SUA ni Chuo au kituo cha ufisadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SUA ni Chuo au kituo cha ufisadi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MchunguZI, Jan 12, 2009.

 1. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2009
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Wana JF, Katika kuhangaikia wanetu wanaorudishwa vyuo Vikuu kwa taratibu ngumu, nilimpa kampani kijana wangu kuelekea SUA. Nimefika kwa mara ya kwanza na kujionea ambayo yamekuwa yakiandikwa magazetini.

  SUA imekaa kama Sekondari ya kata iliyopata mfadhiri. Ikiashiria uhaba wa kifedha. La kushangaza ni aina ya magari yaliyojipanga mbele ya jengo la utawala. Kuna la mkuu wa Chuo, Msaidizi 1 na Msaidizi 2. Yote matatu hakuna la bei chini ya milioni 100! Hizi ni ada za wanetu.

  Kibaya zaidi wanafunzi
  Hawana hosteli,
  Hawana internet,
  Hawana madarasa ya chuo kikuu,
  Hawana viti madarasani vya chuo kikuu
  Hawana mabarabara,
  Maabara pia hakuna!
  Nasikia usiku ni kama kijiji maana hawana taa za nje,

  Je, Ni kweli serikali inakubali kuwa na viongozi kama hawa ambao wanakusanya ada sawa na vyuo vingine, lakini matumizi yao ni ya binafsi tu? Au tusubiri baada ya muda wao ndo tuwapeleke mahakamani kwamba ni mafisadi kama Mramba?

  Lazima hawa walipewa uongozi kwa kufahamiana na kiongozi fulani.

  Mulioko SUA tuambieni Hao viongozi muliwapataje?
   
 2. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Madarasa ya chuo kikuu yakoje? Viti vya chuo kikuu vinatakiwa viweje?
   
 3. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kazi ipo, Chuo kiwe kama sekondari ya kata. Sidhani kama kutakuwa hakuna madarasa ama maabara, labda madarasa hayatoshi na maabara ni chache. Hata UDSM ukienda utakuta kuna wanafunzi wanasikiliza mihadhara tokea nje hasa katika "Seminar rooms".
   
 4. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2009
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Watetezi msiniuwe!
  Nadhani nilikosea kusema Chuo kikuu. Nilimaanisha 'University' Bado huoni madarasa yakoje, viti vikoje?

  Madarasa ya Msingi na Secondari vipimo vyake na mahitaji yako pale Kwa wakurugenzi wa Msingi na Sekondari. Sikuwahi kuona aina hiyo ya madarasa na viti vyake nilipofika University. Sasa nimeona SUA.

  Jamani hebu niambieni ni University gani nchini, ya umma au Serikali isiyokuwa na internet kwa wanafunzi? Hata baadhi ya sec. school sasa zina mawasiliano hayo. Iweje SUA haina na huku wazazi tukidaiwa ada sawa na vyuo vingine?

  Nasema tena, aliyeko SUA tuambie ni viongozi gani mulionao?
   
 5. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwahiyo unaamini gari la mkuu wa chuo limenunuliwa kwa hela ya ada ambayo serikali/ mzazi amelipa? Na hao watatu ulioulizia uhalali wa magari yao wote wana umuhimu wa kuwepo sasa sijaona uhalali wa ufisadi unaodai. Mkuu wa chuo ana msaidizi wa masuala ya elimu na mwingine msaidizi wa masuala ya utawala.

  Muulize huyo kijana wako chuo kina hostel ngapi? Maana kama ni hapo main campus nauhakika kuna hostel si chini ya kumi na mbili, kule solomon mahlangu kuna units sita (ambazo kila moja ina majengo 4) na mabeni mengine ya kulala kwamfano Tabora nk. Bado kuna hostels chuo kimetafuta nje ya eneo la chuo kwa ajili ya wanafunzi kwamfano pale mjini nyuma ya benk ya NMB ukijumlisha magorofa ma 2 au 3 (sikumbuki vizuri) yanayojengwa kwenye eneo la chuo kabla hujaingia ndani ya main campus. Ukisema kuna uhaba wa mabweni sawa lakini ukisema hawana mabweni ni exaggeration kubwa. Sasa ungesoma UD ambako watu wanauziana ubavu si ndo ungedata?

  Huyo mwanao muulize vizuri tena akuambie ukweli, computer labs zipo labda useme hazitoshi, mi nimeshawahi kufanya field practicals kwenye labs zao.

  Kweli wanahitaji kuongeza ubora wa theatre zao

  Maabara hakuna kwenye facaulty gani? Maana kwa masomo ya sua bila maabara sidhani kama shule itaenda. Karibu kila idara ina maabara labda useme hazitoshelezi idadi ya wanafunzi waliopo.

  Ungesema eneo gani la chuo halina mwanga mda wa usiku, maana kuna camopus nyingi. Nakwasababu unasikia ungekaa kusubili uone mwenyewe.

  Labda ungesema ni maamuzi gani ni ya binafsi maana zaidi ya kuonyesha kwamba wana magari ya bei ya juu hujatuambia ni maamuzi gani wanafanya ya kibinafsi.

  Sijui umetumia kigezo gani kufanya conclusion yako hii, lkn kwa kukusaidia tu hizo nafasi tatu ulizozitaja hapo juu ni presidential appointment (wanachaguliwa na raisi). Utaratibu ni kwamba kazi zinatanganzwa watu wanaapply halafu wale watatu bora wanapelekwa kwa raisi kwaajili ya mmoja kuchaguliwa (hivi ndio ninavyojua mimi inawezekana nimekosea)

  Tutakuwa hatuitendei haki nchi yetu kama tutakuwa tunalaumu tu kila kitu bila hata yakuonyesha sababu. Sekta zetu kibao zinamapungufu lakini hatutasaidia kama tukiwa tunalalamika ufisadi hata sehemu isiyohusika badala ya kuweka bayana mapungufu haya yanahitaji marekebisho haya.
   
 6. K

  Koba JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...naamini aliyepost hii topic ana valid point,ila njoo na hard numbers ili kusupport ulichoandika...mfano inawezekana wana internet lakini kumbe ni kama zile za dial up na zipo ofisi ya mkuu wa chuo tuu na walimu,hebu njoo na details kidogo ili tukuelewe!
   
 7. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hi Mndundu

  Naungana na wewe asilimia 200% nimeshafanya consultancy ndogo pale miaka minne iliyopita madai ya mungwana hapo juu si sahihi. Kwanza SUA ni chuo cha sayansi hivyo suala la maabala silakuliza. Pili nina jamaa zangu wamesoma e -commerce hapo sasa kama hakuna internate e-business utasomaje? kibaya zaidi wale jamaa wamesoma mpaka website design na wanadesign website vizuli sana. Huwezi kumaster website design kama hakuna internate. Nadhani kama ulivyosema mkuu alitakiwa kugusia suala la maboresho ambalo almost ni kalibu vyuo vyote Tanzania havina ubora kama vyuo vya wenzetu katika nchi zilizo endelea.
   
 8. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu nakubaliana na wewe hapa kwa 100%.
   
 9. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Ninafikiri kuna hoja ya msingi hapa. Solomon Mahlangu inayozungumziwa ilikuwa ni kambi ya wakimbizi kutoka South Africa. It was not meant for a university. I have been there na kimsingi ni kama sekondari. You cannot tell if you are in a university compound already. Off-campuses are even more worse. Kwa sababu chuo kinatafuta nyumba uswahilini kwa ajili ya wanafunzi waliokosa "accommodation" on-campus. Na sijui kama wanapewa usafiri kutoka off-campus kwenda madarasani, lab. e.t.c. Katika mazingira ya namna hii, ni dhahiri elimu inapoteza ubora wake kwa kiasi fulani.

