Dodoma: Mbunge 'Sugu' afikishwa Mahakamani na Kushinda Kesi ya Kumuita Waziri Mkuu 'Mpumbavu'

Status
Not open for further replies.

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,780
3,208
Leo asubuhi Joseph Mbilinyi (Sugu) alipelekwa mahakamani kwa shitaka la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu, shtaka hili lilifunguliwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma na mwendesha mashitaka wa serikali.

Baada ya kufunguliwa shtaka hilo, Lissu ambaye alikuwa wakili wa Sugu aliitaka mahakama ifutilie mbali shtaka hilo kwani halina msingi wowote wa kisheria na baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na wanasheria wa serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno Mpumbavu ni lugha ya matusi, hakimu ameamua kufuta shtaka hilo na ametangaza kuwa Sugu yuko huru na hana kesi ya kujibu.

Muda huu ndio wanaondoka mahakamani, Sugu, Lissu na baadhi ya wabunge na viongozi wa CHADEMA ambao walikuwa mahakamani hapo.

My take:
Polisi na serikali, mnaendelea kujidhalilisha kwa kufungua kesi ambazo zinaendelea kuwavunjia heshima mbele ya mahkaama na umma wa watz. Acheni kufuata maelekezo ya kina Mwigulu, hawajui sheria, hawajui misingi ya kufungua kesi, nyie kila siku mtakuwa mnafungua kesi mpaka lini wakati mnashindwa.

UPDATES :

Kesi ilikuwa namba 131 ya 2013 na hakimu aliyeisikiliza hiyo kesi anaitwa Elineza Luvanda, nimeweka updates hii kwani naona kuna watu wanapotosha kwa kuanzisha thread za kusema wako Dodoma na ni uongo.
 
Tanzania UPUMBAVU hautakaa uishe kamwe chini ya hawa Magamba!!
 
Mh! halafu wanataka wapelekewe ushahidi wa mbowe khs bomu kule arusha,hivi hakuna jinsi polisi wetu angalau wawe na masomobya jioni juubya majukumu yao?maana naona kama wengi hawana vigezo vile.
 
kwa umuhimu wa ulichoandika mkuu Haki sawa nimestuka mpaka nashindwa kukuamini bali tu kutokana na reputation yako hapa jamvini naweza kuamini haya!!!
Nilichoandika ni sahihi ,ni kuwa juzi alipotakiwa kwenda polisi alienda na Lissu kama wakili wake yakatokea mabishano makubwa sana ya kisheria kuhusu account hiyo na uhalali wake na pia kuhusu Upumbavu kama ni tusi ama laa, polisi wakamtaka Sugu leo aripoti polisi kama kawaida kaenda asubuhi na polisi wakamshikilia kuwa wanampeleka mahakamani , na kweli alifikishwa mahakamani majira ya saa nne asubuhi leo , kukatokea ubishani wa kisheria kuhusu shitaka la kuwa Sugu alimtukana PM na hivyo ni kinyume cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai , hapo ndipo Wakili wa Sugu Lissu alipoweka pingamizi la awali kuwa hakuna kesi ya kujibu kwani mwendesha mashitaka ameshindwa kuonyesha tusi alilotukanwa Pm , ndipo akaitaka mahakama itupilie mbali shitaka hilo kwani halina msingi wa kisheria .

Hakimu aliyekuwa anasikiliza shauri hilo baada ya kupitia kwa kina hoja za pande zote mbilialiamua kutupilia mbali shtaka hilo kwa kuwa upande wa serikali umeshindwa kuithibitishia mahakama juu ya hilo tusi .
 
hata kama ingekuwa ni tusi ni ngumu kuthibitisha
1. Account hiyo ni ya Sugu
2. Aliandika akiwa ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano. Inabidi ithibitishwe kama amepost nje ya nchi inabidi ukafungue mashtaka katika nchi hiyo uhalifu ulipotendeka.
3. mlalamikaji ni nani?
 
Napenda kuiuliza polisi: Hivi mtu anayetumia ubongo wake kinyume na matarajio ya wengi na kinyume na Mungu aliyouumba ufanye kazi anaitwa nani?!
 
Baada ya kuthibiti hivyo pia walitakiwa kuthibitisha account haikuwa hacked then mwisho waiambie mahakama kama neno 'pumbavu' ni tusi, tendo, kiwakilishi au sifa.

Baada ya kuthibitisha kuwa ni tusi au sifa, wathibitishe hana sifa hiyo ndo walipaswa wakafungue kesi.
 
Leo asubuhi Sugu alipelekwa mahakamani kwa shitaka la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu, shtaka hili lilifunguliwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma na mwendesha mashitaka wa serikali.

baada ya kufunguliwa shtaka hilo , Lissu ambaye alikuwa wakili wa sugu aliitaka mahakam ifutilie mali shtaka hilo kwani halina msingi wowote wa kisheria na baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na wanasheria wa serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno Mpumbavu ni lugha ya matusi , hakimu ameamua kufuta shtaka hilo na ametangaza kuwa Sugu yuko huru na hana kesi ya kujibu.

muda huu ndio wanaondoka mahakamani , Sugu, na Lissu na baadhi ya wabunge na viongozi wa chadema ambao walikuwa mahakamani hapo.

my take: Polisi na serikali , mnaendelea kujidhalilisha kwa kufungua kesi ambazo zinaendelea kuwavunjia heshima mbele ya mahkaama na umma wa watz. acheni kufuata maelekezo ya kina Mwigulu , hawajui sheria , hawajui misingi ya kufungua kesi , nyie kila siku mtakuwa mnafungua kesi mpaka lini wakati mnashindwa kila leo?
Yaani wameshindwa kuthibitisha kwamba mpumbavu ni tusi, sasa walifungua kwa misingi ipi? kweli mtu kama unatumika, yaani uwezo wako wa kufikiri unakutoka kabisa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom