Strabag ni janga jingine

Strabag ni janga jingine

Masulupwete

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2012
Posts
2,366
Reaction score
2,438
Kwa wageni wa dsm hii ni kampuni inayotengeneza barabara ya Morogoro kwa ajili ya magari yaendayo kasi. Kwa mtazamo wangu kampuni hii imeonyesha udhaifu sana katika kufanya kazi, kiasi kuna wakati najiuliza iliwezaje kupata hii kazi jamani.

Fikiria, wamechimbachimba kwa ustadi mkubwa barabara toka kimara, ubungo, manzese hadi town center, sasa ishu ngumu ni kuijenga hiyo barabara! Wanajenga kwa mwendo wa konokono kiasi cha kuwapa shida sana watumiaji wa barabara.

Hapo Ubungo Stend ndo balaa tupu hakuna utaratibu mzuri haielewi hata gari zinapitaje,binafsi nimeshashuhudia kuna makampuni yanafanya kazi katika eneo finyu mfano unakuta barabara upande mmoja ina shimo/bonde upande mwingine kuna mlima lakini wajomba wanapiga kazi inaenda vema na magari yanapita vizuri lakini hawa jamaa wamepewa sehemu kubwa ya kufanyia kazi lakini bure kabisa!!!!
 
Ni uzoefu wa watanzania kulalamika katika kila jambo ingawa baadae litakuwa na manufaa kwa kila mmoja wetu: kuna baadhi ya mambo ya kujiuliza je ingelikuwa kwamba hii barabara ujenzi wake haujaanza mpaka leo na kubaki kama ahadi si tungelalama na kusema serikali haitekelezi kabisa ahadi na miradi iliyopo?barabara kiukweli kwa leo imekuwa tabu kupitika kwa sababu ambazo kama wewe unakaa Dar Es Salaam utakuwa umeshuhudia mwenyewe jinsi mvua zilivyokuwa zinanyesha kwa muda mrefu kwa hiyo ndugu mdau kuwa na subira kwani kila maendeleo huja na changamoto zake
 
Dasalama ya leo balaa we fikiria mi ndo nafika kumnyumba saa ivi duh!:angry::angry:
 
Ni maelekezo ya ccm kuwa wajenge polepole ili ifikapo mwaka kesho mwishoni waongeze speed kwa ajili ya 2015 kama promo kwa gambas
 
Kama STRABAG hawafai pendekeza kampuni unayoona inafaa ipewe kazi.
 
Hii kampuni ya kijeruman ni wapuuzi kabisa. kama kuna public holiday hawafanyi kazi. sunday hawafanyi kazi, tukiingia barabarani asubuhi nao wanawasha magreda yao.. hawana utaratibu wala phase za utengenezaji wanachimba chimba kila sehemu na kupaacha na kuamia pengine... wamefunga kisutu to samora 6 months now na hakuna kazi inayoendelea na barabara inapitika wameishapiga lami la zege hapo..wizara ya Dr Magufuri angazia hili janga la taifa wanakula muda wa kuzalishia taifa makazini.
 
Jamani tusiwe wepesi wa kulaumu hii kampuni iko njema sana. Kumwaga zege hadi likauke sio kazi ya siku moja wala mbili na ukumbuke kabla ya kuweka hilo zege kuna Landscaping kubwa sana imefanyika.

Nakumbuka ujenzi wa Sam Nujoma ulilalamikiwa sana huku walalamikaji wakizisifia kampuni zilizokua zinajenga Shekilango na Kilwa roads. Leo hii nenda kajionee tofauti ya roads hizo.
Nadhani tuweni nasubiri sometimes
 
Nakubaliana na maelezo na mtazamo wako. Ukijipa nafasi kutaka kujua nani anapaswa kufanya yale yanayowakwamisha na kuwasababisha kutofanya kazi katika siku na muda waliopanga utagundua siyo wao bali Mteja wao. Nimebahatika kuona kazi za hawa jamaa tofauti na hii ya Dar-Moro Rd kiukweli zimetulia na hazina walakini wala ubabaishaji. Ni wazoefu sana katika miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu. Kama hapa kwetu inakuwa au kuonekana hivyo tuangalie vizuri na tutabaini tatizo haliko kwao na wala si sehemu ya kazi yao kulitatua hilo tatizo.

