Sumaye amgwaya Lowassa!

Sumaye amgwaya Lowassa!

sumaye kweli mr zero! Kila mtu anajua rushwa za ccm, kipi kipya kilichomsukuma zaidi ya rushwa?
I wish waandishi wangemwuliza kabla kama alikuwa na kipya tofauti na hizi pumba
 
Last edited by a moderator:
Hivi unawezaje kumcriticize mtu kabla ya kumpa nafasi ya kumsikiliza? Tusikilize kwanza mheshimiwa atatuambia nini. Ila kitu kikubwa ninachokiona ni kuwa hili jambo sio zuri kwa CCM na kitendo cha Sumaye kwenda kwenye vyombo vya habari kinasema mengi kuhusu hali ilivyo ndani ya hiki chama.

Inajulikana wazi kwamba hivi sasa CCM ipo katika utaratibu wa kujikaanga.

Kitu kinapokaangwa pia ni lazima kuwepo vikorombwezo vya aina mbalimbali ili kuleta ladha sawia.
 
N00B na Wana JF,
Tunashukuru kwa kazi kubwa ya kutuabarisha yaliyojiri,
Kwa maoni yangu hapo, hakuna JIPYA alichoongea, amefunga safari toka Arusha aka Hanang mpaka Dar kuja kuongea *****, ni bora angeyasema huko huko, ametupa Attention kutaka kusikia, ameishia kuongea Mafumbo.
My Take: Ifikie wakati Wanasiasa wawe Wajasiri kwa kuongea UKWELI.
Nawakilisha



Na sisi ambao si waandishi na hizo bahasha hatuchukui? Katupotezea muda, hiki si kitu cha kuitisha mkutano na waandishi na kuongea. Hakuna jipya hapa. Natoka wakuu
 
Kama unataka biashara zako zifanikiwe peperusha bendera ya CCM "Sumaye"

By the way he was JK's boss by then and the later Kiss his *ss kwa sana to be wherever he is! They aren't different at all.
 
Sumaye alikuwa na nia ya kutiririka tatizo amevujisha siri mapema. Kama kawaida magamba wakampa angalizo na baada ya kuchekecha akapotezea.Tunao magamba tunaowakubali lakini ninachojua "TIME WILL TELL NOT SO LONG"

usicheze na system hasa kama we mwenyewe ni mchafu.
Sumai anajijua madudu yake ndomana hana ujasiri wa kupambana kikwelikweli, huwezi kukemea ufisadi wakati na wewe ni miongoni mwao.
 
Sumaye, sumaye bwana shamba wa SKU uyole mbeya. Nakumbuka uliwahi sema anayetaka kufanya biashara aje ccm! Sasa biashara wamefanya mpaka uvunguni kwako, chezea ccm veve! Umepitwa na wakati, wewe ni masalia HATUKUHITAJI, baki huko huko magamba.
 
Inawezekana kweli alitaka kuongea kitu kingine, on the way akatishwa ikabidi achange haraka ndo maana hotuba yako imekosa mashiko....
 
Mimi nafikiri mkubwa huyu apumzike kwani amekwisha ona kuwa magamba wezake wanavyotafuta utawala kwa njia ya mlungula
 
ni vyema tukajikumbusha kuhusu mkutano uliopita kati ya sumaye na waandishi wa habari mwezi machi 2011

Nimejiunga na TANU tangu mwaka 1966, mimi ni mwana CCM tangu
kuanzishwa kwake 1977 na ni mjumbe wa NEC


Sina uhusiano mbaya na UVCCM, sina uhusiano mbaya na yeyote ambaye ni
mwana CCM.

Napenda kuongelea kuhusu 2015, sijaamua kama nitagombea au sitagombea

Wananchi ndio wenye uwezo wa kila jambo katika nchi, wananchi ndio
wanaopiga kura na ndio wanaoamua nani awe kiongozi na nani asiwe.

Makundi matatu yanayoamua nani awe kiongozi ni WANANCHI, CHAMA
anachotoka mwanasiasa na DOLA

Kwanini nimewaita?

Kumeibuka malumbano ndani ya CCM na UVCCM kutokana na matamshi ambayo
yanakanganya na mimi ni mmojawapo ambaye nimeshambuliwa sana.

Nipo hapa kwa niaba yangu mwenyewe, sijatumwa na yeyote na SIMSEMEI
YEYOTE. Nipo hapa kama Frederick Sumaye.

Ningeyapeleka kwenye chama hasa NEC lakini kwakuwa na wenzangu
wameanza kwa mtindo wa kuitisha vyombo vya habari nami nafuata
utaratibu huo


Lengo si kushindana wala kupimana nguvu, lengo ni kuweka uwazi kwa
wananchi watambue uhalisia

Baada ya kuona wananchi wanavyoyapokea maandamano ya CHADEMA na kwa
hamasa kubwa nilishauri CCM itoe ushirikiano kwa serikali kwa kuyajibu
wanayotoa CHADEMA ili kuweza kuweka hali halisi. Mimi kusema CCM
ifanye sikumaanisha MIMI SIMO.

Aidha, sijasema serikali isifanye kazi yake. Waziri Wassira amefanya
kazi ya serikali vema tu

Katika utaratibu wa kawaida, chama kinafanya kazi yake baadae serikali
inakuja kumalizia yanayobakia. Kama kazi ya siasa haijafanyika vema na
chama basi serikali hubeba lawama zisizostahili.

