Sudan Kusini yaongeza muda wa Serikali ya mpito kwa miaka 2

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Viongozi wa Sudan Kusini wametangaza hii leo kwamba Serikali ya mpito ya nchi hiyo itasalia madarakani kwa miaka miwili zaidi ya muda uliokubaliwa, katika hatua ambayo washirika wa kigeni wamesema inakosa uhalali.

Waziri anayehusika na masuala ya baraza la Mawaziri Martin Elia Lomuoro, amesema uamuzi huo ulichukuliwa ili kushughulikia changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa makubaliano ya amani, kufuatia muafaka wa mwaka 2018, uliokomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka mitano, ambamo watu karibu 400, 000 waliuawa.

Sudan Kusini ilipaswa kufanya uchaguzi Februari mwakani, lakini serikali mpaka sasa imeshindwa kutimiza masharti muhimu ya makubaliano, ikiwemo kuandaa katiba mpya.

Kundi la mataifa matatu wafadhili wakuu wa Sudan Kusini, ambayo ni Marekani, Uingereza na Norway limesusia tangazo la leo, likisema Serikali haikushauriana na pande zilizohusika na makubaliano ya 2018 kabla ya kutangaza urefushaji huo.
 
Afrika na jinamizi lake la kung'ang'ania madaraka limegoma kutuachia, ni shida sana.
 
Back
Top Bottom