Elections 2010 Sumaye: Msichague mafisadi mwaka huu

Big up F.T.Sumaye. Nasubiri kwa hamu kumsikia Mh. Salim Ahmed Salim akitupa somo la uraia. Mtu anayetumia pesa au gear za udini ni wa kuogopa. Upo wapi Joseph Warioba?
 
Sumaye si fisadi ila alibambikiwa kashfa ili kummaliza kisiasa. Sumay tunakukumbuka kwa uadilifu wako.

Ungepora kama hawa jamaa wa siku hizi labda na hiki kilichopo kingekuwa hakipo.

Watanzania hilo wanalijua, na kikubwa ni kwamba mgombea urai wa ccm, wazi wazi amewapigia kampeni wote walio tuhumiwa. Hii ina maana ana mgao wa fedha katika njama zote. Watanzania wanajua hilo kinacho fanyika sasa ni kuhadaa umma kwa kutoa tafti za uongo.
WATANZANIA HATUDANGANYIKI TENA!!!!!!!!!!!!!!!
 
Du hii kali sasa, waliosema Chama fulani sasa kimemeguka na kuwa na makundi sasa nona mambo hadharani. Nasubiri kusikia Sheikh Mkuu atasema nini, Tendwa naye atasema nini, maana wao wanaita Siasa kuingizwa kanisani. Askofu mteuli mpya kaweka wazi, kuwa ni jukumu la Kanisa kuwahubiria waumini wake kuchagua viongozi wenye maadili na wenye maslahi kwa Taifa.

Sasa mwenye masikio na asikie na mwenye macho aone kwa hali ilivyo mpaka sasa!!

Mabalozi mpo????? Ushahidi mnao wazi wazi
 
Kwa lugha nyepesi msiwachague Thithiem mwaka huu senkyu Thumae kwa kuwakumbusha watanzania.
 
.. Trilion of Sumaye was constructed to distruct him as was beginning. But, was among of them; so he knows them very much. CCM NI PEPO LINALOHITAJI KUKEMEWA KILA MARA UNAPOSIKIA AU KUHISI!!!
 
MUNGU ambariki kama ameona viongozi mafisadi hawatufai.
na ametupa onyo nasi tusiwachague hao mafisadi.
 
IMG_2587.JPG

Waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye kushoto akiwa na waziri mstaafu Edward Lowassa

WAZIRI mkuu mstaafu, Frederick Sumaye jana aliibuka hadharani na kutoa hotuba kali ya kukemea wagombea wanaotoa rushwa, akisema kuwa njia pekee ya kuwadabisha ni kuwanyima kuta Oktoba 31.Sumaye, ambaye alijaribu karata yake kwenye urais mwaka 2005 na kuangushwa, alisema tatizo kubwa linaloikabili nchi kwa sasa, hasa wakati wa uchaguzi ni rushwa, na hivyo akashauri wananchi watumie silaha yao ya kura kuwashikisha adabu wote wanaotaka uongozi kwa kutoa rushwa.

Sumaye, ambaye hotuba hiyo ni kali ya kwanza kwake tangu astaafu uwaziri mkuu mwaka 2005, alisema: “Rushwa ni tatizo kubwa Tanzania hasa nyakati za uchaguzi.. lazima sote kama taifa tupige vita tukatae utaratibu wa watu wanaotaka uongozi kwa kutununua kama njugu sokoni na tuanze katika uchaguzi huu.”

Sumaye alitoa kauli hiyo katika ibada ya kuwekwa wakfu na kuingizwa kazini kwa askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Pare, Charles Mjema na msaidizi wake, Mchungaji Timothy Msangi.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na maaskofu 25 kutoka ndani na nje ya nchi, wakiongozwa na mkuu wa kanisa hilo, Dk Alex Malasusa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe na viongozi wa serikali na wananchi.

Sumaye alisema watu wanaochaguliwa kwa kutoa rushwa huwa hawawathamini wananchi wanapopata uongozi na kwamba hutumia kipindi chao cha miaka mitano kukusanya fedha nyingine kwa ajili ya kuhonga tena wananchi ili warejeshwe madarakani.

"Hivi sasa inaonekana huwezi kushinda uchaguzi bila kuhonga wapigakura. Kwa staili hiyo mshindi anakuwa kiongozi si kwa sababu anapendwa na watu bali kwa sababu ya kununua uongozi," alisema mbunge huyo wa zamani Hanang, ambaye alikumbwa na tuhuma nyingi za kashfa wakati akielekea kuwania urais.

“Kiongozi anayepatikana kwa njia ya rushwa yeye mwenyewe lazima ni mwizi na ni fisadi, vinginevyo hizo fedha za kuhonga angezipata wapi. Kiongozi mtoa rushwa ni mali ya watu fulani, yaani wale waliompa fedha.”
Waziri mkuu huyo mstaafu alisema kiongozi wa aina hiyo hawezi kuwa na huruma kwani anawaona wananchi wake kama bidhaa sokoni.
“Mimi nasema hivi; hata kama mgombea ni wa chama chako lakini unajua alihonga; hata kama na wewe hizo fedha zilikufikia na ukazila, usimpigie kura Oktoba 31. Hivyo ndio njia pekee tutakayowashikisha adabu.”

Sumaye ambaye hotuba yake ilikuwa ikikatishwa mara kwa mara kwa makofi ya kumshangilia, alisema kiongozi anayeingia madarakani kwa rushwa atatumia miaka yake mitano kutafuta fedha za kuwahonga wananchi kwa kipindi cha pili.
Naye Askofu Mjema alisema KKKT haishabikii chama chochote cha siasa wala mgombea lakini linao wajibu wa kuwahimiza waumini wake kuchagua viongozi watakaoweka mbele maslahi yao.

“Tunahitaji kupata viongozi waadilifu na waaminifu. Ni aibu kwa Mtanzania kurubuniwa kiasi cha kuuza haki yake ya msingi ya kuchagua kiongozi anayefaa. Tumesikia ipo minong’ono ya watu kununua shahada hii ni dhambi,” alisema.
Askofu Mjema alisema moja kati ya mambo yanayotoa dalili mbaya nchini ni namna neno “wapinzani’ linavyotumika kiasi kwamba wapo walioko upinzani ambao biashara zao zimehujumiwa, kutishwa maisha au kubambikiwa kesi.

“Hii ni ishara tosha kuwa na tunaweza kufikia mahali tukakifanya kisiwa cha amani duniani (Tanzania) kikawa kisiwa cha vurugu duniani. Ni vyema Watanzania, vyombo vya dola na wanasiasa tukawa makini na jambo hili,” alisema.
Askofu Mjema ametoa wito kwa wataalamu wa Kiswahili kutafuta msamiati mbadala wa neno “wapinzani” ambao utatumiwa na Watanzania kutambuana katika uwanja wa siasa kuliko wa sasa unaoibua hisia za mgawanyiko.
Alipendekeza mwaka ujao uwe mwaka wa kutimiza ahadi na kurudisha mambo katika mstari na kuitaka serikali kuutumia mwaka kesho kujitathmini na kanisa linapeleka serikalini mambo ambayo hawajayakamilisha.

Askofu huyo alisema zipo taarifa hivi sasa kuwa wawekezaji mbalimbali wanaoikimbilia Tanzania kwa ajili ya kuchukua malighafi mbalimbali wataliachia taifa hili mashimo matupu na jangwa kwa kizazi kijacho pasipo kuwaachia urithi.
“Matatizo makubwa ya nchi za Afrika ni ukosefu wa viongozi watumishi. Wengi wa viongozi wanaoibukia katika rushwa na ufisadi kwa hiyo wanajitajirisha wenyewe na kuwaacha wananchi wao masikini,” alisema.

Alitumia mkusanyiko huo kuzipongeza serikali za rais mstaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete kwa namna walivyojituma katika kushughulikia mgogoro wa dayosisi hiyo uliodumu kwa miaka 12.
Askofu Mjema alisema anatumia siku hiyo ya jana kuutangazia ulimwengu kuwa mgogoro uliokuwepo sasa umekwisha na hiyo jana wachungaji wa Dayosisi ya Pare na ile iliyokuwa ikijiita ya Mwanga waliingizwa kazini kwa pamoja.

Alihidi kutumia nafasi yake kama askofu, kusimamia na kulinda upendo na amani miongoni mwa wachungaji, waumini na wazee wa kanisa katika wilaya za Same na Mwanga na akaomba ushirikiano katika kufikia malengo hay
 
Kwa kauli hii ukweli ni kwamba Sumaye amehama rasmi kutoka CCM kwenda upinzani. nategemea CCM watamhoji kwa kukiuka msimamo wa chama chake, CCM.
Ila kwa kuzingatia matukio na mwenendo wa kampeni ulivyo ndani ya CCM, ni dhahiri chama hicho kakiwezi kuthubutu kumhoji Sumaye maana wataongeza mgawanyiko uliopo sasa.
Tunapoona kampeni za Kikwete zikiongozwa na wanafamilia watatu; Miraji (mfuko wa kampeni), RIZ1 (mikakati) na Salima (uhamasishaji), wakati CCM ina wakongwa wake, lakini wapo kimya, tujue mambo yamekwisha chacha.
Tusubiri kigogo mwingine akitangaza kuhamia Chadama/kuungana Dr. Silaa.
wakhtanabahu
 
"The politician is an acrobat. He keeps his balance by saying the opposite of what he does."
 
Huyu hatampa JK kura, si kwa sababu yeye (Sumaye) ni msafi zaidi., ila kwa sababu JK ni mchafu ni hasimu wake mkuu.
 
Sumaye chonde chonde wasije wakakuita mdini. masheik wamesema tumewasikia na wewe umesema tumekusikia na Askofu Mjema amesema tumemsikia. Ngoja tupime kwa akili za mbayuwayu. hahahahahahahahaha
Hata hivyo mheshimiwa Sumaye, bila kuumauma maneno mie kura yangu nampatia Dr Slaa 31.10. maana yeye sio fisadi lakini ni kiboko cha fisadiz.
 
Wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005; Fredrick Sumaye aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo alizushiwa mambo mengi na kuandamwa na magazeti yaliyoandika uongo uliokuwa ukienezwa na Kikwete na timu yake ya kampeni. Sumaye alidhihakiwa na kudodoswa na magazeti ambayo yanaandika hata leo habari zia maji taka za kupotosha ukweli.

Habari za magazetini zilizotolewa na Kikwete ziliwadhalilisha na kuwadhihaki wagombea wote wakati ule hasa wale waliokuwa na nguvu akiwemo Fredrick Sumaye, John Malecela na Salim Ahmed Salim. Si vizuri kukumbushia maji taka yaliyotoka kwenye timu ya kikwete lakini wagombea wale tena wanaccm wenzake walitukanwa na kuvuliwa utu wao hata kuitwa wauwaji, mafisadi na wasaliti wa taifa letu.

Wakati wa kujitetea; Fredrick Sumaye alisema kuwa kama Kikwete anatumia magazeti na kila njia kuwapakaza watu na kuwauwa kwa kutumia magazeti na vyombo vingine vya habari wakati akiwa mtu wa kawaida, atakapokuwa Rais atatumia mabavu au hata risasi kuwamaliza washindani wake!

Sasa anatumia nguvu za urais ( Dola ) kuhakikisha anarudi madarakani. Anatumia jeshi (Shimbo) anatumia TBC na Dailynews, anamtumia Msajili na tume ya uchaguzi na siku si nyingi tutaanza kuona polisi nao wakitumiwa ingawa mpaka sasa hivi, polisi wanaonekana kuwa katikati bado.

Tusubiri tuone risasi za kikwetew zitakavyo pambana nasi siku tutakapokuwa tunalinda kura zetu.

Hatutaogopa risasi na wala hatutadanganyika kuondoka vituoni. tutalinda Kura zetu wakitaka watupige risasi ili utabiri na maneno ya Sumaye yatimie kikamilifu na huyo Kikwete akisubutu aishie international Criminal Court kule The Hague.
 
Back
Top Bottom