Jamani anaekataa umuhimu wa Mh Mbilinyi mbunge wa Mbeya mjini hakika wanatatizo la kifkra na wanatatizo pia kwenye mioyo yao na dhamira zao ni za kishetani,nawashauri wapitie blog ya Mbeya yetu.com waone picha za umati ulikuja kumsikiliza mbunge wao aliekuwa anasubiriwa kuleta amani ndani ya jiji la Mbeya,mkuu wa mkoa Kandoro hakusikilizwa na watu anaowaongoza wala mkuu wa wilaya Balama leo alipotaka kuongea wananchi wakasema hakukusanyika kumsikiliza yeye ikalazimika akae,na ndipo alipoanza mbunge wao kuhutubia.umati huo sio kitu cha kubeza,na amani iliyorudishwa kwa juhudi za Mbilinyi sio za kubezwa,kumbuka polisi jana walielemewa na ikabidi JKT kuingilia kuwasaidia hata leo JWTZ walikuwepo kuongeza nguvu ya usalama hasa baada ya kuona watu wamekuja kwa wingi sana.sasa nyie mnaohangaishwa na roho za kutu,za wivu,za kinafiki na msiokuwa hata na aibu mnabeza mambo aloyafanya Sugu jijini mbeya,kweli hii ni hatari ya CCM.Nendeni mkamuulize Kandoro na Balama watawaambia mziki wa mbeya,mapambano yalikuwa si mchezo,serikali ya mkoa na CCM yote walishindwa kuumaliza wala kuwatuliza wananchi wa Mbeya. JIFUNZENI KITU JUU YA TUKIO HILI SIO KUBISHA KAMA WENDAWAZIMU