Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Nianze kwa kusema, wote tunajua strategy ya ushindi wa Magufuli toka uchaguzi wa 2015 na hata uchaguzi huu wa 2020 imejikita kuhakikisha anazoa kura za kutosha kutoka kwa Wasukuma.
Natambua huko Kanda ya Ziwa kunajumusha pia mikoa ya Kagera na Mara ambako nadhani Lissu anaenda kufanya vizuri sana.
Wasiwasi wangu upo kwenye kuwashawishi Wasukuma wamuache yule anayejitanabaisha kama mwenzao. Kila akipata upenyo, Magufuli anakitwanga Kisukuma, na hafanyi hivi kwa bahati mbaya.
Magufuli anaweza kuwa hajui Kiingereza na hana exposure sana ya mambo ya kimataifa ila anayaelewa sana mambo ya makabila. Hata yale aliyoyakwaza amefanya hivyo akiwa anajua anawakwaza. Labda anaona hawahitaji.
Ushauri wangu kwa timu ya kampeni ya Lissu, kama muda bado unaruhusu, na nyie mkiwa mikoa hiyo yenye Wasukuma wengi, anzeni kutwanga lugha yao. Lissu jifunze maneno mawili matatu hata ya kuwachekesha tu, yatasaidia.
Kwenye issue za sera, waambieni hayo hayo mnayowaambia sasa ila katika lugha yao. Watawaamini zaidi. Waambieni pia kuna wanasiasa wanataka kuwatumia tu kama chambo.