Stress za kuachwa

Stress za kuachwa

Anonymous

Senior Member
Joined
Apr 6, 2006
Posts
127
Reaction score
353
Nadhani mko salama kabisa.

Mimi nikiwa na stress za kuachwa au kukataliwa kwanza nafuta namba ha huyo mtu, narestore simu kabisa

Naingia chumbani kwangu, nafanya usafi, nafua, napika nakula chakula kizuri ninachopendelea.

Natoka naenda shopping huko naenda nunua kila ninachohitaji, nitanunua shuka, nguo, kila kitu hadi na ambavyo sivihitaji

Nikirudi nyumbani nafanya usafi tena mara ya pili naoga, nakaa sasa naangalia movie na series.

Hapo sasa nakuwa afadhali stress zimepungua.

Vipi kwako mdau wa JF ni kitu gani unafanya ukiwa na stress za kuachwa/ kukataliwa?
 
Ninachukua lipstick ninaandika kwenye karatasi “he wasn’t good enough for me” ninaibadika kwenye derssing table. Nikimkumbuka tu ninaisoma ile karatasi.
Sasa hapo si ndio unakuwa unajikumbushia kabisa?
 
Kama nilimpenda kweli...
1. Naliaaaaaaa
2. Naimbaaaaa
3. Natoa picha zangu za zamani naangalia napata kumbukumbu itayoondoa huzuni
4. Natoka kwenda snowcream.... Hapo ntakula flavour zote siku hiyo.
5. Narudi nyumbani naangalia movie hadi usiku wa manane na ntajikuta nimelala sebleni hadi asubuhi.
6. Maisha mapya yanaanza hata nikipishana nae wala sipati huzuni Wala chuki, naona kama njmepishana na mtu ambaye sijawahi kutana nae maishani.

Kasie Matata.
 
Hahaa mkuu kama naona jinsi ulivyokuwa unahama mkoa
Miaka Ile kambi ilikua Tanga, Kwahio naweza kwenda Mwanga, nakumbuka niliondoka Tanga saa nane mchana nikaenda Makambako Iringa miaka Ile, dah!! Sijawahi kumpiga wala kumnunia mtu.

Au sometimes natafuta hotel nzuri saaaana naenda kukaa hapo for a night or two, nilishalala De Francee Hotel Kipindi kile na mara ya mwisho ilikua Landmark Hotel ya Mbezi Wakati ni mpya, two nights Hahahahah
 
Kama nilimpenda kweli...
1. Naliaaaaaaa
2. Naimbaaaaa
3. Natoa picha zangu za zamani naangalia napata kumbukumbu itayoondoa huzuni
4. Natoka kwenda snowcream.... Hapo ntakula flavour zote siku hiyo.
5. Narudi nyumbani naangalia movie hadi usiku wa manane na ntajikuta nimelala sebleni hadi asubuhi.
6. Maisha mapya yanaanza hata nikipishana nae wala sipati huzuni Wala chuki, naona kama njmepishana na mtu ambaye sijawahi kutana nae maishani.

Kasie Matata.
Hii nimeipenda sana!
 
Miaka Ile kambi ilikua Tanga, Kwahio naweza kwenda Mwanga, nakumbuka niliondoka Tanga saa nane mchana nikaenda Makambako Iringa miaka Ile, dah!! Sijawahi kumpiga wala kumnunia mtu.

Au sometimes natafuta hotel nzuri saaaana naenda kukaa hapo for a night or two, nilishalala De Francee Hotel Kipindi kile na mara ya mwisho ilikua Landmark Hotel ya Mbezi Wakati ni mpya, two nights Hahahahah
Aisee! Na hii kitu inakuwa ni automatic wala hufundishwi!!
 
Back
Top Bottom