kama kweli lissu anajua kwamba kupeleka kesi hii mahakamani ni umbumbumbu wa kisheria na pia atakuwa anavunja ama kukiuka katiba iliyopo, basi ni dhahiri kwamba tendo lile lilifanyika kwa makusudi kwa kujua kwamba mbunge ana hiyo kinga.
kama ukiaangalia footage ile, mh. sugu hakuonekana kumtishia askari kwa kuaka kumpiga akiwa ndani ya bunge, ingawa alitolewa nje kwa njia ya kushusha heshima kidogo. ila muendelezo wa footage inaonesha nje ya ukumbu sugu anamvamia askari.. naamini kama kweli wabunge wa upinzani walitoka nje wote ni naweza kuamini kwa njia moja ama nyingine kwamba sugu alishawishiwa kufanya aliyofanya kwa sababu tu kuna kunga ya mbunge ama ndani ya bunge ama kwenye viwanja vya bunge.
kwa upande mwingine, nadhani kamati ya nidham na maadili ya wabunge kama ipo na kufanya kazi basi ni vema ikachukua hatua yake. hatuwezi, binafsi siwezi kukaa na kuona utovu wa nidhamu unaoletwa na baadhi ya wabunge ambao naweza kusema wana upeo mdogo sana kwenye siasa na nyanja zake zote. kutoka kwenye jukwaa lakuimba matusi na kushabikiwa na watu ndo unataka kuleta bungeni
kama ni kweli mh sugu anataka kutetea wanyonge ama kupigania haki kama navyosema, basi ni dhahiri ajenge hoja sio kutumia nguvu kulaimisha umaarufu. aige mfano kwa kina mnyika, slaa, mbowe na hata zitto na lissu pia..