Suala la dini litanikosesha ndoa. Naombeni ushauri

Matongee

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
253
629
Wakuu naandika huku nina stress. Huwa ni mzito wa kuongelea mambo yangu ya mapenzi ila hapa JF naona ni sehemu sahihi ya kuomba ushauri kwasababu kila mtu yupo huru kwa feki ID.

Kiufupi mimi ni kijana mdogo wa miaka 37, mkristo na mwanachama wa CCM. Baada ya kumpata msichana tuliyependana nikaona anafaa kwa ndoa. Mkoa niliopo kikazi ni mkoa wa mbali kutoka kwetu. Nilipofikia uamuzi huu nikaona niwapigie wazazi simu na kuwajulisha kwanza nia yangu hii. Baada ya maswali kadhaa wazazi wakaona iko poa tunaweza anza mchakato wa kuelekea ndoa. Ila kwa upande wa mama ndo akaja na jambo linalonifanya niombe ushauri.

Mimi kwetu wasabato wazuri kabisa ila mimi binafsi tangu nikiwa na miaka 19 nilianza kwenda tofauti na usabato. Imefikia wakati ni kama tu sina dini. Siendi kanisa lolote kwa miaka mingi. Ikitokea nimeenda ni labda msiba, harusi au ibada nyingine maalum. Kwa miaka mingi nimekuwa nikijitafuta sana kuhusu suala la imani kwasababu kwenye SDA siwezi kabisa. Siku za karibuni nimegundua moyo wangu upo kwenye misa ya kwanza ya Roman Catholic. Yaani najiona nikiwa imara kiroho na familia yangu tarajiwa ndani ya RC.

Huyu mchumba wangu ni KKKT ila mama yangu kasema hataki ndoa ya dhehebu lingine zaidi ya SDA (Sabato). Na hata nikilazimisha yeye hatakaa aifurahie. Kimsingi inaonekana baraka zake itakuwa ngumu kuzipata nikifunga ndoa kwenye dhehebu lingine. Hadi sasa sijafikia muafaka na mama.

Nishaurini wakuu.
 
Lakini mbona mvurugano ni mkubwa sana?

Mama anataka ndoa ufunge SDA mchumba yeye KKKT wewe mwenye jukumu lako Catholic aisee chief set kwanza haya mambo vizuri,kama baba yupo mueleze ukweli yeye ndiye mwepesi zaidi kuelewa ataenda kumuelewesha mkewe.

Miaka 37 hujaoa mzee hawezi kutetea hayo mambo ya imani yeye atakuharakisha umalize haraka uanze familia
 
Baba hana tatizo lolote hata nikitaka kufunga kimila.
 
Mpumbavu, umri mkubwa akili ndogo, Achana na dini, dini ni upuuzi, ukimpenda mtu tumia akili na nguvu kumchukua, usisikilize maneno ya watu, hata mzazi/wazaz kuna muda inatakiwa kuwapuuza maana hayo ni maisha yako si yao, ukicheza vibaya utaharibu maisha yako na wao watabaki kusheherekea kushindwa kwako wakikualumu kuwa walikwambia.

Basi tu mambo ya ndoa mnayapaga ugumu usio na tija, litie mimba litoto la watu, hao wanaomng'ang'ania watakueletea bila kudai hela wala imani yako.

Ushauri: achana na maneno ya watu fanya lililo akilin mwako
 
Wakuu naandika huku nina stress. Huwa ni mzito wa kuongelea mambo yangu ya mapenzi ila hapa JF naona ni sehemu sahihi ya kuomba ushauri kwasababu kila mtu yupo huru kwa feki ID.

Kiufupi mimi ni kijana mdogo wa miaka 37, mkristo na mwanachama wa CCM. Baada ya kumpata msichana tuliyependana nikaona anafaa kwa ndoa. Mkoa niliopo kikazi ni mkoa wa mbali kutoka kwetu. Nilipofikia uamuzi huu nikaona niwapigie wazazi simu na kuwajulisha kwanza nia yangu hii. Baada ya maswali kadhaa wazazi wakaona iko poa tunaweza anza mchakato wa kuelekea ndoa. Ila kwa upande wa mama ndo akaja na jambo linalonifanya niombe ushauri.

