Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 31,279
- 32,323
Nawasilisha maoni haya kwa Mamlaka husika, leo asubuhi nimeshuka Magufuli terminal kwa bus na kushushwa kama watawala walivyoamuru, tukiwa wengi tu, tukavuka kwenda upande wa pili kutafuta daladala za kwenda mjini, kiukweli, nimejifunza ule usemi wa "mwenye shibe hamtambui mwenye njaa" una maana kubwa sana, Jiji la Dar bado lina changamoto kubwa sana ya usafiri, kiuhalisia RC wa Dar anatakiwa kujitathimini kama kweli maamuzi aliyotoa yalifanyiwa utafiti wa kina juu ya zuio la mabasi makubwa kutowapa msaada wasafiri wanaoelekea mjini. Narudia kutoa ushauri, ninawaomba watanzania wenzangu tuungane kwa mara nyingine kuisihi serikali kuu kulitazama kipekee jambo hili.
- Makamu wa Rais akiwa Kigoma Juzi amewatahadharisha wana Kigoma kuwa makini juu ya Covid 19, hii ikiwa ni pamoja na mikoa mingine 9 yenye takwimu za uwepo wa ugonjwa huo kwa asilimia kadhaa, sidhani Dar inakosekana kwenye orodha hiyo, shidda ya usafiri tuliyokutana nayo Mbezi katika kupanda daladala ni kichocheo kingine cha maambukizi ya ugonjwa huo. Mwenzetu Makala anatumia gari la serikali, hapati machungu wanayopata wananchi wa kipato duni, akina mama na watoto na mizigo. Shida na adha iliyopo ni kubwa, tunaililia serikali kutazama upya maamuzi hayo kandamizi.
- Kama sababu kubwa ni kuongeza mapato kwa serikali kupitia hizo biashara alizotaja RC, basi ni bora mara 100 abiria wanaotoka mikoani wakatozwa hiyo nauli ya shilingi 400 kwenye mabasi makubwa ili kupunguza msongamano wa abiria kwenye daladala na hata stand hizo mbili ili kuwanusuru dhidi ya maambukizi mapya yanayoendelea.
- RC na timu yake wafanya utafiti wa namna bora ya kuongeza mapato waliyokusudia badala ya huo mpango waliouanzisha, siku zote tunakwama kwenda mbele kwasababu ya kutofanya tafiti kabla kutoa maamuzi sahihi.
- Yapo madhara mengi sana yanatokana na maamuzi ya RC, ila wananchi tumekosa mshikamano wa namna bora ya kuyafikisha kwa ngazi za juu zaidi ili kuwanusuru raia wasio na uwezo.
- Tegemeo la mwananchi ni kuona kiongozi anatumia ubunifu wake kutatua kero zinazowakabili katika kuondokana na umasikini, lakini alichokifanya RC ni kuongeza umasikini kwa wananchi masikini