Sumaye amgwaya Lowassa!

naona kwa pambeni kama sued kubenea, naye anaandika habari apeleke wapi? wakati gazeti lake limefungiwa?
 
Kwa kifupi huyu PM mstaafu hana jipya. Anasahau wao ndi waasisi wa rushwa a.k.a takrima,mtetezi wa rushwa na mlinzi wa rushwa wakati akiwa madarakani. Sasa timu uliyoifundisha ikikufunga GOLI utalalamika wakati UTEACHER wako umejibu. Loo! mtu mzima aone aibu.
 
Ukitaka kujua kama nguo uliyovaa ni chafu ni vizuri kuivua na kuichunguza ikiwa haipo mwilini mwako,Sumaye hawezi kusema maovu ya ccm waziwazi kwasababu si utaratibu wa chama,kama chama kuna mahali pa kusemea hayo na katu si kwenye press conference.binafsi nilitegemea kabisa kuwa hakuna jipya lolote litakalojiri and that is what happened.huo ndio ulikua mwanzo wa mwisho wa wazir mkuu mstafuu.
 
Hivi unawezaje kumcriticize mtu kabla ya kumpa nafasi ya kumsikiliza? Tusikilize kwanza mheshimiwa atatuambia nini. Ila kitu kikubwa ninachokiona ni kuwa hili jambo sio zuri kwa CCM na kitendo cha Sumaye kwenda kwenye vyombo vya habari kinasema mengi kuhusu hali ilivyo ndani ya hiki chama.
 
Huyu PM mstaafu hana jipya. Amesahau kama ndiye alikuwa mwasisi, mlezi na mtetezi wa rushwa a.k.a takrima wakati alipokuwa madarakani na yule rafiki yake. Sasa timu aliyoifundisha ikifunga Goli analalamika nini wakati hiyo ni UKOCHA umejibu. Lazima atafakari sana maana amesahau alikotoka.
 
Hivi unawezaje kumcriticize mtu kabla ya kumpa nafasi ya kumsikiliza? Tusikilize kwanza mheshimiwa atatuambia nini. Ila kitu kikubwa ninachokiona ni kuwa hili jambo sio zuri kwa CCM na kitendo cha Sumaye kwenda kwenye vyombo vya habari kinasema mengi kuhusu hali ilivyo ndani ya hiki chama.

Naam mkuu uko sahihi kabisa, tusiwe wepesi wa kusema na kumtusi mtu. Nafikiri sio busara kukosoa media kukubali kwenda kumsikiliza Sumaye kabla hata ya kujua agenda zitakazojiri. Ni wajibu wa Media kukusanya habari na kuwahabari wateja wake, ukizingatia aliyeitisha mkutano ni mtu muhimu katika nchi yetu.

Pia tusisahau kuwa kila mtu ana freedom of expression....so ni wajibu wa sumaye kujieleza...tena kutengua tanzu na kuondoa maswali mengi yaliyokuwa vichwani kwa watu. Tatizo letu tulitaka aseme yale ambayo tulifikiri angesema.
 
Mkuu ni kama tumetoka kapa, sijaona kipya alichosema Sumaye, labda ni macho yangu hayasomi vizuri.

Mkuu Bongolender, Usisisngizie macho aliyokupatia Muumba. Ni pumba tu. Mbona hajawataja wala Rushwa. Ni general blah blah tu
 
Hakuna kitu kitamu kama taaluma! unapokuwa mwanataaluma/msomi mara nyingi unapenda kuongeza maarifa yako kupitia katika tafiti mbalimbali katika eneo husika! Moja kati ya kanuni kuu ya utafiti ni kufanya kitu ambacho either kinaongeza maarifa au ni maarifa mapya unagenerate.,otherwise hakuna haja ya utafiti!

Natamani sana hata katika siasa ingekuwa hivyo kwamba mtu unapoofanya kitu aim katika mojawapo la hayo!

Nimeshawishika kuandika hivi kutokana na mkutano wa leo kati ya Mh. Sumaye na waandishi wa habari.,I thought kulikuwa na jambo ambalo its very burning kipya kwenye vile tunavyovijua au tunaongezea pale tusipopajua! Loh! To my surprise anaongelea Rushwa ndani ya CCM! Is it something ambayo ilihitaji kusumbua na kuwakusanya waandishi wa habari mmmh! Me nadhani angeweza tu kuwaambia watu kwamba wasome kitabu cha Prof. Mwandosya kinachoitwa Mchakato wa uchaguzi Mbeya cha mwaka 2012. Kila kitu kimo humo fitina zote zimedadavuliwa kwa kina!

Jamani hebu viongozi wetu tumieni busara tumieni muda wenu na wetu vizuri. Tuambieni mambo ya msingi ambayo yatatusaidia kumove kutoka point ya umaskini tuliyopo kwenda kwenye point yenye heri kidogo....
 
Alienda Azania front kusali ili iweje sasa afu anakuja kutudanganya hapa na kuendelea kuficha maovu......
 
Huyu jamaa ni muoga wa Kushindwa, amekua PM kwa miaka Kumi, na huko kote alikuwa anapata kila anachotaka, sasa safari hii kafeli kdg tu anakuja na sababu za kipuuzi kabisa tena mbele ya waandishi wa habari.... mie nilitegemea atakuja na list of Names ndani ya CCM ambao wametumia Rushwa katika Uchaguzi wa ndani.

Ila nae ni mroho tu hana cha kusaidia wananchi wala nini.... koz nadhani hakuna Kiongozi anaemiliki Ardhi Mingi kama yeye. Kama kweli angekua anapenda wananchi angeanza na kupunguza ardhi ile kwa kugawa kwa wananchi.
 
2012-10-07_13-34-36_880.jpg 2012-10-07_13-36-01_925.jpg 2012-10-07_13-36-48_236.jpg
 
yaani sumaye unazidi kugalagaza p yako, haya tu ndo uliyotaka kuongea na waandishi wa habari au kuna jingine?. anyway unatafuta huruma ya watz, kubali tu umeshindwa na we mwenyewe si msafi kiasi cha kuwanyoshea vidole wenzako, eti watoa rushwa.
 
Waandishi wa habari wangekuwa na msimamo wangemuumbua palepale na kutoandika chochote alichosema.

Ni unafiki tu kwani mbona hawatoki ccm kama chama hakichukui hatua!
 
Sikuwa na tegemeo la jambo jipya kutoka kwake. Nilijua atarudia hayo hayo ya rushwa ndani ya ccm. Nagu alipanda dau jamaa akapigwa chini. Kama sio ubahili wake labda angeshinda
 
Sumaye alikuwa na nia ya kutiririka tatizo amevujisha siri mapema. Kama kawaida magamba wakampa angalizo na baada ya kuchekecha akapotezea.Tunao magamba tunaowakubali lakini ninachojua "TIME WILL TELL NOT SO LONG"
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Aaah aah nilishawaambia hamna kitu hapo, watu wakasema ooh sumaye anapasua jipu, hamna hiyo kitu mtaona ccm lao moja ni ufisadi kwa kwenda mbele!
 
Back
Top Bottom