SUK yaigomea JMT kupelekwa FBI Zanzibar

Status
Not open for further replies.
Yawezekana Zanzibar kuna kitu na watawala wanalifahamu ndiyo maana Maalim alikuja kusikia neno ugaidi.
 
Wao ndio wanashiriki mauwaji, unategemea watakubali waje waumbuliwe?
 
Hayo mambo yakuwaita viongozi majina ya ajabu watu wakianza kumuita Dr Slaa majina ya ajabu nyie ndiyo mnakuwa wa kwanza kulia lia.
Mimi najua wewe unamwita Padri binafsi sijalalamika, sijui jitihada za kukanusha mtu kuitwa Dhaifu ziliishia wapi?
 
Mkuu Ngongo,
Mbona tunaambiwa FBI tayari wapo Zanzibari.

Kamishna wa jeshi la polisi zanzibar, hana taarifa za ujio wao na amekanusha uwepo wao visiwani humo....we taarifa hizo umezitoa wapi? Mlicheka na nyani sasa mtavuna mabua!
 
Serikali ya Zanzibar ndiyo inayoratibu ugaidi Zanzibar hasa Maali Seif, hakuna mtu anayeweza kukubali kuja kuumbuliwa. Ila iwe isiwe huu muungano ni lazima tuuvunje.
 
Mkuu Ngongo,
Mbona tunaambiwa FBI tayari wapo Zanzibari.

wameshagawanywa tayari watano zenji, watano mtwara watano Dar na kumi watatembelea baadhi ya maeneo kuliko na hisia za machafuko niliwaona jana pale Makumbusho
 
Mkuu sifongo unajua Zanzibar walitengeneza katiba yao mpya ambayo kwa kiasi kikubwa inakiuka katiba ya JMT .Hili jambo limeshazungumzwa sana na Tindu Lissu bahati mbaya bunge la Mama Makinda wakalifinyanga finyanga.
Mkuu Ngongo, hapo ni patamu sana. Mtu alimfuga chui na baadae chui akamtafuna mtoto wa mfugaji!
 
Mkuu wangu Ritz leo nilikuwa napata supu mitaa ya Arusha City Park nilikaaa meza moja na afisa nyeti akawa anaropoka jinsi wazanzibar wanavyompelekesha Dr Kikwete hadi wanazuia maagizo yake ikiwemo hili la FBI kupelekwa Zanzibar.
Halafu tanzania nchi ya ajabu sana kuna wakati maafisa nyeti kabisa utakuta linaropoka bila kujua linaongea na watu gani? kuna jamaa mmoja usalama wa kikwete siku moja nimekaanae kwenye basi akaanza kumwaga siri za serikali huku yeye akijitambulisha mpaka anakotoa na ukoo wake wako wangapi yeye ni mtoto wa ngapi watu tuamsikiliza tu, binafsi mimi nilijiuliza hivi hawa ndiyo usalama wa kikwete anao wategemea....
 
FBI hawana haja ya kuomba ruhusa yako.......hata wasipoombwa watachunguza tu.....
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Heshima kwenu wanajamvi,

Taarifa toka chini ya kapeti zinasema Serekali ya umoja wa kitaifa Zainzibar chini ya uongozi wa Dr Shein na makamu wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad wameikatalia serkali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania chini uongozi wa Amiri jeshi mkuu Dr Jakaya Mrisho Kikwete kupeleka kikundi cha kijasusi Zanzibar kwaajili ya upepelezi mauaji ya Padre Mushi.

Habari zilizozagaa mitaani kwamba Rais Kikwete ameomba msaada wa mashirika ya kijasusi toka mataifa ya kigeni kusaidia upelelezi uenda zikakwama ikiwa serekali ya SUK itaendelea na msimamo wake.

Naomba kuwasilisha.

Mkuu, weka habari iliyo juu ya kapeti. Hii habari ya chini ya kapeti ni sawa sawa na "uzushi"...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom