Fredrick Sumaye: Najuta, tulikosea kubadili vyuo vya kati kuwa vikuu

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Sumaye, aliyekuwa Waziri Mkuu Serikali ya Awamu ya Tatu, alisema kasi ya kupanua vyuo vikuu haikuendana na ukuaji wa uchumi kwa kuwa vijana wengi waliomaliza shahada hawakuwa na ujuzi wa kufanya kazi za fani walizosomea.

Kauli ya Sumaye inafanana na ya aliyekuwa Rais wa awamu hiyo, Benjamin Mkapa ambaye mwaka 2018 alishauri mfumo wa elimu kupitiwa upya kutokana na dosari zilizopo.

Tayari Serikali imeshaanza kufanya mapitio ya Sera ya Elimu ya mwaka 2014 na mitalaa yake.

Akizungumza katika mahojiano na redio ya Clouds, Sumaye alikiri kuwa katika nafasi yake ya uwaziri mkuu alikuwa sehemu ya mabadiliko hayo ambayo yameleta matokeo hasi kwa Taifa.

Alisema endapo upanuzi wa elimu ungefanyika kulingana na uchumi unavyokua, tatizo la ukosefu wa ajira lisingekuwa kubwa kama sasa kwa sababu vijana wangeweza kujiajiri na kutengeneza ajira kwa wengine.

“Kosa ambalo tumelifanya kama Taifa kulikuwa na mhemko fulani wa watu kubadilisha kila chuo kuwa chuo kikuu, hadi leo naamini kuwa hilo ni kosa na mimi ni sehemu ya hilo kosa kwa sababu hata wakati wetu kuna vyuo vya kati tulivyovibadili kuwa vyuo vikuu,” alisema Sumaye.

“Vingine niliwahi kukataa hadi maprofesa walikuwa wananifuata nyumbani usiku kuja kuomba niruhusu vyuo vyao vipandishwe hadhi kuwa vyuo vikuu,” alisema.

Sumaye alisema hatua hiyo ilisababisha vyuo vya kada ya kati vilivyokuwa muhimu kiuchumi, kufa.

“Tumeua, mfano Chuo cha Ushirika Moshi kilikuwa kinatoa vijana mahiri katika ushirika, lakini tukakifanya chuo kikuu, sasa wote wanatafuta kazi mitaani,” alisema Sumaye.

Safari yake ya elimu

Kama ilivyo kwa watoto wengine kutoka jamii za kifugaji, haikuwa rahisi kwa Sumaye kwenda shule, bali aliandaliwa kuwa mfugaji.

Alisema akiwa na umri wa miaka saba mpango wa serikali ya kikoloni wa kuwapeleka shuleni watoto wote wenye umri wa kuwa shule, ukafika rasmi kijijini kwao.

Alisema mwishoni mwa mwaka 1957, chifu akiwa ameambatana na tarishi katika eneo walilokuwa wakichunga alimkamata kaka yake kwa ajili ya kumuandikisha shule, lakini baba yake hakukubaliana na hilo.

“Kwa kuwa baba alikuwa ameshaweka utegemezi mkubwa kwa kaka kwa ajili ya kumsaidia kuangalia mifugo, akaomba nikaandikishwe mimi kama mbadala wa kaka, alifanya hivyo kwa makusudi kabisa akijua hawawezi kunikubali kwa sababu ni mdogo,” alisema Sumaye.

“Tarishi alinipeleka shuleni nikiwa nimeambatana na kijana mwingine wa pale kijijini, yule mwenzangu alikuwa mkubwa sana kunizidi. Tulipofika shuleni alitangulia mwenzangu mimi nikajificha.”

Alisema umri wa yule kijana aliyeambatana naye ulikuwa mkubwa kiasi kwamba mwalimu alikataa kumuandikisha, alipoangaliwa Sumaye ikaonekana pia hafai kwa kuwa umri wake ni mdogo.

Hata hivyo, mwaka uliofuata alisema alianza darasa la kwanza, akitembea umbali wa kilomita 16 kuifuata shule ilipo na umbali huo huo kurejea nyumbani akikatiza porini ambako pia kulikuwa na wanyama wakali, wakiwamo chui na duma.

“Siwezi kusahau, nilikuwa namsikia mama akimka saa nane hadi saa tisa (usiku), akisaga mahindi anipikie ugali nile ndiyo nianze safari ya kwenda shule alfajiri. Kutokana na njia ninayopita kuwa na wanyama wakali wakati mwingine mama yangu alikuwa akinisindikiza,” alisema Sumaye.

