Sudan Kusini: Rais Salva Kiir avunja Bunge

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
154
500
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amelivunja bunge katika hatua iliyosubiriwa kwa muda mrefu, akipanga kuwateua wabunge wapya kutoka pande mbili zilizokuwa na mzozo nchini humo.

Msemaji wa Kiir amewaeleza waandishi wa habari siku ya Jumapili kuwa bunge jipya litaunda muda si mrefu, ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyotiwa saini kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza mwaka 2013.

Makubaliano hayo yanataka kuongezwa kwa idadi ya wabunge, kutoka 400 wa hivi sasa hadi kufikia 550, na lazima bunge hilo lihusishe watu kutoka pande zote mbili zilizokuwa katika mzozo.

Mzozo wa Sudan Kusini ulianza mwaka 2013 baada ya Rais Kiir, kutoka jamii ya Wadinka alipomfukuza kazi makamu wake, Riek Machar kutoka Kabila la Nuer.

Wawili hao wamewahi kusaini mikataba mingi kumaliza mgogoro baina yao, ambao umesababisha vita vya zaidi ya watu 400,000, wakishindwa kukubaliana kufikia Serikali ya Umoja wa Kitaifa hadi mwaka 2020.

Licha ya kufikia makubaliano, mapigano bado yanaendelea katika baadhi ya maeneo ya nchi, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Chanzo: Reuters
 
Kv100

Senior Member
Apr 13, 2021
179
250

South sudan is a failed State. Ukabila, corruption na lack of governance vimetamalaki.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom