zao na kauli zao za nasaha.
   
 7. LUSAJO L.M.

  LUSAJO L.M. JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 223
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ngoja tumsikie Makamba atasemaje juu ya hili.
   
 8. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  tober 2010
  B-pepe
  Chapa
  Maoni
  Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye

  Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, amewataka Watanzania kuwaumbua viongozi wanaotumia rushwa katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kuwa vitendo hivyo ni ukiukaji wa sheria na dharau kwa wananchi.

  Sumaye alitoa rai hiyo jana katika ibada ya kumsimika Askofu wa Dayosisi ya Pare ya Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT), Charles Robson Mjema iliyofanyika katika makao makuu ya Dayosisi hiyo wilayani Same na kuhudhuriwa na viongozi na waumini wa Kanisa hilo, akiwemo Mkuu wa Kanisa hilo, Alex Malasusa.

  Sumaye alisema pamoja na mambo mengi mabaya yanayosababishwa na rushwa, hatua ya mtu kutaka kumununua mwingine kwa lengo la kupata nafasi ya uongozi huku akidai kuwa anataka kuwatumikia watu hao aliowanunua ni dharau na fedheha kubwa. Sumaye aliwataka wananchi kutokubali kufikishwa hapo kwani mtu wa aina hiyo hata kama ni ndugu yako hafai kuwa kiongozi.

  “Mimi nasema mtu anayetaka kuwanunua watu kama njugu sokoni hawezi kukumbuka kutatua tatizo lako kwani akishapata uongozi baada ya kumaliza kurudisha gharama zake ataanza kujipanga kwa ajili ya kuendeleza biashara yake ya kuwanunua tena, hivyo hafai na hata kama mmeshapewa hela na mmekula msimchague siku ya kura,“ alisema Sumaye.

  Akizungumzia migogoro inayoikabili jamii na madhehebu ya kidini, alisema haiwezekani kuitenganisha na madhambi yanayotokana na rushwa kwani kiini chake ni utendaji mbovu wa baadhi ya viongozi wanaokiuka maadili ambao asilimia kubwa ni wale waliopatikana kwa njia ya rushwa.

  Alilitaka KKKT kuongeza jitihada za kukabiliana na changamoto zinazotokana na utendaji mbovu wa baadhi ya viongozi hasa wakati huu ambao kuna mahusiano makubwa ya masuala ya kidini na kisiasa

  Sumaye pamoja na kulishauri Kanisa hilo kuona umuhimu wa kubadili mfumo wake wa kuwapata viongozi wakiwemo maaskofu, aliwataka viongozi wa dini kutochoka kuwaeleza waumini na wananchi kwa ujumla ubaya wa viongozi wanaotokana na rushwa.

  Akizungumza katika sherehe hizo, Askofu Malasusa pamoja na kuthibitisha kuwepo kwa changamoto kubwa katika kukabiliana na matatizo yanayosabishwa na utendaji mbovu wa baadhi ya viongozi, alisema Kanisa hilo limeanza mchakato wa kurekebisha mfumo wa kuwapata viongozi.

  SOURCE: Nipashe
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,364
  Trophy Points: 280

  Jamani, la kuvunda halina ubani
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sumaye si ndio kuna kipindi alikuwa na kama trillion kwenye account zake?
  Leo anawakana wenzie
   
 11. Mzalendo

  Mzalendo Senior Member

  #11
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  it takes a thief to catch a thief ndugu, kwahiyo statement ya huyu bwana inauzito sana especially mida hii,huyu bwana alikuwa waziri mkuu kwa miaka kumi, kama ni fisadi inamaana atakuwa insider mwenye nafasi kama ya Salvatore "Sammy the Bull" Gravano wa hile familia ya kihalifu ya Gambino ,
   
 12. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Anachosema ni kweli. Hakuna haja ya kuchagua mafisadi, whether wako katika upinzani au katika chama tawala. fisadi ni fisadi tu regardless yuko wapi.
   