Malumbano ya kisiasa hujibiwa kisiasa, CCM walitakiwa kuwajibu CHADEMA
na si kazi ya serikali kufanya kazi ya kisiasa

CCM inafahamu kazi ya kisiasa na kimekuwa kikifanya hivyo tangu
zamani. Viongozi wetu wamekuwa wakifanya hivyo kwenye kila ngazi. Ni
shughuli ya chama na haihitaji maamuzi ya vikao.

Akiongea Sumaye linaonekana tatizo kubwa na tena ni utovu wa nidhamu.
Nimeshutumiwa na hata kutukanwa na wengine ndani ya chama

Nifafanue:

Nimeshutumiwa kuwa namshutumu mwenyekiti wa chama. Nilijibu nikadhani
mambo yameisha kumbe ndo kwanza yameanza.

Nimeshutumiwa na UVCCM Pwani kuwa - Sumaye na Lowassa wana mpango wa
kukivuruga chama ili wafikie malengo yao 2015


Kama Lowassa na Sumaye wanautaka urais 2015, kwanini washirikiane?
2015 kutakuwa na marais wawili?

Hakuna sehemu hata moja ambapo niliwahi kumtaja rais katika maongezi
yangu, madai kuwa namtukana na kumchafua rais ni tuhumu za uwongo
kabisa

UVCCM wanadai sisi tumeshiba na sasa tumevimbiwa... Tuwaache nao wale
kama sisi.

Haya ni matusi na kejeli na inasikitisha sana

Ina maana UVCCM wana mgombea wao ndo maana wengine tunaonekana kero
kwao kwani tunamvurugia mtu wao. Vijana wenye tamaa ya KULA ni hatari
kwa taifa

Eti vijana wanataka wamweke mtu wao ili wale? Imenishtua sana!

Wanadai tunakibomoa chama, wanadai kuwa tunataka rais atoke kaskazini.
Kwa madai yao nchi itaendelea kusonga mbele na wanatupa pole
tunaodhani rais lazima atoke kaskazini.


Ubaguzi huu wa ukanda tena kutoka UVCCM mkoa wa Pwani usipochukuliwa
hatua utalipeleka pabaya taifa!


UVCCM wana mpango wa kupambana kina Sitta na Sumaye. Wanataka hawa
wasipewe nafasi katika chama, wanadai watapigana ndani na nje ya chama
kuhakikisha watu hawa hawapewi nafasi.



Sitta yashaanza kumkuta ya UVCCM huko Tabora!

Kuna maoni mengine yanaweza kuwa na athari kwa chama hivyo ni juu ya
kiongozi husika kuangalia athari ya kutoa maoni husika.

Serikali yoyote iliyochaguliwa kidemokrasia LAZIMA itasemwa na
kukebehiwa. Kiongozi yeyote na chama chochote kilichochaguliwa
kidemokrasia, kitasemwa na watu watakikebehi. Si ajabu


Nimeshtushwa SANA na kauli ya UVCCM mkoa wa Pwani kuwa suala la rais
ajaye 2015 lipo mikononi mwa rais Kikwete! Hili linanishtua, siamini
kama rais Kikwete anamjua rais ajaye 2015


Sasa hivi mtu yeyote akiongea ndani ya CCM ataambiwa anautaka urais,
hii inaweza kuwaziba wengi midomo

Nawaomba watanzania, yeyote atakayejaribu kutumia njia za udanganyifu
kwa RUSHWA, KUTENGANISHA WATU, tumkatae kwa nguvu zote


Tunakosa muda wa kujielekeza katika mambo ya msingi tunaanza siasa za
kupakana matope - Sumaye

Nategemea nimeeleweka, sitarajii kuibua malumbano na sitarajii kurejea
kuongea na waandishi juu ya hili. Mimi ni mwana CCM na sipo chama
chochote cha siasa zaidi ya hiki.


Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
 
Ni binadamu dhaifu pekee,asiyeweza kutekeleza mambo yaliyokwisha kuamuliwa...R.I.P Sokoine!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kama mlitegemea atangaze anahamia chadema mmeliwa. Hivi hii si hadithi ya sizitaki mbichi hizi??? Kerere za machura zimezidi. Kumshabikia sumaye ilikuwa ni kutaka ajiunge na mavuvuzera ya slaaa haingii ngooo,

ubabe wa chadema wasomi udsm wamesema nini vile? teh teh teh teh uwongo na uzandiki kumbe una chuki na cdm mods wakastukia wakakachanilia mbali kathread kako teh teh teh.
 
Nashukuru mkuu kwa kutukumbusha yaliyotokea mwaka mmoja nyuma .Sasa kama ndiyo hivyo kwanini mkubwa huyu ameamua kufunika kombe mwanaharamu apite?
 
Silly! Mlolongo wa woga unazudi kukua, tunaye
Mwakyembe (nimepewa sumu nikirudi nitaja ongea kila kitu... kimya) ,
Dr. Ulimboka ( niombeeni nipone naja kumtaja aliyenikwida ...kimya),
Frederick Sumaye (Sina ubaya na mtu yeyote akimaanisha anawaonyesha hana kinyongo wamtafutie pa kumweka apate namna ya kuishi shame eeh... au mnajisafisha kwa Masai/Mmeru ili asije akawafanya kitu mbaya?
 
SUMAYE is a sounding BRASS.... hana la maana wazee kama hawa bora wakae vijijini walee wajukuu zao
 
Sijaona la maana hapa zaidi ya bla bla za kila siku za wanasiasa wetu na tumezoea haya
 
Back
Top Bottom