Sukari: Dr. Ackson Tulia (Naibu Spika), upongezwe?

Sukari: Dr. Ackson Tulia (Naibu Spika), upongezwe?

Leo asubuhi,Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe ( CCM) alitoa hoja ya haja ya dharura kulitaka Bunge kujadili uhaba wa sukari nchini. Bashe alitoa mfano wa bei ya sukari kwasasa,kuthibitisha uhaba uliopo kwa sasa,kuwa kilo moja inauzwa kati ya 3000 na 4000.

Pamoja na kupata uungwaji mkono utakiwayo,kwa Wabunge wenzake kusimama,Kiti cha Spika chini ya Dr. Tulia kiliizima hoja hiyo ya Bashe. Naibu Spika Dr. Tulia alisema kuwa hakuna haja kuwepo mjadala wa uhaba wa sukari nchini kwa kuwa Waziri Mkuu Majaliwa alishatoa taarifa ya serikali.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa Serikali ina nia ya kutoa vibali vya kuagiza sukari. Naibu Spika yuko sawa kuizima hoja ya Bashe?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)

She is right. The PM advised the MP last couple of days that the government had given license to import sugar. Importation process might take some few weeks/ months till the consignment arrive in country and eventually have some impact in the supply
 
Baada ya miaka minne ndo tutaweza kuona serikali ya awamu ya 5 inavyoweza kutatua kero za wananchi.
 
Hivi kuna mtanzania yeyote anaye jua wapi JPM ana ipeleka nchi hii, au ni ushabiki tu. Sababu mpaka sasa tunacho sikia ni kutumbua majipu tu, sija sikia akisema ndani ya miaka mitano hii tuta itoa nchi hapa na kuifikisha hapa au ndani ya miaka kumi ijayo. Hata kama utakusanya kodi vipi lakini kama huna vision na mission hufiki kokote, itabaki kutoa fedha kasma hii kupeleka kule, na kutoa kule kupeleka kule kutokana na matukio ya hapa kwa hapa mwisho muda unaisha ukiwa unapambana na dharula.
Mathink tanks wenyewe ndo akina nape.hapo utagemea nn
 
  1. Leo sukari ya kutumia home nimenunua kilo NNE kwa Tsh. 10,000,,,kutoka elfu 8 kg4, iyo ndani ya hapa Dar, ni hatari
 
Lazima kunywa chai.

Kwa watoto Kama wewe ni lazima mnywe chai,na ndo mnaotushugulisha kununua sukari, ingekuwa sisi wenyewe watu wazima unapiga viazi vyako au mihogo iliyokaangwa na Pepsi au Coca baridi,hapo imetoka,
 
Hoja ya vibali haina uhusiano na majadiliano, kwa nini walizuia uagizaji hali wakijua viwanda vya ndani havikizi, serekali ya jpm ijitafsiri iache kukurupuka
Hivi hata wakiruhusu mjadala kuhusu sukari mwisho wake utakuwa mini?
 
Waziri Mkuu alisema sukari imeshaan
Leo asubuhi,Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe ( CCM) alitoa hoja ya haja ya dharura kulitaka Bunge kujadili uhaba wa sukari nchini. Bashe alitoa mfano wa bei ya sukari kwasasa,kuthibitisha uhaba uliopo kwa sasa,kuwa kilo moja inauzwa kati ya 3000 na 4000.

Pamoja na kupata uungwaji mkono utakiwayo,kwa Wabunge wenzake kusimama,Kiti cha Spika chini ya Dr. Tulia kiliizima hoja hiyo ya Bashe. Naibu Spika Dr. Tulia alisema kuwa hakuna haja kuwepo mjadala wa uhaba wa sukari nchini kwa kuwa Waziri Mkuu Majaliwa alishatoa taarifa ya serikali.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa Serikali ina nia ya kutoa vibali vya kuagiza sukari. Naibu Spika yuko sawa kuizima hoja ya Bashe?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
na itafika karibuni - siyo kutoa vibali. Hata hivyo sioni ni kwa nini Bunge lipoteze muda kujadili kitu ambacho hakitabadilisha lolote. Sukari ni siasa za kibiashara na kimakundi ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom