Wakati wa mkwamo wa uchumi wa ulaya miaka ya 1930s,ujerumani nayo haikuachwa na mtikisiko huo, alipochukua madaraka Adolf Hitler alionekana kama mkombozi wa hali mbaya ya uchumi inayowakabili. Msimamo wake aliouchukua wa chuki dhidi ya wayahudi akiwalaumu ndiyo sababu ya matatizo yote yaliwavutia watu wengi wakawa wanaimba sifa zake. Kilichotokea baadae dunia hadi leo wanakumbukia, walitengengeneza mmoja wa madikteta aliyesababisha maafa katika historia ya dunia hii.
Dikteta anapenda kusifiwa, hapendi kukosolewa (rejea kesi ya kijana aliyeita bwege), na asiyetaka kukosolewa ataminya uhuru wa vyombo vya habari (kuzuia matangazo live ya bunge) , atataka kuhodhi madaraka yote(bunge, mahakama mifano tunaiona) , ataweza puppets wake ili wawe answerable kwake (tunamuona na mfano ndiyo huyo mama hapo bungeni), wabunge wa CCM nawaomba waendelee kusema tu ndiiiiyooooo! Nawaapia wakija kushtuka na uzwazwa wao it will be too late, haijachukua hata miezi sita tunaanza kuisoma namba, na bado tuna miaka minne na miezi sita TITAKOMA!!!