  Well, utakapotembelea SUA ndipo utakapofahamu kuwa "we are not serious". Taasisi kama SUA ilipaswa kuwa ndio chachu ya maendeleo kwa nchi yetu. Lakini mambo sivyo yalivyo. SUA ni kama imetelekezwa. Na huwezi kujua vipaumbele vya serikali vinapangwa namna gani & if at all they believe in research and innovations. The government should invest heavily on education (including higher education). They should turn our higher learning institutions into knowledge base/think tanks and the source of skilled labor. Mediocre graduates will do nothing significant to our country. Things should not be let to continue as they are now.

  Thanks.
   
 10. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Hali ya SUA ilishaanza kuwa mbaya siku nyingi. Na hii ilisababishwa kuongezwa idadi ya wanafunzi bila kuongeza au ku-improve facilities. Kwa mfano Bsc. Agric General ambayo ilikuwa inachukua wanfunzi 120 in 1990 iliongeza kufikia wanafunzi about 400 by 1994 bila kuimprove any facility. Vet, Food Sc. number za wanfunzi zili-double bila kuongeza maabara wala lecture halls. Kwenye maabara wanfuzi walikuwa wanabanana.

  Hiyo Solomon Mahlangu, ni kweli kabisa haikujengwa katika standards zilizokuwepo pale SUA enzi hizo. Wanafunzi walikuwa wanalala mpaka sita kwenye chumba na maisha yalikuwa kama kwenye mahanga ya JKT. Believe me or not but that was the fact by then unless there is an improvement now. Mwanafunzi wa Solomon Mahlangu alikuwa ni second citizen pale chuoni as compared to that of main campus.

  Kwa hali niliyoiacha enzi za mid to late 1990s sitoshangaa kusikia kuwa hali imekuwa mbaya zaidi. Nafikiri Ushirombo anaweza kuthibitisha hali ya sasa ya SUA.
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Zero

  Chuo kilianza haribika mara baada ya uongozi wa juu kuamua kuwa wanasiasa Prof Msolla akiwa DVC anahusika na hili. Chuo kilipoteza uelekeo na dira, idadi ya wanafunzi ikawa inaongezeka bila kuongeza vitendea kazi, waalimu wengi waaandamizi wakaanza kuwa demolarized, ukaingia ukabila, na ukanda...na ufisadi ukashika hatamu. Ndo maana hata ubora wa graduates wa pale umepungua maradufu...Linganisha wanafunzi wa late 80s, 90s na hawa wa dotcom, 2000s inajualikana kuna wanafunzi huwa wa div 0 stil huwa wanapata udahili pale. Kuna wengine wamesoma HGL lakini wanafanya BSc Agr ama Food Sc, sababu baba zao wamewaleta kwa vimemo.

  All in all serikali nayo inachangia kiasi kikubwa kushusha ubora, sasa hivi kasma inayoenda vyuo vikuu inategemea sana na recruitment ya wanafunzi, ili vyuo vipate hiyo ni kuweka idadi kubwa ya wanafunzi ili wapate kasma kubwa ya serikali maana hutoa kwa kichwa cha mwanafunzi. Hii ni evident kwa vyuo vyote vya umma. I am sorry kwa watoto wetu sisi maskini tusioweza kuwapeleka vyuo binafsi na vyuo vya nje, watapata elimu duni washindwe kirahisi kwenye soko la ajira.

  Ushi wa Rombo
   
 12. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakuu Marshall na Mndundu naomba na mimi kuongeza 100% nyingine juu ya hili nakubaliana nalo kabisa
   
 13. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2009
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Kweli nimepata chalenji. Kwa kuulizwa maswali mengi imenibidi nitafute mawasiliano na walio na ufahamu wa SUA kuliko mimi. Nimekusanya habari za kutosha kuhusu maelezo yangu ya mwanzo. Huenda mengine nisiweze kuyaeleza kwa undani lakini nimeweza kuielewa SUA.