 13. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  yeye alipewa nafasi akaichezea...sasa anataka nini...kwani hakuyajua haya tangu enzi zile??
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Hapana, atajibu Tambwe Hizza.
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha kuona CCM sasa hivi haina watu safi kujibu tuhuma.
   
 16. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Huyu hakununua wapiga kura 'enzi zake'? Au ni yaleyale tunayosikia kwa wazazi wetu wanaodai kuwa 'vijana siku hizi wameharibika, hawana adabu' nk nk, wakati wao enzi zao walitenda hayohayo na zaidi? Namshauri atubu kwanza ya kwake hadharani, kisha atafadhalishe wengine kuwa wasifuate mfano huo.
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Tenhh jk kazi unayo mwaka huu
   
 18. minda

  minda JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  sumaye amekiuka makubaliano yasiyo rasmi ndani ya ccm ya kutoshiriki katika majadiliano ya michakato ya uchaguzi kwenye jukwaa la umma wa watanzania na badala yake kuanzisha mashambulizi kutoka gizani kwa njia ya sms za uchochezi wa kidini, kikabila, na rangi na hivyo iwe rahisi kuwaweka kizuizini wanasiasa wanaopendwa na watanzania.

  sumaye anastahili kupewa athabu na kamati ya nidhamu ya chama chetu kinachoongozwa na msafi chenge.
   
 19. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tamko la Sumaye kwa kiinereza wanasema ni far reaching yaani limelenga mbali sana. Sumaye anamsema JK na kundi lake lakini ametumia nafasi kuonekana kama kwamba ni maonyo ya jumla kwa wananchi. Mlengwa hasa ni hasimu wake JK.
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  Sumaye: Msichague mafisadi mwaka huu Send to a friend Monday, 11 October 2010 07:48 0diggsdigg

  [​IMG] Waziri MKuu Mstaafu Frederick Sumaye

  Daniel Mjema, Same
  WAZIRI mkuu mstaafu, Frederick Sumaye jana aliibuka hadharani na kutoa hotuba kali ya kukemea wagombea wanaotoa rushwa, akisema kuwa njia pekee ya kuwadabisha ni kuwanyima kuta Oktoba 31.Sumaye, ambaye alijaribu karata yake kwenye urais mwaka 2005 na kuangushwa, alisema tatizo kubwa linaloikabili nchi kwa sasa, hasa wakati wa uchaguzi ni rushwa, na hivyo akashauri wananchi watumie silaha yao ya kura kuwashikisha adabu wote wanaotaka uongozi kwa kutoa rushwa.

  Sumaye, ambaye hotuba hiyo ni kali ya kwanza kwake tangu astaafu uwaziri mkuu mwaka 2005, alisema: “Rushwa ni tatizo kubwa Tanzania hasa nyakati za uchaguzi.. lazima sote kama taifa tupige vita tukatae utaratibu wa watu wanaotaka uongozi kwa kutununua kama njugu sokoni na tuanze katika uchaguzi huu.”

  Sumaye alitoa kauli hiyo katika ibada ya kuwekwa wakfu na kuingizwa kazini kwa askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Pare, Charles Mjema na msaidizi wake, Mchungaji Timothy Msangi.

  Sherehe hizo zilihudhuriwa na maaskofu 25 kutoka ndani na nje ya nchi, wakiongozwa na mkuu wa kanisa hilo, Dk Alex Malasusa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe na viongozi wa serikali na wananchi.

  Sumaye alisema watu wanaochaguliwa kwa kutoa rushwa huwa hawawathamini wananchi wanapopata uongozi na kwamba hutumia kipindi chao cha miaka mitano kukusanya fedha nyingine kwa ajili ya kuhonga tena wananchi ili warejeshwe madarakani.

  "Hivi sasa inaonekana huwezi kushinda uchaguzi bila kuhonga wapigakura. Kwa staili hiyo mshindi anakuwa kiongozi si kwa sababu anapendwa na watu bali kwa sababu ya kununua uongozi," alisema mbunge huyo wa zamani Hanang, ambaye alikumbwa na tuhuma nyingi za kashfa wakati akielekea kuwania urais.

