- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Vidonda vya tumbo hutokea pale asidi ya tumboni inapoharibu tabaka linalolinda ukuta wa tumbo na kusababisha kidonda. Dalili za kawaida ni maumivu ya kuhisi kuungua tumboni, kutopata mmeng'enyo wa mzuri wa chakula. Vidonda vinaweza kupona pale chanzo kinachosababisha hali hiyo kinapodhibitiwa. Ni muhimu mtoa huduma za afya kubaini chanzo cha kidonda ili kupendekeza matibabu sahihi.
Madai
Kumekuwa na madai ya muda mrefu kuwa stress (Msongo wa mawazo) unaweza kusababisha vidonda vya tumbo.
Uhalisia ni upi?
Ufuatiliaji umebaini kuwa stress si chanzo cha msongo wa mawazo moja kwa moja, bali inaweza kuwa ni kichocheo cha ugonjwa huo kwa wale ambao wanao huo ugonjwa tayari.
Benjamin Kimaro, Daktari Bingwa kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili anafafanua kuhusu uhusiano uliopo kati ya msongo wa mawazo na vidonda vya tumbo.
Dkt. Kimaro anaeleza kuwa uhusiano wa msongo wa mawazo au stress na vidonda vya tumbo una nadharia yake au theory ambayo ni ya kifiziolojia.
Hii inatokana na ukweli kwamba unapokuwa na msongo wa mawazo au stress, kuna kemikali ambazo zinazalishwa mbalimbali mwilini ambazo kemikali hizo huwa zinaenda kuondoa balance iliyopo katika uwiano mzima wa ulinzi wa tumbo. Inavyotokea hali hiyo ina maana hata zile prostaglandins na other chemical mediators ambazo zimejengwa kwa ajili ya kuzuia swala zima la ule ukuta wa tumbo usije ukamenyenywa, ni kwamba ukiondoa hiyo balance ina maana ni inawezekana kabisa ule ukuta ukamenyenywa na swala zima la enzymes.
Enzymes ambazo huwa zinamenya chakula, na ueleweke ule ukuta ukifikikiwa na wenyewe ni protini in nature. Kwa hiyo wale enzymes ambao ni protini in nature wanaweza wakameng'enya ule ukuta ukatengeneza vidonda mbalimbali na kama hata risk factors, changamoto zingine ambazo zinawezekana zikaingilia pale zinatokea, basi kuna uwezekano pia wa mtu kupata vidonda vya tumbo.
Haina maana kwamba kila mtu mwenye stress, msongo wa mawazo mkubwa ambao anashindwa kuumiliki anaweza akapata vidonda vya tumbo, hapana. Ila kuna uwezekano, kwa hiyo is a risk factor, ni mojawapo ya hatarishi kwamba mtu anayepitia hali hiyo kwa muda mrefu anaweza akapata hivyo vidonda vya tumbo.