Kuna habari hapa chini mpya ambayo imechukua nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari vinavyotoa taarifa za sekta ya Ujenzi Ulaya. Sidhani kama itakuwa na athari zozote kwenye utendaji wao wa huu mradi wa Tanzania?!

According to a press release of the Austrian construction firm STRABAG, its CEO, Hans Peter Haselsteiner resigned yesterday.
The CEO of STRABAG, Dr. Hans Peter Haselsteiner, tendered his resignation from the management board of the publicly listed construction company effective with the end of the 2013 Annual General Meeting. It is his intention to continue to support the management board as an authorised representative in matters concerning the group's internationalisation and strategic orientation. After discussion, the supervisory board accepted the resignation of Hans Peter Haselsteiner effective with the end of the Annual General Meeting on 14 June 2013. Dr. Thomas Birtel, Deputy CEO, was appointed as new CEO by the supervisory board at the same meeting. Dr. Alfred Gusenbauer, chairman of the STRABAG SE supervisory board: "On behalf of all employees and the supervisory board, I am grateful that Hans Peter Haselsteiner will remain with the company in another function. We believe that Thomas Birtel, who has been with the group for nearly twenty years, is perfectly prepared to continue to successfully shape STRABAG's future." STRABAG SE will hold its financial press conference on 30 April 2013 at 10:00 a.m. at the group headquarters in Vienna. Source: STRABAG
 
Kama STRABAG hawafai pendekeza kampuni unayoona inafaa ipewe kazi.

sijaona sehemu yoyote aliyosema hawa jama ha hawafai..amehoji utendaji kazi wao tu,ili wajirekebishe au waongeze spidi ya ujenzi kama itawezekana.
 
Unataka waripue fasta, halafu uanze tena kulalama
 
Strabag wanafanya kazi kwa juhudi sana, tena wanajitahid japo mazinngira ya kazi ni magumu, ujenzi wa mjin tena ni kuboresha barabara kwa kuijenga upya ni mradi mkubwa na unahitaji muda, tuwavumilie tu watamaliza ndan ya muda wa mkataba wao.

Sent from my BlackBerry 9380 using JamiiForums
 
Mshazoea wachina wangekua washamaliza kisha baada ya miezi sita mnakoma kuringa
kumbuka jamaa hawajengi barabara tu.wanatengeneza pia miundombinu ya mifereji kupitisja majitaka ndani kwa ndani.bila kusahau wanaboresha line za mawasiliano.
 
Ni uzoefu wa watanzania kulalamika katika kila jambo ingawa baadae litakuwa na manufaa kwa kila mmoja wetu: kuna baadhi ya mambo ya kujiuliza je ingelikuwa kwamba hii barabara ujenzi wake haujaanza mpaka leo na kubaki kama ahadi si tungelalama na kusema serikali haitekelezi kabisa ahadi na miradi iliyopo?barabara kiukweli kwa leo imekuwa tabu kupitika kwa sababu ambazo kama wewe unakaa Dar Es Salaam utakuwa umeshuhudia mwenyewe jinsi mvua zilivyokuwa zinanyesha kwa muda mrefu kwa hiyo ndugu mdau kuwa na subira kwani kila maendeleo huja na changamoto zake

Afadhali umenisaidia kumpa jibu linalo jitosheleza.Wa Tz tupunguze kupiga domo. Mnataka walipue kazi halafu mje na hoja ya kusema CCM wameiba hela kwa kutujengea barabara mbovu? Aaagh nchi hii labda aje YESU kututawala.
 
Strabag wanafanya kazi kwa juhudi sana, tena wanajitahid japo mazinngira ya kazi ni magumu, ujenzi wa mjin tena ni kuboresha barabara kwa kuijenga upya ni mradi mkubwa na unahitaji muda, tuwavumilie tu watamaliza ndan ya muda wa mkataba wao.

Sent from my BlackBerry 9380 using JamiiForums

Mleta uzi kazoea kazi za wachina.Faster with low standard but full decorations.
 
Back
Top Bottom