  “Kiongozi anayepatikana kwa njia ya rushwa yeye mwenyewe lazima ni mwizi na ni fisadi, vinginevyo hizo fedha za kuhonga angezipata wapi. Kiongozi mtoa rushwa ni mali ya watu fulani, yaani wale waliompa fedha.”
  Waziri mkuu huyo mstaafu alisema kiongozi wa aina hiyo hawezi kuwa na huruma kwani anawaona wananchi wake kama bidhaa sokoni.
  “Mimi nasema hivi; hata kama mgombea ni wa chama chako lakini unajua alihonga; hata kama na wewe hizo fedha zilikufikia na ukazila, usimpigie kura Oktoba 31. Hivyo ndio njia pekee tutakayowashikisha adabu.”

  Sumaye ambaye hotuba yake ilikuwa ikikatishwa mara kwa mara kwa makofi ya kumshangilia, alisema kiongozi anayeingia madarakani kwa rushwa atatumia miaka yake mitano kutafuta fedha za kuwahonga wananchi kwa kipindi cha pili.
  Naye Askofu Mjema alisema KKKT haishabikii chama chochote cha siasa wala mgombea lakini linao wajibu wa kuwahimiza waumini wake kuchagua viongozi watakaoweka mbele maslahi yao.

  “Tunahitaji kupata viongozi waadilifu na waaminifu. Ni aibu kwa Mtanzania kurubuniwa kiasi cha kuuza haki yake ya msingi ya kuchagua kiongozi anayefaa. Tumesikia ipo minong’ono ya watu kununua shahada hii ni dhambi,” alisema.
  Askofu Mjema alisema moja kati ya mambo yanayotoa dalili mbaya nchini ni namna neno “wapinzani’ linavyotumika kiasi kwamba wapo walioko upinzani ambao biashara zao zimehujumiwa, kutishwa maisha au kubambikiwa kesi.

  “Hii ni ishara tosha kuwa na tunaweza kufikia mahali tukakifanya kisiwa cha amani duniani (Tanzania) kikawa kisiwa cha vurugu duniani. Ni vyema Watanzania, vyombo vya dola na wanasiasa tukawa makini na jambo hili,” alisema.
  Askofu Mjema ametoa wito kwa wataalamu wa Kiswahili kutafuta msamiati mbadala wa neno “wapinzani” ambao utatumiwa na Watanzania kutambuana katika uwanja wa siasa kuliko wa sasa unaoibua hisia za mgawanyiko.
  Alipendekeza mwaka ujao uwe mwaka wa kutimiza ahadi na kurudisha mambo katika mstari na kuitaka serikali kuutumia mwaka kesho kujitathmini na kanisa linapeleka serikalini mambo ambayo hawajayakamilisha.

  Askofu huyo alisema zipo taarifa hivi sasa kuwa wawekezaji mbalimbali wanaoikimbilia Tanzania kwa ajili ya kuchukua malighafi mbalimbali wataliachia taifa hili mashimo matupu na jangwa kwa kizazi kijacho pasipo kuwaachia urithi.
  “Matatizo makubwa ya nchi za Afrika ni ukosefu wa viongozi watumishi. Wengi wa viongozi wanaoibukia katika rushwa na ufisadi kwa hiyo wanajitajirisha wenyewe na kuwaacha wananchi wao masikini,” alisema.

  Alitumia mkusanyiko huo kuzipongeza serikali za rais mstaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete kwa namna walivyojituma katika kushughulikia mgogoro wa dayosisi hiyo uliodumu kwa miaka 12.
  Askofu Mjema alisema anatumia siku hiyo ya jana kuutangazia ulimwengu kuwa mgogoro uliokuwepo sasa umekwisha na hiyo jana wachungaji wa Dayosisi ya Pare na ile iliyokuwa ikijiita ya Mwanga waliingizwa kazini kwa pamoja.
  Alihidi kutumia nafasi yake kama askofu, kusimamia na kulinda upendo na amani miongoni mwa wachungaji, waumini na wazee wa kanisa katika wilaya za Same na Mwanga na akaomba ushirikiano katika kufikia malengo hayo.
   
Loading...