  UFISADI
  Niliyoambiwa ni kwamba bajeti inayotolewa na serikali huwa ni sehemu (fraction) ya bajeti nzima ya chuo. Sehemu nyingine ya bajeti inatakiwa ipatikane toka ktk ada za wanafunzi. Hili halipingiki na ndiyo maana sasa hivi vyuo vinashindana kuingiza wanafunzi weengi bila kujali uwezo wa vyuo. wanafunzi ni njia ya kupata kipato kikubwa.

  Katika vikao vya ugawaji wa pesa za bajeti, ni chuo kinachohusika na siyo wizara ya fedha au ya Elimu. Kwa mwaka huu wa bajeti, kilichotokea ni kwamba, makubaliano ya ndani ya bajeti hayakusema lolote juu ya ununuzi wa magari chuoni. Kulikuwa na upungufu mkubwa wa pesa za bajeti. Lakini ghafla magari yalinunuliwa kwa ajili ya watawala. Kama nilivyosema kila gari ni zaidi ya milioni 100. Je, mimi kama mzazi ninapofika ktk chuo kama hicho na kukuta magari kama hayo ambayo chuo kiliona ni priority, wakati huo huo kijana wangu akiniambia hawana internet ya kueleweka, nisifu utawala.

  Kwa ufupi pia nimeambiwa suala la kununua magari kumbe lilileta mgogoro mkubwa kati ya utawala na chama cha waalimu chuoni hapo. Mambo mengine hayana uthibitisho lakini pia nasikia manunuzi hayo ilikuwa ni ya lazima kama ndege ya Rais kwa sababu kulikuwa na 10% kwa wakuu wa chuo.
  Hapo utasema ada ninayolipa haikutumika? Ni kwa nini magari matatu yanunuliwe bila kujali hali ya taaluma. Kwa nini yanunuliwe wakati watawala walikiri kwamba wana bajeti ndogo sana kwa mwaka huu. Kweli chuo hakikuwa na magari ya kuwapa au ni urimbukeni?

  Ktk maelezo ya baadhi ya wana JF wanaieleza hali ya Chuo na kampasi zake. Nilichothibitishiwa ni kwamba, Mazimbu hakuna interneti hadi leo hii tunapojadiliana na bahati mbaya hiyo mazimbu ndiyo yenye wanafunzi wengi kuliko sehemu ya uatawala.

  Sasa achana na internet labda kwa wengine hawaioni ni tatizo. Chuo hakina vitabu vya kueleweka. library ipo kama jengo bila vitabu. Ni chuo kisichokuwa na bookshop.

  Kwa siku moja ya kuuliza wenyeji, nimepewa maelezo yanayotia aibu. Nimekaribishwa nikajionee aina ya madarasa ambayo hivi karibuni yalifanyiwa matengenezo. Nasikia ni uozo mtupu na inaaminika zimetumika milioni zaidi ya 600. Hapo sasa sisemi mengi maana nimeambiwa kuna mtu ni untouchable yeye akisha amua hakuna wa kubisha katika utawala. nitauliza jina niwape lakini ni mtu wa planning ambaye ni master of everything. tangu kupanga bajeti hadi kusimamia majengo. Huyu kiumbe ndo anaweka chuo ktk hali ngumu. Kila aliyejuu anawekewa kitu ktk akaunti na ni kimya. Hapa pia nimeahidiwa kupewa akaunti mbali mbali na kiasi alichoweka yeye pesa ili kuwalainisha.

  UKABILA
  Kwa wale munaotetea SUA labda mulisoma hapo zamani lakini habari za leo ni kwamba mbali na mambo ya Msolla na ufisadi wake, sasa hivi kuna mama mmoja ametajwa kwa jina la Perecy(?) sikulipata vizuri lakini ni Mkuu msaidizi utawala na fedha. Yeye sasa hivi anatajwa kuongoza kwa ukabila. Nasikia kikubwa anachotaka kusikia ni wewe ni Msukuma basi. Kwa wachaga nasikia ana uadui nanyi maana katokea vet. Muliosoma vet semeni. Mama huyu sisemi yote niliyoambiwa maana hayahusiki na hili la SUA lakini kimekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya chuo. Mbali na kijana wangu huyu ambaye labda hamfahamu vizuri, kwa aliye na mwanafunzi au rafiki mfanyakazi, aulize ni mtu wa aina gani. Tatizo lake kubwa pia nimeambiwa ni tamaa ya vijisenti.

  Naomba tusiitete SUA kwa kusema eti hata UDSM iko hivyo. Ulinganifu haufanyi SUA kuwa safi.

  HOSTEL
  Hili la Hosteli jamani tusiseme. Kama UDSM wanabebana sawa lakini hizo Hostel wanazobebana zilijengwa kama hosteli za University. Nimeuliza kimoja kimoja. Nilipouliza Hostel za Mazimbu nimeambiwa njoo ujionee mwenyewe. Nimeambiwa ni vioski vya aina yake na kama mmoja wetu alivyosema. Zilikuwa ni kambi za wakimbizi na hakuna nyongeza yoyote iliyofanyika.

  Mmenipa homework. Nimeifanya nusu kwa simu nikaishiwa credit. Nitatatafuta mengine. Ukiwa na rafiki yaonekana mambo mengi yako hadarani sana. kila mtu anakupa kwa uhakika.
   
 14. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #14
  Jan 14, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  msola alikuwa VC hapo kumbukeni!!!
   
 15. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #15
  Jan 14, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wakuu,

  Hivi hayo matatizo au mapungufu yaliyobandikwa na MchunguZI ni kwa SUA pekee? Mimi nadhani hiyo hali ni kwa "Vyuo-Vikuu" vyote hapa Tanzania. Kuanzia Main Campus (UDSM), nenda Muchs, nenda UDOM nakadhalika nakadhalika:

  - Walimu
  - Lecture threatre
  - Mabweni
  - Canteen/Cafeteria
  - Usafi wa Mazingira na upatikanaji wa MAJI SALAMA
  - Huduma za matibabu
  - Library
  - Bookshops
  - Internet facilities
  - e.t.c
  Vyote ni MATATIZO matupu.

  Sina uhakika kama ni swala la Ma-VC au viongozi wnegineo ndani ya vyuo, nadhani tatizo lipo kwenye SERA ya ELIMU YA JUU (if it does exist) and UTEKELEZAJI WA HIYO SERA.

  Kama VC anaendesha gari ya 100m, si kwa MAAMUZI YAKE binafsi, hapana, ni NDIVYO ILIVYOHANISHWA (probably na Board of Directors au Wizara MAMA au SERIKALI for that matter).

  Mwenye MAANDIKO kuhusu ELIMU ya Juu naomba atupatie hapa JF tuyapitie na I surely believe you will see where the weakness lies!!!

  Have a nice day
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Jan 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Baadhi ya matatizo anayoyazungumzoa Mchunguzi ni kweli yapo lakini yanaweza kuwa hayapo kwa level ambayo aliionyesha katika post zake. Nilichokigundua ni kuwa Mchunguzi alifanya (visual) observation ya haraka haraka na kuuliza maswali mawili matatu kwa aliokuwa nao karibu na ndio maana kati ya vitu alivyovinotice awali ni magari (ambayo aliyaona).
  nakushauri ukipata muda, rudi tena SUA, uombe uonyeshwe vifaa ambavyo chuo hicho vinakitumia katika masomo na tafiti. Nakuhakikishia mathani kuwa hautakuja tena na hoja kuhusu maabara kwa mtindo ambao umekuja nayo.
  Ni kweli kuwa SUA kuna matatizo (kama yalivyo katika taasisi nyingi hapa nchini) lakini hii ni moja ya tasisi ambazo ziko ahueni katika yale inayoyafanya.
  tatizo kubwa linalokikabili chuo hich ni kutotumika ipasavyo wka matokeo ya tafiti zake na kutothaminiwa kwa wtaalamu wake na wanasiasa.
  SUA imeshakamiliasha tafiti nyingi sana katika kilimo cha kisasa na iwapo serikali ingekuwa na utashi wa kutekeleza hata nusu ya waliyoyabaini, tungekuwa tumepiga hatua kubwa sana katika maendeleo ya kilimo
   
