Suala ya Pensheni laibuka Bungeni, Lissu na Zitto watoa hoja, Mhagama ataka lijadiliwe kikamati



Duuuuuuuuuuuuuuu.ndiyoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
 
Kwa Bunge lilivyosasa si sheria zote zinazopitishwa Bungeni wabunge walikubaliana nazo bali wanatimiza wanachotaka watawala. Kwa hii sheria ya mifuko ya jamii tutahitaji HANSARD ili kila mwanajimbo ajiu mbunge wake alichangia nini. Mlioko mjengoni tunaomba HANSARD za mjadala wa sheria ya mifuko ya jamii

Tafuta kuna thread imeweka ansard.
 
This is ridiculous! Vijana wa sasa tunaishi leo siyo kesho. Wengi hutuna mpango wa kufanya kazi za kuajiriwa hadi kustaafu bali tunatafuta mitaji tujiajiri. Hivi serikali inapopiga kelele watu wajiajiri bila kuwapa mitaji wanategemea nini?Sisi wengine tunategemea michango yetu iwe mitaji mambo ya kufikisha miaka 60 ni mawazo mufilisi kabisa na haikubaliki! Kama serikali inajali wastaafu ingeonesha mfano kwa wazee wa Africa masharika wanaopuliziwa maji ya kuwasha kila siku. Kwa hili serikali ya CCM iwe makini kama inataka kuendelea kututawala. Hivi inawezekana kukopeshwa nyumba ya m.60 au 80 wakati umechangia m. 10 au 15 tu? Kwa wale wanaocha kazi na kujiunga na mashirika ya kimataifa yenye mifumo yao ya pension kama UN, AfDB,WB na mengineyo na wale wanakwenda kufanya kazi nje ya nchi inakuwaje? Hii SSRA naona inajitahidi kuiondoa CCM madarakani!!! Kwa hili wafanyakazi tupo pamoja!!!!!
Hiki ni kipimo kwa wabunge wote!Ngoja tuone hiyo saa saba yatajiri mambo gani.

Absolutely ridiculous!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
wabunge wa CCM hawakumzomea Lissu kwa vile hoja ilipitishwa na bunge! Walichowaza ni kama vile mh Lissu anataka kuiteka hoja yao ambayo imetolewa na mh Jaffo mbunge wa kisarawe.

Hoja ya wabunge wa CCM ama hoja yetu sisi wananchi wafanyakazi wa Tanzania?
 
Kwa Bunge lilivyosasa si sheria zote zinazopitishwa Bungeni wabunge walikubaliana nazo bali wanatimiza wanachotaka watawala. Kwa hii sheria ya mifuko ya jamii tutahitaji HANSARD ili kila mwanajimbo ajiu mbunge wake alichangia nini. Mlioko mjengoni tunaomba HANSARD za mjadala wa sheria ya mifuko ya jamii


bahati nzuri mi ninayo..hii hapa..hicho kipemgere cha kuzuia mafao ya wafanyakazi kimechomekwa baada ya sheria kupita
 
Watanzania memory ya watanzania imebaki kb ndogo sana kama ilivyoshuka umri wa kuishi.

Leo, ulimboka akishuka nchini na kuitisha press conference, ishu ya mafao, urais wa zito, msg za mwigulu hazitajadiliwa tena.

Headline itakua Dr Uli awataja wauaji wake.
 
Nimeshangazwa sana na unafiki wa Wabunge na hata Mwenyekiti Jenister Mhagama. Hii sgeria wameipitisha wenyewe miezi michache tu iliyopita, leo wanaona ati haina maslahi ya wananchi.
Sina imani na hili Bunge, wanakula kodi zetu bure.
 
CCM ni matapeli, inawezekana mswaada uliokuwa umepelekwa Bungeni ni mwingine na alio saini rais na kuwa sheria ni kitu kingine, Haiwezekani mswaada kama ule upite ukiidhinisha dhuluma kwa wafanyakazi wake
Wengi wanashangaa ilikuwae wabunge wa so called upinzani hawakuliona hili kabisa!!!!! Ukweli ni kuwa, Serikali inawajua vizuri hawawabunge na inaelewa jinsi ya kuwa tune, waliporushiwa fupa la tume ya katiba wakasahau kila linaloletwa bungeni.
ni kweli maswali hapa inabidi yaongezeke juu ya suala hili!
Kuna mswada ambao Dr. Slaa aliibua na kusema kuwa rais alisaini kitu tofauti na kilichopitishwa na wabunge na ikadhiirika baadae kuwa ilikuwa kweli, nadhani waziri aliyehusika hapa alikuwa Mh. Phillip Marmo.

Je, ina maana raisi naye hapa hakusoma na kushauriana na wasidizi wake?
Kama hayo yote hayakutokea basi kutakuwa na makusudi fulani na kilicho wazi ni kuwa inawezekana kuna watu hawana nia njema na nchi hii au wamejisahau kupita mipaka. Ngoja tusubiri

 
Niliwahi kusema juu ya mvutano wa vyama bungeni na kukomalia mambo ya kujisafisha kwa CCM ya kutafuta wafuasi kwa CDM na haya ni matokeo madogo sana kwani zipo sheria nyingi tu walizozipitisha bila kusoma kwa umakini na kupata maoni ya wananchi tena wapiga kura.

