Yawezekana huu ukawa ndio mwisho wa nguvu na ushawishi wa CCM Kanda ya Ziwa. Chama gani mbadala kina mikakati kutumia fursa hii?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,503
2,046
Baada ya kufariki kwa Rais Magufuli sioni ni kwa jinsi gani wakazi wa Kanda hiyo wataendelea kukiunga mkono hiki chama hasa kwa sababu kuu zipatazo tatu kama ifuatavyo.

Mosi: Uungwaji mkono kwa CCM katika Kanda ya Ziwa haukujengwa katika hoja bali ulijengwa katika ushabiki ukanda na ukabila. Ilifika mahali mtu alijisikia fahari kuwa Msukuma ama mtu mwenye asili ya Kanda ya Ziwa. Utakuta zinaalikwa ngoma toka usukumani kwenda kutumbuiza mkoani Dar ili tu kukonga moyo wa Rais. Zaidi ya hayo kisukuma kiligeuka kuwa lugha ya kawaida sana kunako majukwaa ya kisiasa na kiserikali.

Pili: Katika makabila mengi ya kifugaji ambayo ndiyo mengi kwa Tanzania ikiwemo Kanda ya iwa, hayakubaliani sana na jinsia ya kike hasa kunapohusika kuongoza. Wao humchukulia mwanamke kama kiumbe wa dalaja la pili.

Tatu: Miradi mingi iliyoelekezwa huko Kanda ya Ziwa siku za marehemu ina uwezekano mkubwa wa kutelekezwa au kutekelezwa kwa kiwango kidogo sana, hii nayo itaongeza chuki kwa watu wa Kanda ya Ziwa kuona ni kana kwamba CCM imesaliti maono ya shujaa wao.

Endapo uchaguzi ungeitishwa sasa sioni ni jinsi gani CCM ingeepuka kura za hasira toka kanda hii
 
Mimi napenda CCM ipasuke tupate chama mbadala.

Maana vilivyopo ni kama havitoshi.
Fisiemu inatakiwa ipigwe mpaka ipasuke, itulie tuli wala isikimbilie kujipasua baada ya kuona maji yamezidi unga. Hatupigi bomu mochwari
 
Safi ikijipasukia hakuna wa kubeba lawama zaidi ya wao.
Siwapendi Fisiem toka enzi na enzi, pili niliwachukia zaidi baada ya Jiwe kuwa Rais, pamoja na hayo yote lakini naiona hatari mbele kama fisiemu watapasuka, hapa nazungumzia kwa maslahi mapana ya nchi. Siwapendi lakini waendelee tu kuwa wamoja.
 
Baada ya kufariki kwa mheshmiwa rais sioni ni kwa jinsi gani wakazi wa kanda hiyo wataendelea kukiunga mkono hiki chama hasa kwa sababu kuu zipatazo tatu kama ifuatavyo.
Mosi. uungwaji mkono kwa ccm katika kanda ya ziwa haukujengwa katika hoja bali ulijengwa katika ushabiki ukanda na ukabila. Ilifika mahali mtu alijiskia fahari kua msukuma ama mtu mwenye asili ya kanda ya ziwa. Utakuta zinaalikwa ngoma toka usukumani kwenda kutumbuiza mkoani Dar ili tu kukonga moyo wa rais. Zaidi ya hayo kisukuma kiligeuka kua lugha ya kawaida sana kunako majukwaa ya kisiasa na kiserikali.
Pili. Katika makabila mengi ya kifugaji ambayo ndiyo mengi kwa Tanzania ikiwemo kanda ya ziwa, hayakubaliani sana na jinsia ya kike hasa kunapohusika kuongoza. Wao humchukulia mwanamke kama kiumbe wa dalaja la pili.
Tatu. Miradi mingi iliyoelekezwa huko kanda ya ziwa siku za marehemu ina uwezekano mkubwa wa kutelekezwa au kutekelezwa kwa kiwango kidogo sana, hii nayo itaongeza chuki kwa watu wa kanda ya ziwa kuona ni kana kwamba ccm imesaliti maono ya shujaa wao.
Endapo uchaguzi ungeitishwa sasa sioni ni jinsi gani ccm ingeepuka kura za hasira toka kanda hii
Chama kikuu kanda ya ziwa ni CHADEMA na ni wakati sasa wana ziwa kushika kadi za CDM, ccm imewaangusha tangu uhuru.
 
Mimi napenda CCM ipasuke tupate chama mbadala.

Maana vilivyopo ni kama havitoshi.
Hakuna CCM, Kuna Dola.

Hata serikali iliyopo madarakani sasa hivi iliingia kibabe.

Na mpaka sasa hakuna mpambanaji, kila mtu yuko kibra.

Kutoka madarakani au kutotoka ni hisani yake mwenyewe.
 
Mimi napenda CCM ipasuke tupate chama mbadala.

Maana vilivyopo ni kama havitoshi.

Ccm ipasuke kisha upate chama mbadala kinachotosha! Kama ccm yenyewe ikiwa moja haiwezi kushinda uchaguzi wowote wa halali, huku kikiwa na uwezo mdogo wa kujenga hoja, ni ubora upi unaoutegemea toka ndani ya huo uchafu?
 
Ccm ipasuke kisha upate chama mbadala kinachotosha! Kama ccm yenyewe ikiwa moja haiwezi kushinda uchaguzi wowote wa halali, huku kikiwa na uwezo mdogo wa kujenga hoja, ni ubora upi unaoutegemea toka ndani ya huo uchafu?
Utakuwako tu we subiri.
 
Hakuna CCM, Kuna Dola.

Hata serikali iliyopo madarakani sasa hivi iliingia kibabe.

Na mpaka sasa hakuna mpambanaji, kila mtu yuko kibra.

Kutoka madarakani au kutotoka ni hisani yake mwenyewe.
Tuwatie pressure watoke.

Nchi ni yetu hii
 
Siwapendi Fisiem toka enzi na enzi, pili niliwachukia zaidi baada ya Jiwe kuwa Rais, pamoja na hayo yote lakini naiona hatari mbele kama fisiemu watapasuka, hapa nazungumzia kwa maslahi mapana ya nchi. Siwapendi lakini waendelee tu kuwa wamoja.
Tatizo wako kimatumbo yao zaidi.

Bora wapasuke hata msukosuko ukitokea ipo siku utaishi.

Nothing stay forever
 
CCM itashindwa tu endapo vitu vitatu vitatokea
1 IGP na jeshi la police liamue kutenda haki kwa vyama vyote

2 CDF akatae dhuluma

3 Tume ya uchaguzi iundwe na watu ambao hawatokani na vyama vya siasa au kuchaguliwa na wanasiasa

Nje ya hapo CCM itaendelea kutawala japo najua watu wa kanda ya ziwa wanaweza kushift pakubwa sana ila hawana chama mbadala cha kwenda zaidi ya yote wataacha kupiga kura tu na kitendo hiki bado kitaifaisha CCM tu.
 
Back
Top Bottom