 17. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,028
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  Huna takwimu huna haki ya kuongea. Bazazi ametoka hapo mwaka jana Novemba ktk warsha na yote kasoro magari ni uongo. Labda kwa vile nimekaa pale muda mfupi ila fanya utafiti sio kukurupuka.
   
 18. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2009
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Nadhani ungeendelea kunipa chalenji ili nikutafutie ushahidi badala ya kutumia mambo tofauti usiyokuwa nayo ushahidi.

  Kwa imani yako taasisi nyingi hapa nchini zinapokuwa na matatizo ndo zinifanye nione haki ya SUA kuwa hivyo? Nilichokisema ni Uongozi wa kifisadi sasa kama unapingana na hayo eti tu kwa sababu ulikuwepo ktk Warsha basi ni tatizo.

  Unatetea utafiti mzuri wa SUA, kweli unaamini ni mzuri? Mbona tafiti za ilonga na ukiriguru hazijawahi kuachwa kama hizo za SUA. Au SUA inaonewa.

  Naomba usiamini kama Bazazi kwamba data ndo mwisho wa yote. Data gani au tafiti gani? Kama umepitia kwa mwalimu kama mimi lazima uwe unafahamu kwamba matokeo ya tafiti siyo ukweli bali huwa ni arguments kutokana na hizo unazoziita data, basi! Watafiti koote Duniani wana data nyingi sana lakini nyingi ni rubbish.
  Mtafiti anayejikinga kwa data akidhani ni truth, huyo ni balaa!

  Je hizo data ndo zinawafanya viongozi waonyeshe hizo sura za kikabila?

  SUA haina lolote muulize kijana wako kama unaye kama mimi. Sasa hivi hakuna hata shamba la mfano, na hayo yaliachwa tangu miaka ya 90. Hiyo nayo inahitaji nguvu ya nje ya chuo.

  Bado nitaendelea kukupa maelezo meengi ya SUA na leo nimempata mtu wa mjini Morogoro. Yeye anachojua SUA ni mashuhuri kwa kuanzisha Bar za pombe. Mashamba ya SUA sasa ni pori la vibaka. Huyu ni mtu wa mitaani. lakini rudi kwa watu wa chuoni uwaulize kama mimi. usilaani visual assessment wakati hata wewe ilikuwa hivyo eti ulipokuwepo kwenye seminar na warsha.

  Hawa watu tusiwatetee lazima watuonyeshe uwezo wa elimu yao badala ya kuwa mashuhuri kudai uongozi ambao unawaponyoka. Mulikoko Bongo kama mimi waulizeni walioko vyuoni kama kweli hao wakuu wametimiza wajibu wao kama wakuu wa vyuo ili kutatua matatizo ya wanafunzi na bodi ya mikopo. Nothing.
   
 19. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Serikali kupitia Wizara ya Elimu izimulike vyuo vya Elimu ya juu kwa kuviboresha kwa ubora wa elimu hapa nchini.Kama serikali imeridhia kupunguza matumizi basi vivyo hivyo ifanyike katika vyuo hivi ili fedha kidogo inayopatikana itimize majukumu muhimu na si anasa.
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu, labda kiswahili kinanisumbua, lakini naomba unifafanulie maana ya neno bazazi na kwa nini umeamua kuniita hivyo?
  Inaonekana unachanganya mambo kwa sababu unaniweka kana kwamba nilisema kwua nilikwenda kwenye warsha au semina, sikumbuki kulisema hilo!
   
Loading...