Sugu aunguruma Bungeni, atetea kazi za wasanii

Mi binafsi amenikosha moyo wangu,
Ameongea mambo ya msingi sana kuhusu wizara hiyo
Big up Mr Sugu
 
hivi analitendea haki jimbo lake la mbeya kwa
kuzungumza sana kuhusu wasaniii???????????
mkuu, huu jamaa yuko sawa sana japo kuwa hapa tanzania alifahamika sana kwa nyimbo ambazo watu walikuwa hawazikubali sana na pia kutokana na hali hiyo hata uwezo wa kujenga hoja na kufanya shughuli za maendeleo alikuwa haaminiwi na watu lakini ...........mambo yako poa sana!!!!!
 
Kama kila mbunge ingekuwa kazi ni kuzungumzia jimbo lake,je issue za kitaifa azungumze nani? Big up mheshimiwa J.Mbilinyi
 
Ni ujinga mtupu kumshabikia mpuuzi kama huyu. Mbeya tumekubali tuna mbunge kivuli mpaka 2015
 
CDM wako makini sana. Wanatoa hotuba ambazo ziko detailed na zinagusa kila sector katika wizara husika. Walao wanawakumbusha wahusika serikalini nini wanatakiwa kufanya.
 
Bravo Kijana, tatizo magamba kila watakachokisema CDM hawakitaki, hata siku mtu akiomba muongozo kuna moto watabisha tu
 
Sugu ananikosha sana.anachonifurahisha mweshimiwa huyu ni kwamba,kila siku anakuwa zaidi kiupeo na kiuwasilishaji hoja na uchangiaji bungeni.ameongea mambo ya msingi sana na yenye kutetea pande zote za wizara husika tofauti na waziri husika aliyeongelea suala la mpira wa miguu.
pongezi sana sugu,tuko pamoja mpaka kieleweke


I suggested that such an increadible speech would have been presented by not virtual MP from CDM but by actual CCM michezo utamaduni na muzic. A comprehensive speech addressing current issues. I loved it
 
Sugu anajitahidi sana, ni mtu wa kujifunza, atafanya vizuri kadri siku zinavyokwenda. Ruge na Clouds wataanguka. Kwenye biashara tunasema wameshafika kwenye kileleni na sasa wanaanza kushuka /kuporomoka, wataporomoka mpaka chini, just wait and see?

Nasikia wameboronga kwenye Fiesta kuruhusu watoto kuingia, tupeni data.
 
Verygood tunataka wawakilishi kama hawa sekta anaijua na anaichambua vizuri,sio mambo ya magamba mtu hajui kitu chochote kuhusu nishati eti anapewa uwaziri wa nishati na madini,AMENIKOSHA SANA HUYU KIJANA ANAYEITWA SUGU BIG UP C H A D E M A.
 
Ebwana mimi kanikosha alipoulizia sanaa pub. Kumbw ile club ushauzwa na wajanja?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom