Sugu Kakurupuka? Je anajenga ama anabomoa?

Sugu Kakurupuka? Je anajenga ama anabomoa?

wanafiki hawajifichi, watadhihiri tu.
cdm kwa mwendo huu inazidi kudhalilika.
ni ujinga wa hali ya juu chama kupigana vita na mtu mmoja, mnamjengea umaarufu na ujasiri zaidi huku wenyewe mkijishusha na kujidhalilisha

Tumia akili na siyo unakurupuka,Sugu alikuwa anawakilisha maoni ya kambi ya upinzani,siyo yake binafsi au ya chadema kama unavyotaka kutuaminisha.Wacha ushabiki Wako husio na manufaa kwa Uma.
 
Unajua hii nchi ina mapungufu mengi sana ya kisheria na kwa wanasiasa makini hutumia hizo "loopholes" hata kama CAG ataikagua ZZK Co.(Leka Tutigike) ataonekana msafi kwa sababu ametumia hizo weakness za kisheria, ni jukumu letu Vijana wa kizazi hiki kuacha kushabikia wanasiasa,Kukaa siku nzima kumpamba Zito ama Mbilinyi, haileti sense..ukifatilia mchakato mzima na kwa watu wanaojua media(Advertisement) utajua tu kuna pesa chafu lakini wenye documentantion za kutosha,kwa hili suala ZZK ni ataonekana msafi ingawa ni mchafu..Tujaribu kuifikiria na kuweka nguvu zetu kwenye katiba tuitakayo (WANANCHI) na ndo njia pekee ya kuliokoa Taifa hili..
 
Anataka sifa za kijinga kwa kuzushia wengine uongo japo hatashinda kwenye vita hivi elimu yenyewe ndiyo vile mwenzangu na mie.
 
Zitto zuberi Kabwe, naamini hata siku moja CDM watakapopishana na mnyika ama Sugu tutayajua na wao madudu yao. Hamna msafi CDM wala ndugu zao CCM. Nasema haya kwa sababu CCM ni ukoo wa Panya lakini CDM baadhi yao wametokana na ukoo wa Panya. Kwa hiyo ninachojifunza hapa Panya wana koo nyingi, kuna wale ambao huwa tunawafanyia mazoezi maabara panya weupe wale, lakini wale nao ni panya japo tunawafuga na wanamafaida kwetu ila watabaki kuwa panya tu, siku tukiwasahau watatuibia kama hawa panya weusi. Kwahiyo sishangai kinachomtokea zitto na chadema yake maana wote ni koo za panya na hii imeshajidhihirisha sasa. Zitto cha msingi ajibu hoja kwa panya wenzie maana ameshachafuka na sasa ameshakuwa panya mchafu. Hahahaha CCM na CDM wote ni zao la ukoo wa panya.
 
nahisi kutakua na mgogoro wa kimaslahi, ilitakiwa itangazwe tenda ya mtu au kikundi kinachoweza kutunga huo wimbo, ili uchaguliwe wimbo mzuri, pia katika matumizi ya pesa yaendane na VFM- Value for money,
milioni hizo ili kupapa wanachama wa mfuko, inamaana hakuna njia mbadala ya kutafuta wanachama kutunga mziki huo? ina maana watanzania ni wajinga kiasi kwamba mpaka watungiwe mziki ndio wanajua umuhimu wa kitu fulani? kama ni hivyo watunge muziki kwa kila kitu ambacho kipo mbele yetu na serikali iwe inalipa, msaniii kama una wazo la kutunga wimbo unatunga tu, just imagine ferooz angepewa pesa na TTACAIDS ndio atunge wimbo wa starehhe
 
Naye Meneja Uhusiano wa Tanapa, Paschal Shelutete alikiri kufahamu jambo hilo na kusema: "Leka Dutigite ilifika Hifadhi ya Saadan na kuitangaza kupitia kazi za sanaa... sikumbuki ni lini lakini walifanya kazi na DvD zake zipo.

"Ifahamike si Leka Dutigite pekee, tunafanya kazi na wasanii mbalimbali kutangaza vivutio, mbuga na hifadhi zetu," alisema Shelutete.

NSSF nayo yalonga

Meneja Kiongozi wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume alisema pesa walizozitoa kwa kundi hilo zilikuwa malipo ya kutengenezea wimbo maalumu wa shirika hilo na nyingine ni za udhamini wa onyesho lililofanyika mwaka jana mkoani Tanga.

"Kweli mara ya kwanza tuliwalipa Sh25 milioni wasanii wa kundi hilo ili watutengenezee wimbo na Sh56 milioni zilikuwa za udhamini wa onyesho lao, lakini kwa masharti ya kututangaza jambo ambalo lilikuwa na mafanikio kwetu kwani tumefanikiwa kupata wateja wapya 30,000 kutoka sekta isiyo rasmi," alisema Chiume.

Alisisitiza kuwa wametumia kiwango hicho cha pesa ili kujitangaza kwa kuwa hata mashirika ya kijamii yanapaswa kufanya hivyo ili kuvutia wateja wengi zaidi.
Kwako Ms Chiume - mliwapataje wasanii hawa? Mlitangaza tenda wasanii mbalimbali wakaomba kazi ya kutengeneza wimbo wimbo? Leka Dutigite wakaibuka kidedea - au ilikuwaje?
 
wanafiki hawajifichi, watadhihiri tu.
cdm kwa mwendo huu inazidi kudhalilika.
ni ujinga wa hali ya juu chama kupigana vita na mtu mmoja,
mnamjengea umaarufu na ujasiri zaidi huku wenyewe mkijishusha na kujidhalilisha

Dah! Mkuu umeongea umeongea lugha nzito! yenye hekima ya hali ya juu! Lakin ndio hivyo tena lakuvunda halina ubani.


Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
Tumia akili na siyo unakurupuka,Sugu alikuwa anawakilisha maoni ya kambi ya upinzani,siyo yake binafsi au ya chadema kama unavyotaka kutuaminisha.Wacha ushabiki Wako husio na manufaa kwa Uma.
ni ujinga wa hali ya juu chama kupigana vita na mtu mmoja,
mnamjengea umaarufu na ujasiri zaidi huku wenyewe mkijishusha na kujidhalilisha



Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
uyu bwana sugu msamehen tu :der: pasua kichwa kweli nae ka mlev vile.,,,.😛hoto:
 
Back
Top Bottom