Mimi kwetu wasabato wazuri kabisa ila mimi binafsi tangu nikiwa na miaka 19 nilianza kwenda tofauti na usabato. Imefikia wakati ni kama tu sina dini. Siendi kanisa lolote kwa miaka mingi. Ikitokea nimeenda ni labda msiba, harusi au ibada nyingine maalum. Kwa miaka mingi nimekuwa nikijitafuta sana kuhusu suala la imani kwasababu kwenye SDA siwezi kabisa. Siku za karibuni nimegundua moyo wangu upo kwenye misa ya kwanza ya Roman Catholic. Yaani najiona nikiwa imara kiroho na familia yangu tarajiwa ndani ya RC.

Huyu mchumba wangu ni KKKT ila mama yangu kasema hataki ndoa ya dhehebu lingine zaidi ya SDA (Sabato). Na hata nikilazimisha yeye hatakaa aifurahie. Kimsingi inaonekana baraka zake itakuwa ngumu kuzipata nikifunga ndoa kwenye dhehebu lingine. Hadi sasa sijafikia muafaka na mama.

Nishaurini wakuu.
Wewe na mchumba'ko rudini kwenye uasilia wenu, Uislam.

Simpo.
 
Mpumbavu, umri mkubwa akili ndogo, Achana na dini, dini ni upuuzi, ukimpenda mtu tumia akili na nguvu kumchukua, usisikilize maneno ya watu, hata mzazi/wazaz kuna muda inatakiwa kuwapuuza maana hayo ni maisha yako si yao, ukicheza vibaya utaharibu maisha yako na wao watabaki kusheherekea kushindwa kwako wakikualumu kuwa walikwambia.

Basi tu mambo ya ndoa mnayapaga ugumu usio na tija, litie mimba litoto la watu, hao wanaomng'ang'ania watakueletea bila kudai hela wala imani yako.

Ushauri: achana na maneno ya watu fanya lililo akilin mwako
Una ushauri mzuri sana ila umeandika kama teja.
 
Kuna wazazi wengine hawataki kuwaachilia watoto hasa wakiume , hupenda wawe chini yao hata kama ni mkubwa na awe na kipato basi ni shida na hiyo SDA utakuwa jita or kurya na ndiyo zao, 37yrs bado unapangiwa daa wazazi wengine jamani!
 
Wakuu naandika huku nina stress. Huwa ni mzito wa kuongelea mambo yangu ya mapenzi ila hapa JF naona ni sehemu sahihi ya kuomba ushauri kwasababu kila mtu yupo huru kwa feki ID.

Kiufupi mimi ni kijana mdogo wa miaka 37, mkristo na mwanachama wa CCM. Baada ya kumpata msichana tuliyependana nikaona anafaa kwa ndoa. Mkoa niliopo kikazi ni mkoa wa mbali kutoka kwetu. Nilipofikia uamuzi huu nikaona niwapigie wazazi simu na kuwajulisha kwanza nia yangu hii. Baada ya maswali kadhaa wazazi wakaona iko poa tunaweza anza mchakato wa kuelekea ndoa. Ila kwa upande wa mama ndo akaja na jambo linalonifanya niombe ushauri.

Mimi kwetu wasabato wazuri kabisa ila mimi binafsi tangu nikiwa na miaka 19 nilianza kwenda tofauti na usabato. Imefikia wakati ni kama tu sina dini. Siendi kanisa lolote kwa miaka mingi. Ikitokea nimeenda ni labda msiba, harusi au ibada nyingine maalum. Kwa miaka mingi nimekuwa nikijitafuta sana kuhusu suala la imani kwasababu kwenye SDA siwezi kabisa. Siku za karibuni nimegundua moyo wangu upo kwenye misa ya kwanza ya Roman Catholic. Yaani najiona nikiwa imara kiroho na familia yangu tarajiwa ndani ya RC.

Huyu mchumba wangu ni KKKT ila mama yangu kasema hataki ndoa ya dhehebu lingine zaidi ya SDA (Sabato). Na hata nikilazimisha yeye hatakaa aifurahie. Kimsingi inaonekana baraka zake itakuwa ngumu kuzipata nikifunga ndoa kwenye dhehebu lingine. Hadi sasa sijafikia muafaka na mama.

Nishaurini wakuu.
Kijana mdogo?Wa miaka 37("salasini na sabaaaa").Mwana CCM?Hahahahaaa!Dah!Siongezi neno wala kushauri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom