Sultan Qaboos karibu Tanzania

albuluushiy

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2013
Posts
1,404
Reaction score
687
Qaboos bin Said Al Said alizaliwa tarehe 18 Novemba mwaka 1940 katika mji wa Salala ulio kusini mwa Oman.Ndiye mtoto pekee wa Sultan Said bin Taimur.Mama yake ni malkia Mazoon al-Mashani.

Elimu ya msingi aliipata mjini Salala na baadae Pune nchini India.Alipofika miaka 16 alipelekwa kwa masomo ya juu nchini Uiengereza.Alipofika miaka 20 aliingia kwenye kikosi cha kijeshi cha kifalme kinachoitwa sandhurst. Baada ya kufaulu mafunzo katika chuo hicho alijiunga na jeshi la kiiengereza na kupangiwa shughuli za kijeshi kwenye bataliani ya 1 nchini Ujerumani ambako alikaa huko kwa muda wa mwaka mmoja na hata kushika nafasi za unadhimu kwenye jeshi hilo la kiiengereza.

Sultan Qaboos baadae aliacha shughuli za kijeshi na  akaanza kuchukua mafunzo ya namna ya kuendesha serikali za kiraia.Baada ya hapo alifanya ziara ndefu ya kuizunguka dunia kabla kurudi nyumbani kwao  Salalah.Alipofika Salala aliisoma dini yake ya kiislamu na historia ya nchi yake ya Oman.

Mwaka 1976 mfalme Qaboos alimuoa bint Ami yake, bi Kamila,nee sayyida Nawwal bint Tariq.Hata hivyo ndoa hiyo haikudumu na tangu aachane na mkewe huyo hajaoa tena na wala hana mtoto.

Mnamo mwezi Julai mwaka 1970 kikosi cha jeshi kilichomuunga mkono Qaboos kilipambana na kikosi cha jeshi cha mfame Said bin Taimur  na kufanikiwa kumpindua baba yake huyo.Serikali ya Uiengereza ilisaidia kuimarisha utawala wa mfalme Qaboos baada ya mapinduzi hayo.

Tangu mfalme Qaboos atawale Oman amefanikiwa kubadili hali za kiuchumi za raia wake na kuleta maendeleo makubwa nchini humo.

Ukoo wa mfalme Qaboos wa Abusaidy ndio uliokuwa na mahusiano makubwa na ukanda wote wa pwani ya mashariki ya Afrika na hata kuwa na utawala wa pamoja ambapo ulijenga makao makuu ya utawala wake nchini Zanzibar ambayo sasa ni nchi ndugu waTanganyika ambazo kwa pamoja zinaunda jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Kwa zaidi ya karne moja raia wa ufalme huo waliweza kupenya kibiashara na kusambaa kote mashariki na kati ya Afrika.

Kutokana na ukweli huo wa kihistoria na mafungamano kati ya Oman na Tanzania zipo kila sababu kwa mfalme Qaboos bin Said kuja kutembelea Tanzania akianzia Zanzibar.

Kutokana na mapenzi makubwa ya wengi wetu kwake siku atakapofika tutajitokeza kwa wingi kwenye mitaa ya Shangani mjini Zanzibar au Kariakoo jijini Dar es salaam kujipanga barabarani kumpokea na kusalimiana nae.

Moja ya maeneo ambayo yanaweza kuwa kivutio na mapumziko ya sultan huyo wa Oman ni mbuga za wanyama za Serengeti,Loliondo na Ngorongoro. Kwa heshima na taadhima na kwa niaba ya wapenzi wa utawala wa Sultanate of Oman nachukua fursa hii kumkaribisha his majesty Sultan Qaboos bin Said aje kuitembelea Tanzania.
 
Anakuja kuchukua nini na yeye kwenye hili shamba la bibi
 
Nilifikiria anakuja,kumbe wamkaribisha.Huyu alitakiwa awajali vizazi vyenye asili ya Oman,waliopo Tanzania.Kwa sababu mababu zao walikuja Tanzania,kutokana na Omani kutawala Zanzibar na Pwani ya Tanganyika.Na pia kuishukuru Tanzania kwa kuwapa haki sawa,waTanzania wenye asili ya Omani.
 
Aanze kuwatambuwa WaTanzania wenye asili ya Omani.Waziri mkuu wa Tanzania amekwenda Omani na kuzungumza na wa Omani Wenye asili ya Tanzania,na kuna mipango mizuri watafanyiwa wanufaike hapa Tanzania.Kwa nini Oman hajishughulishi na vizazi vyenye asili ya Oman,waliopo Tanzania.
 
mbna mapadri hawana wake na maisha yanaenda?ila waache tu kuiba wake za watu kama padri slaa

sharti mojawapo la kuwa padri ni kuishi useja. Sasa kwanini sultan hajaoa tena na wakati mafundisho yanatutaka tuwe na wake wa4?
- Hilo la watoto siliongelei ni kudra za mwenyezi Mungu.
 
Hii topic atakuwa ameleta mzee Mohamed Said kwa mlango wa nyuma. Mzee MS anatamani sultanate of Oman ifike hadi Zanzibar na kila siku anayapinga mapinduzi matukufu yaliyoongozwa na Field Marshal John Okello
 
Hii topic atakuwa ameleta mzee Mohamed Said kwa mlango wa nyuma. Mzee MS anatamani sultanate of Oman ifike hadi Zanzibar na kila siku anayapinga mapinduzi matukufu yaliyoongozwa na Field Marshal John Okello
Mapinduzi ni Mapinduzi tu hakuna issue ya Utukufu wala Utakatifu! Na amini Znz ingekuwa mbali sana kwa maendeleo ya kiuchumi kama si hayo Mapinduzi uchwara!
 
Kikwajuni One siku nyingine si lazima uquote kila kitu.Habari ikiwa ndefu unaweza kumtaja jina tu mleta mada naye akajua kuwa kuna mtu kanitaja bwana Kikwajuni One. Wanaotumia simu wanateseka sana kwa mtindo huu wa kuquote habari ndefu. Heshima mbele mkuu Kikwajuni One ni ushauri tu
 
Last edited by a moderator:
Huyu hausiki na ku injinia babu zetu kuuzwa kwao na kuhasiwa?
 
Unaweza kukuta huyo Mfalme ni mbuzi wa shughuli.

1. Kwanini mke alimkimbia.

2. Kwanini hakutaka kuoa baada ya kuachana na mke wake.

3. Hana mtoto maana yake ufalme wake utakwisha siku mauti ikimfika.

sultan hana mke wala mtoto??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…