Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 55,030
- 59,682
Naye Meneja Uhusiano wa Tanapa, Paschal Shelutete alikiri kufahamu jambo hilo na kusema: Leka Dutigite ilifika Hifadhi ya Saadan na kuitangaza kupitia kazi za sanaa... sikumbuki ni lini lakini walifanya kazi na DvD zake zipo.
Ifahamike si Leka Dutigite pekee, tunafanya kazi na wasanii mbalimbali kutangaza vivutio, mbuga na hifadhi zetu, alisema Shelutete.
NSSF nayo yalonga
Meneja Kiongozi wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume alisema pesa walizozitoa kwa kundi hilo zilikuwa malipo ya kutengenezea wimbo maalumu wa shirika hilo na nyingine ni za udhamini wa onyesho lililofanyika mwaka jana mkoani Tanga.
Kweli mara ya kwanza tuliwalipa Sh25 milioni wasanii wa kundi hilo ili watutengenezee wimbo na Sh56 milioni zilikuwa za udhamini wa onyesho lao, lakini kwa masharti ya kututangaza jambo ambalo lilikuwa na mafanikio kwetu kwani tumefanikiwa kupata wateja wapya 30,000 kutoka sekta isiyo rasmi, alisema Chiume.
Alisisitiza kuwa wametumia kiwango hicho cha pesa ili kujitangaza kwa kuwa hata mashirika ya kijamii yanapaswa kufanya hivyo ili kuvutia wateja wengi zaidi.