Alisema alipomaliza darasa la nne alichaguliwa kuingia darasa la tano na baada ya kumaliza darasa la nane alichaguliwa kwenda Shule ya Sekondari ya Ilboru iliyopo Arusha. “Baba alikataa kuuza ng’ombe wake ili aninulie mahitaji ya kwenda shule hivyo ikabidi nikae nyumbani,” alisema Sumaye.

Kutokana na hilo, alisema alisota nyumbani mwezi mzima kiasi cha kukata tamaa na kumpa fomu rafiki yake ili achukue nafasi hiyo, hata hivyo, rafiki yake naye akaikataa akisema amechelewa.

“Nikiwa natembea nirudi nyumbani eneo la mnadani nikakutana na kaka yangu, akaniambia alikuwa ananitafuta mimi, mama ameuza ng’ombe wake na kupata pesa ambazo amezitoa ili ninunue mahitaji niende shule,” alisema.

Pamoja na kupata hela ya kuendea shule, alisema bado alikuwa na wasiwasi wa kupokelewa kwa kuwa alikuwa amechelewa.

Sumaye alisema alipofika shule, alimkuta mwalimu wa zamu aliyemtaka asome kipengele cha muda kwenye fomu ya kujiunga, hali iliyomfanya abaki akilia.

“Nikaenda kwa mkuu wa shule nikiwa nalia, yule baba alikuwa muungwana, akaniuliza mtoto unataka kusoma nikamjibu ndiyo, akasema haya utasoma. Kuanzia siku hiyo rasmi nikaanza masomo Ilboru,” alisema Sumaye.

Alisema alimaliza kidato cha nne na kupata ufaulu wa daraja la kwanza, hata hivyo akaona asiende kidato cha tano, badala yake asome kozi yoyote ya ufundi.

Sumaye alisema aliomba kozi ya ufundi na akapangiwa Chuo cha Ufundi cha Dar es Salaam (DIT) ambako alisoma kwa miezi michache kabla ya kutafuta kozi nyingine aliyoona inaweza kuwa na tija zaidi kwake.

Hata hivyo, alisema alijadiliana na mwenzake waliyetoka naye Ilboru na kwenda Wizara ya Kilimo kuomba kusoma kozi ya kilimo.

Alisema mwenzake alipelekwa Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na yeye akapelekwa Chuo cha Kilimo cha Egerton kilichopo Kenya katika kozi ya uhandisi wa kilimo kwa ngazi ya diploma.

Kuhusu kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu, Sumaye, aliyekuwa mbunge wa Hanang mkoani Manyara, alisema licha ya kuwa na kaliba ya uongozi tangu akiwa shuleni, hakufikiria kwamba siku moja angehudumu katika nafasi ya juu serikalini.
 
Sasa hivi vyuo vikuu vina matawi mpaka simiyu...
Ni mwendo wa shahada tu.... hata aliepata four nae akiunga vizur anapewa.

Vyuo vikuu hadi kwenye super market, kama pale Mwanza.

Hakuna ujuzi wala nini.... end of the day.. nchi imezalisha chawa wengi kuliko wanyonywaji.

Wengine wameibukia kwenye fan ya transport officer.. na serikal imebariki... Twende kaz..
Bomu lingine kubwa ni hili la vyuo vya afya...

D4 tu unakuwa Nurse, Daktar, Mfamasia nk... twende kazi.
 
Ndiyo maana mzee anajuta
 
Hiyo Elimu Yao kina sumaye na mliosoma zamani , je? Mmefanya Jambo gani la maana .

Yaani nashangaa Sana kuona mtu anasema Elimu ya Zama hizi haifai ni kweli haifai lakini hata Elimu ya zamani haifai vilevile.

Wazee waliosoma zamani ndo Hawa wezi, mafisadi majambazi walioleta Katiba mbovu na upuuzi mwingine Kama huo
 
Ukweli mtupu. Chawa walishaanza kuwa wengi kuliko wanyonywaji.
 
Hiyo Elimu Yao kina sumaye na mliosoma zamani , je? Mmefanya Jambo gani la maana .

Yaani nashangaa Sana kuona mtu anasema Elimu ya Zama hizi haifai ni kweli haifai lakini hata Elimu ya zamani haifai vilevile.

Wazee waliosoma zamani ndo Hawa wezi, mafisadi majambazi walioleta Katiba mbovu na upuuzi mwingine Kama huo
naona umekuja na mhemko bila kudadafua hoja kama vile upo katika nni hii zako. Hoja ni kwamba kuua Vyuo vya kati ambayo vilikuwa vinatoa elimu ya umahiri. Hivyo vyuo vyote tuvuruhusu kutoa maafisa ndo penye tatizo. Graduate ni Officer. Sasa kama kila anayemaliza chuo ni Officer nani atatumwa?
 
Hata BAADHI ya shule za msingi ambazo zilikuwa na madarasa yaliyojengwa vizuri na mkoloni nayo yalibadirishwa kuwa vyuo vya Wali u badala ya kujenga vyuo vipya.
 
Kama walikurupuka hilo halina msaada kwa sasa, ndo maana kiongozi unatakiwa uwe na vision na kuchambua hoja za kitaalamu zinazotolewa kwa weledi mkubwa. Kwani kipindi hicho walikuwa na uhaba wa maafisa hadi waanzishe utitiri wa vyuo vikuu?
 
Sumaye, aliyekuwa Waziri Mkuu Serikali ya Awamu ya Tatu, alisema kasi ya kupanua vyuo vikuu haikuendana na ukuaji wa uchumi kwa kuwa vijana wengi waliomaliza shahada hawakuwa na ujuzi wa kufanya kazi za fani walizosomea.

Kauli ya Sumaye inafanana na ya aliyekuwa Rais wa awamu hiyo, Benjamin Mkapa ambaye mwaka 2018 alishauri mfumo wa elimu kupitiwa upya kutokana na dosari zilizopo.

Tayari Serikali imeshaanza kufanya mapitio ya Sera ya Elimu ya mwaka 2014 na mitalaa yake.

Akizungumza katika mahojiano na redio ya Clouds, Sumaye alikiri kuwa katika nafasi yake ya uwaziri mkuu alikuwa sehemu ya mabadiliko hayo ambayo yameleta matokeo hasi kwa Taifa.

Alisema endapo upanuzi wa elimu ungefanyika kulingana na uchumi unavyokua, tatizo la ukosefu wa ajira lisingekuwa kubwa kama sasa kwa sababu vijana wangeweza kujiajiri na kutengeneza ajira kwa wengine.

“Kosa ambalo tumelifanya kama Taifa kulikuwa na mhemko fulani wa watu kubadilisha kila chuo kuwa chuo kikuu, hadi leo naamini kuwa hilo ni kosa na mimi ni sehemu ya hilo kosa kwa sababu hata wakati wetu kuna vyuo vya kati tulivyovibadili kuwa vyuo vikuu,” alisema Sumaye.

“Vingine niliwahi kukataa hadi maprofesa walikuwa wananifuata nyumbani usiku kuja kuomba niruhusu vyuo vyao vipandishwe hadhi kuwa vyuo vikuu,” alisema.

Sumaye alisema hatua hiyo ilisababisha vyuo vya kada ya kati vilivyokuwa muhimu kiuchumi, kufa.

“Tumeua, mfano Chuo cha Ushirika Moshi kilikuwa kinatoa vijana mahiri katika ushirika, lakini tukakifanya chuo kikuu, sasa wote wanatafuta kazi mitaani,” alisema Sumaye.

Safari yake ya elimu

Kama ilivyo kwa watoto wengine kutoka jamii za kifugaji, haikuwa rahisi kwa Sumaye kwenda shule, bali aliandaliwa kuwa mfugaji.

Alisema akiwa na umri wa miaka saba mpango wa serikali ya kikoloni wa kuwapeleka shuleni watoto wote wenye umri wa kuwa shule, ukafika rasmi kijijini kwao.

Alisema mwishoni mwa mwaka 1957, chifu akiwa ameambatana na tarishi katika eneo walilokuwa wakichunga alimkamata kaka yake kwa ajili ya kumuandikisha shule, lakini baba yake hakukubaliana na hilo.

“Kwa kuwa baba alikuwa ameshaweka utegemezi mkubwa kwa kaka kwa ajili ya kumsaidia kuangalia mifugo, akaomba nikaandikishwe mimi kama mbadala wa kaka, alifanya hivyo kwa makusudi kabisa akijua hawawezi kunikubali kwa sababu ni mdogo,” alisema Sumaye.

“Tarishi alinipeleka shuleni nikiwa nimeambatana na kijana mwingine wa pale kijijini, yule mwenzangu alikuwa mkubwa sana kunizidi. Tulipofika shuleni alitangulia mwenzangu mimi nikajificha.”

Alisema umri wa yule kijana aliyeambatana naye ulikuwa mkubwa kiasi kwamba mwalimu alikataa kumuandikisha, alipoangaliwa Sumaye ikaonekana pia hafai kwa kuwa umri wake ni mdogo.

Hata hivyo, mwaka uliofuata alisema alianza darasa la kwanza, akitembea umbali wa kilomita 16 kuifuata shule ilipo na umbali huo huo kurejea nyumbani akikatiza porini ambako pia kulikuwa na wanyama wakali, wakiwamo chui na duma.

“Siwezi kusahau, nilikuwa namsikia mama akimka saa nane hadi saa tisa (usiku), akisaga mahindi anipikie ugali nile ndiyo nianze safari ya kwenda shule alfajiri. Kutokana na njia ninayopita kuwa na wanyama wakali wakati mwingine mama yangu alikuwa akinisindikiza,” alisema Sumaye.

Alisema alipomaliza darasa la nne alichaguliwa kuingia darasa la tano na baada ya kumaliza darasa la nane alichaguliwa kwenda Shule ya Sekondari ya Ilboru iliyopo Arusha. “Baba alikataa kuuza ng’ombe wake ili aninulie mahitaji ya kwenda shule hivyo ikabidi nikae nyumbani,” alisema Sumaye.

Kutokana na hilo, alisema alisota nyumbani mwezi mzima kiasi cha kukata tamaa na kumpa fomu rafiki yake ili achukue nafasi hiyo, hata hivyo, rafiki yake naye akaikataa akisema amechelewa.

“Nikiwa natembea nirudi nyumbani eneo la mnadani nikakutana na kaka yangu, akaniambia alikuwa ananitafuta mimi, mama ameuza ng’ombe wake na kupata pesa ambazo amezitoa ili ninunue mahitaji niende shule,” alisema.

Pamoja na kupata hela ya kuendea shule, alisema bado alikuwa na wasiwasi wa kupokelewa kwa kuwa alikuwa amechelewa.

Sumaye alisema alipofika shule, alimkuta mwalimu wa zamu aliyemtaka asome kipengele cha muda kwenye fomu ya kujiunga, hali iliyomfanya abaki akilia.

“Nikaenda kwa mkuu wa shule nikiwa nalia, yule baba alikuwa muungwana, akaniuliza mtoto unataka kusoma nikamjibu ndiyo, akasema haya utasoma. Kuanzia siku hiyo rasmi nikaanza masomo Ilboru,” alisema Sumaye.

Alisema alimaliza kidato cha nne na kupata ufaulu wa daraja la kwanza, hata hivyo akaona asiende kidato cha tano, badala yake asome kozi yoyote ya ufundi.

Sumaye alisema aliomba kozi ya ufundi na akapangiwa Chuo cha Ufundi cha Dar es Salaam (DIT) ambako alisoma kwa miezi michache kabla ya kutafuta kozi nyingine aliyoona inaweza kuwa na tija zaidi kwake.

Hata hivyo, alisema alijadiliana na mwenzake waliyetoka naye Ilboru na kwenda Wizara ya Kilimo kuomba kusoma kozi ya kilimo.

Alisema mwenzake alipelekwa Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na yeye akapelekwa Chuo cha Kilimo cha Egerton kilichopo Kenya katika kozi ya uhandisi wa kilimo kwa ngazi ya diploma.

Kuhusu kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu, Sumaye, aliyekuwa mbunge wa Hanang mkoani Manyara, alisema licha ya kuwa na kaliba ya uongozi tangu akiwa shuleni, hakufikiria kwamba siku moja angehudumu katika nafasi ya juu serikalini.

Lile lilikuwa kosa kubwa sana, hasa kwenye vyuo vya ufundi, kama vile Dar Tech, Arusha Tech na Mbeya Tech. Vyuo vya namna ile vilistahili kuongezwa sana, lakini wakaviua.

Vile vyuo vya kati vilikuwa vinampa mtu msingi wa kuwa na Elimu na maarifa. Ndio maana waliopitia vile vyuo na baadaye mpaka kuja kuwa na shahada walikuwa na Elimu na maarifa ya kutenda.

Leo hii, mtu anamaliza chuo kikuu, mpaka ana makaratasi ya PhD, ana Elimu lakini hana maarifa, na hawezi kutenda kitu chochote cha kikaonekana.

Leo hii wamejaa wahandisi maneno, hatuna wahandisi wa kufanya vitu vikaonekana. Vyuo vile vya namna ya Arusha Tech, Dar Tech ma Mbeya Tech, kama vungeendelezwa na kuingezwa, bila shaka sasa hivi pikipiki tungekuwa tunatengeneza wenyewe, simu tungekuwa tunatengebeza wenyewe, na vipuli mbalimbali vya mitambo mbalimbali vingekuwa vinatengenezwa nchini.
 
Uko sahihi
 
Back
Top Bottom