Sukuma Gang is Real: Waanza kumtisha Rais Samia, wamtumia Msukuma kudai mkoa wa Chato kinguvu

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,102
36,076
Hili kundi sio la kufikirika lipo na litamtesa sana mama Samia.

Nipo kanda ya Ziwa kiukweli mama yangu Samia huku watu hawakupendi kwa sababu mbili.

Watu wa huku wana mfumo dume hawaamini kama mwanamke anaweza kuwa Rais.

Pili ni wivu tu na roho mbaya,wanaona kama wewe unafaidi matunda ya mwenazake bure

Hawaamini kama utaendeleza miradi ya mwendazake aliyoianzisha kanda ya ziwa.

Kuna mikoa kama Geita hususan wilaya ya Chato imerudi nyuma kimaendeleo,enzi za mwendazake ikulu ilihamia Chato,mzunguko wa hela ukawa mkubwa,sasa hotel za Chato ni makazi ya popo, mji umepooza dorooo.

Sasa wameamua kumtikisa Rais wetu mpendwa mama Samia kwa kudai mkoa wa Chato,katika hili wanamtumia Dk Msukuma kumtisha mama.

Chato haina ardhi wala hadhi vya kuwa mkoa, huo ndio ukweli,mama simamia haki.nadhani ifike muda sasa mambo ya kutengeneza mikoa mipya ywfike tamati.

China USA na Russia ni kubwa ila hawana ujinga huu,kikubwa serikali ipeleke huduma bora kwa wananchi basi kwa kuzisogeza karibu.

Mwisho Sukuma Gang waambiwe kuwa mama yetu Samia yuko pale kitini kwa sababu ya katiba,na waambiwe kuwa Hayati Magufuli aliitwa na Bwana Mbinguni kwa mapenzi yake,
Tutulie tujenge nchi
,waache nongwa.
 
20230117_093205.jpg
 
Mbunge anaweza kumtisha rais?

mbunge wa kongwa bw ndugai aliporopoka alipata kisa gani?

Marehem magufuli aliwah kusema, kuna mhimili uliojichimbia kuliko yote, kwa tafsiri yangu hata bunge halina ubavu, sembuse tajiri, mzurumaji, jambazi mstaafu, mfadhili wa ujambazi na mkwepa kodi daktari msuku?
 
Hawamtishi direct,wanatumia vimaneno fulani kumtisha waziri wa Tamisemi kuwa tunataka mkoa tunataka mkoa wakati wanajua maamuzi ya mwisho ya kuunda mkoa yanatoka kwa Rais,na Rais alishasema vigezo havipo
 
Hili kundi sio la kufikirika lipo na litamtesa sana mama Samia.
Nipo kanda ya Ziwa kiukweli mama yangu Samia huku watu hawakupendi kwa sababu mbili.

Watu wa huku wana mfumo dume hawaamini kama mwanamke anaweza kuwa Rais.

Pili ni wivu tu na roho mbaya,wanaona kama wewe unafaidi matunda ya mwenazake bure

Hawaamini kama utaendeleza miradi ya mwendazake aliyoianzisha kanda ya ziwa.

Kuna mikoa kama Geita hususan wilaya ya Chato imerudi nyuma kimaendeleo,enzi za mwendazake ikulu ilihamia Chato,mzunguko wa hela ukawa mkubwa,sasa hotel za Chato ni makazi ya popo,mji umepooza dorooo.

Sasa wameamua kumtikisa Rais wetu mpendwa mama Samia kwa kudai mkoa wa Chato,katika hili wanamtumia Dk Msukuma kumtisha mama.

Chato haina ardhi wala hadhi vya kuwa mkoa ,huo ndio ukweli,mama simamia haki.nadhani ifike muda sasa mambo ya kutengeneza mikoa mipya ywfike tamati
China USA na Russia ni kubwa ila hawana ujinga huu,kikubwa serikali ipeleke huduma bora kwa wananchi basi kwa kuzisogeza karibu.

Mwisho Sukuma Gang waambiwe kuwa mama yetu Samia yuko pale kitini kwa sababu ya katiba,na waambiwe kuwa Hayati Magufuli aliitwa na Bwana Mbinguni kwa mapenzi yake,Rais samia hausiki na kifo cha Hayati Magufuli na hana uwezo huo ,waache nongwa
Kwani kuna shida gani chato ikiwa mkoa? Mbona mnapenda kukuza mambo kijinga yaonekane yanamaana sana? Mnaacha kuoambania mindege inayotua huko Loliondo mnapambana Chato usiwe mkoa!
 
Mkuu

Mdukuzi ACHA kumchonganisha Rais na WATU Wake!

Mission yako ni Nini!?

Nyuzi zako zinasukuma kete kimya kimya KWA lengo FULANI!

Wenye macho tumeona!

"Rais samia hahusiki na kifo cha jpm"

Nani kamtuhum KWA hilo Hadi unaleta hilo jukwaani!!?

Mmeanza au ndio kile cha kuanza kuvujisha ushahidi wa meseji na sauti Ili kutimiza azma FULANI!!?

Ngoja nione,tuhuma hizo ni kubwa Sana!

"Mungu ibariki TANZANIA nchi yetu niipendayo Sana"
 
Chato haina ardhi kwa hiyo wilaya iko angani?Russia na china huwezi kuzifananisha na Tanzania, hakuna uwiano. Kwanini usitolee mfano wa nchi za afrika mashariki na kati?kwa hali yoyote ile mm naunga mkono chato kuwa mkoa kwa maslahi mapana ya wananchi wanafuata huduma mbali(makao makuu ya mikoa).
 
Back
Top Bottom