Kama ameshindwa kwa kuwa rushwa ilitumika kumwangusha na yeye hatakata rufaa kwa ajili ya hilo, kwangu mimi inamaanisha kuwa anakmubaliana na matokeo hayo yaliyotokana na matumizi ya rushwa. Kwa maneno mengine, anbakubaliana na rushwa ndani ya chama chake.... bado tuna safari ndefu
Sumaye:
Hanang'kulikuwa na matumizi makubwa ye fedha, uharamia wa kuhamisha watu... Sitokata rufaa wala sitolalamika chamani maana kila jambo lilikuwa hadharani na media ilitoa taarifa.
Siko CCM kwa ajili ya vyeo... Nchi nyingi zimeingia katika vurugu na kuhatarisha amani ktk uchaguzi,,, Tanzania tusichafue kwa kusababisha matatizo kwa kutimia vibaya umasikini wa Watanzania.
Najua si matamu kwa masikio ya wengine na tusiwanyamazishe wanaozungumzie kwa uwazi.
Mungu ibariki Tanzania
Sumaye alikuwa na nia ya kutiririka tatizo amevujisha siri mapema. Kama kawaida magamba wakampa angalizo na baada ya kuchekecha akapotezea.Tunao magamba tunaowakubali lakini ninachojua "TIME WILL TELL NOT SO LONG"
vipi amezungumzia chochote juu ya ile kauli yake aliyoitoa ktk Uwanja wa Namfua Singida kuwa
"ukitaka mambo yako yakunyookee njoo CCM" ? sasa hapo alimaanisha nini kama sio rushwa na kupendeleana.
leo rushwa hiyo hiyo kwa kuwa imemnyima uongozi analalamika ? mkuki kwa nguruwe?
akamuulize mwenzie aliesema akirudi CCM basi amzini mama yake, amerud basi hadi leo akili yake haijakaa sawa, labda hadi amzini kweli.
Nidhani ni press conference ya kutangaza nia!. Kumbe ni press co ya blah blah!.Sumaye yeye sio mtaji lolote, sio mtaji chochote, na akihama CCM, atajihamia yeye kama yeye, hana wafuasi wowote wa kutishia usalama wa CCM!. Angetishia kuhama yule Mzee wa ....ndio CCM ingetingishika!.
Hata hivyo, sifa za kugombea urais kupitia CCM sio ujumbe wa NEC bali ni kwa mwana CCM yoyote mwenye sifa!, hivyo hata kama Sumaye amebwagwa ujumbe wa NEC na ki..da wake, kisa ki..da huyo pia katembea na Muzeiye, hiyo sio sababu ya yeye kuihama CCM!.
Kwa vile Sumaye hata kitu chochote cha maana zaidi tule tujumba alitotujenga kwa mikopo ya kifisadi ya NSSF, then hana jeuri yoyote ya kuihama CCM wakati tegemeo lake ni mafao ya kustaafu ambayo ni 80% ya current PM!. Japo hata akihama pensheni yake iko pale pale, bali masimango yatammaliza bure!.
Wapiganaji wa kweli ni wale ambao wako tayari to take risk kwa kusimama mbali na uvundo kuwathibitishia watanzania kuwa huku tuliko chama kimetekwa na mafisadi.
Wale kina Sumaye type, wanaopigania nafsi zao, mtawatambua kwa kutokubali kuriski nafasi zao ndani ya CCM ambako mafisadi wana upper hand. Kwa vile CCM ina wenyewe, na baadhi ya wenyewe hao ndio hao hao mafisadi na wengine wao ndio hao kina Sumaye, hapa ni mwendo wa mwenye kisu kikali ndie anayekula nyama, maadamu wenye nguvu ni mafisadi, mwenye nguvu mpishe, hao kina Sumaye type watajikuta kuliko kuriski loosing, wakijua hawawezi kuwashinda, watatumia formular ya 'if you can't beat them, join them' watajiunga nao na wote wakuwa kwenye tenga moja la samaki, na wote watakuwa ndio wale wale!.
P.
Katika uchaguzi wa demokrasia, mtu huchaguliwa kwa uwezo na kwa ajili yao kuwatumikia, katika demokrasia ya rushwa, fedha huwachagulia watu mwakilishi kwa ajili ya waliotoa fedha, kama nimetoa fedha kwa ajili yako, na wapiga kura wanakua wapiga mihuri.
Sasa imetoka mtu kuhonga achaguliwe, na sasa mtu anatoa rushwa kununua watu ili apate kujenga mtandao wake na sasa ni rushwa ya kimtandao ambayo ni hatari sana...