Hili liko very direct,so tusibirie mengine makubwa zaidi ya haya.sheria haijaanza kazi inafanyiwa marekebisho wanatumia pesa za wananchi kukaa bungeni kusema ndio wengine kususia bunge na utoro.

sijui tanzania ni nani ataikomboa.hatuna uzalendo na uchungu wa nchi yetu sasa kizazi kinachokuja ndo balaa kwani waliondoa hata kale kasomo cha urai na kukaita maarifa ya jamii.
 
bahati nzuri mi ninayo..hii hapa..hicho kipemgere cha kuzuia mafao ya wafanyakazi kimechomekwa baada ya sheria kupita

Niwakumbusha mapema kwani hii iliwahi kutokea mwaka2009 baahati nzuri DR slaa dr.WA UKWELI akawa makini.Huyu babu mimi namkubali sana ni makini kuliko unavyoweza kufikiria HAKUNAGA KAMA DR.Slaa put away all ushabiki na chuki the guy deserves to our next presidaaaaaaaaaaaa.

Wabunge wetu waweke mazoea ya kufanya RECONCILIATION ili kuhakiki walichokijadili na kile kilichopitishwa yaani kuwepo na internal check ot enhance controls over forgery.
Leo litakuwa somo kwa wabunge wetu kuwa JK ni wa ku-handle with care anapenda sna forgery.Nadhani hakuamini siku slaa alipomshushua juu ya kipengeere kilichochomekwa

Werema anakichwa cha kufuga nywele au cha kutumia kufikiri??????????????????????????????

 
Kuna uwezekano hicho kifungu kilichomekwa makusudi baada ya kutoka bungeni maana hawa jamaa kwa hila sishangai kuna wakati tena walichakachua sheria nafiri ya gharama za uchaguzi na wabunge wakashtuka
 
Amini usiamini hiki kipengere kimemekwa baada ya sheria kupita mimi nilifuatilia kusikiliza bunge hii hoja ilipopelekwa bungeni april 2012 hakikuwepo wala wabunge hawakujadili.Kinachogomba hapa hawa wabunge wetu hajajua wajibu wao.Wanatakiwa kufuatilia kila sheria zinaposainiwa na mkulu kuona kama inafanana na ya mwanzo.Inabidi wabunge wafuatilie ili kama ikionekana kilichopmekwa wai-task serikali kwa forgery

hawakua makini kusoma mswada walikua na harakati tu angalia hansard ya april 13 kwenye web ya bunge
 
Wabunge wa ccm watachakachua maana hawa ni zaidi ya Vilaza ...
Wabunge wa upinzani kwa sasa nao wanalala sana. make hakuna hoja ya msingi wanaanzisha siku hizi.
 
Wabunge huwa na mechi za kirafiki na mashirika ya hifadhi za jamii..
 
hata hvyo wamechelewa sana mkanganyiko huu umechukua muda mrefu sana mpka raia wameanza kureact ndo wanashtuka, ukweli ni kuwa bunge letu ni dhaifu kwa ujumla wao,nakumbuka kuna thead nyingi humu ziliwaita hata wabunge wetu wa upinzani japo watupe ufafanuzi nao hakuna hata mmoja aliyejitokeza iliniuma sana BUNGE DHAIFU HUTUNGA SHERIA DHAIFU ZIKIMKUTA NA RAIS DHAIFU HUZISAINI HARAKA.
 
Hoja ililetwa na mhe.Jafu wa ccm;sawa ila waliyosema ndiyo kipindi cha bunge la April walikuwa wengi which means ni ccm ndio waliikubali mswada huo upite coz ndio wengi bungeni.Kuna wa kuwazuia ccm wasipitishe wanachokitaka bubgeni?

Ni kweli kabisa tumeshuhudia hoja nyingi zikipita kwa mtindo wa NDIOOOOOOOOOOOO!!!!!!

Mfano Bajeti iliyosomwa bungeni mwezi June 2012, ilipita kwa NDIOOOOOOOOOO!!! za wabunge wa CCM. hivyo hata hili pia lilipitishwa na CCM kwa kiburi cha wingi wao. Wasijitetee leo baada ya kuona wananchi tunalalamika, wao wanaweka siasa hata katika maisha ya Binadamu kwa manufaa yao tu ya kisiasa.

Ni wakati kwa wabunge wetu pasipo kuangalia itikadi kuwa makini katika kupitisha hoja bungeni. Wananchi tunafuatilia ingawa hatuna sehemu ya kuongelea utumbo unaofanyika bungeni zaidi ya kusubiri mwaka 2015 katika sanduku la kura tutakutana tena kwa wote wanaoshabikia NDIOOOOOOOO!!!!!!




MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom