DSE 1,2,3 : "Ninunue hisa za kampuni ipi ?"

DSE 1,2,3 : "Ninunue hisa za kampuni ipi ?"

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,759
Reaction score
3,222
"Ninunue hisa za kampuni ipi ?"
Hili ni moja ya swali ambalo kila Mwanahisa alishawahi kujiuliza au huwa anajiuliza. Leo nitatoa njia nyepesi ambazo utatumia katika kuchagua kampuni utakayoenda nunua hisa zake

NJIA hizo ni

1. Bei ya hisa : Unapofika sokoni,bei huwa ni moja ya kipimo kizuri cha kuchagua bidhaa ipi itakufaa.Bei kubwa uhusishwa na Kampuni zenye kufanya vizuri sokoni huku bei ndogo uhusishwa na Kampuni zenye perfomamce ndogo.

  • Hii ni kweli kwa 60% ; Hisa za CRDB ni bei ndogo kuliko hisa za MKOMBOZI BANK japokuwa CRDB ndiyo inayotengeneza faida na uhakika wa gawio.
2. Matukio ya kila siku : Kama ilivyo kwa masoko ya bidhaa za Vyakula au mavazi,matukio nayo hupelekea kupanda au kuporomoka kwa thamani au bei ya hisa za Kampuni flani
  • Kipindi cha korona : Hisa za makampuni ya mitandao ya mawasiliano,afya na vyakula ni zilikuwa juu kuliko
  • Tunaelekea kwenye AFCON 2027 ; Mashabiki na watalii kadhaa watakuja kwa ajili ya michuano hiyo,na Ndege ndiyo itakuwa chanzo kikuu cha kuwaleta wageni hao nchini. Kampuni ya SWISPORT
3.Wawekezaji wakubwa walipo: Unaambiwa fuata nyuki ule Asali ,pekenyua ripoti za mwaka za makampuni ya DSE Utaona zimeainisha majina ya wanahisa wake wakubwa wenye umiliki wa zaidi ya 1% ya hisa. Kuna majina ukiyaona nawe wekeza.
mfano :
Angalia taasisi kama PSSSF,NSSSF and UTT ,
watu binafsi kama Hans Angaya Masha,Saronga Massawe,Ukoo wa Kadri

4.Sera ya nchi husika : Serikali inapokuja na sera flani ya maendeleo na kuifanyia kampeni hii huweza Kusababisha tasnia inayoguswa na sera ile kutengeneza hela zaidi
  • Mfano; kwenye mkakati wa Serikali wa kuhamia Dodoma ilianzisha ujenzi mkubwa wa majengo ya Serikali Pamoja na Barabara,Vifaa vingi vya ujenzi Pamoja na Simenti zilihitajika maradufu,Kampuni za Simba na Twiga zikatengeneza faida kubwa sana.

5.Kampuni inayozungumziwa zaidi : wanakwambia kizuri kinajiuza na kibaya chaji angaisha.Sasa kwa awamu ya kwanza nenda ukanunu hisa za Kampuni ambayo wengi wanaizungumzia zaidi.
Mfano; Kwa kipindi cha karibuni ; watu wengi nimeona wamekuwa wakizungumzia benki ya CRDB pale linapokuja suala la kununua hisa,ukifanya utafanya utafiti wa haraka kweli CRDB imekuwa vizuri.


6. USHAURI WA WAKALA : Unaweza omba ushauri kutoka kwa wakala wako alimaarufu Broker.Kwakuwa nao ni wapo kwenye biashara hii,ina maana wanajua mwenendo wa soko jinsi ulivyo.


itaendelea...
 
Back
Top Bottom