Strabag ni janga jingine

Strabag ni janga jingine

Mkuu hao watu ni janga la kitaifa.

Ni jumapili hii iliyopita muda wa saa 1 kasoro jioni nikiwa natoka City Centre kuelekea Kimara kulitokea kituko ambacho kilisababisha nimpe jibu moja baya sana askari wa traffic. Ilikuwa hivi:

Nilipofika pale nje ya Kiwanda cha Kibuku, jamaa wa Strabag wakiwa na lorry lao kubwa lenye matofali ya kuziba barabara, walikuwa wamepaki katikati ya barabara na mmoja wao akashuka akawa anaelekea madereva wote tupitie upande wa kulia (Ambao ndio unaopitisha magari yatokayo Kimara kwenda Mjini). Ikabidi tukubali na kuanza kubanana na magari yatokayo Kimara kwenye "road lane" moja.

Ghafla huku nyuma tena wale jamaa wa Strabag wakaifungua tena njia wakati huo sisi upande wakulia tumeshapigana pini, wa Kimara-Mjini hawaendi wala wa Mjini-Kimara hatuendi huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha. Akatokea Police Traffic mmoja akaanza kutukana madereva wanaotoka Mjini-Kimara na kudai wao ndiyo chanzo cha Msongamano huo.

Kwa kweli yale maneno aliyokuwa anatukanwa dereva aliyekuwa mbele yangu niliona yananihusu na mimi pia kwa kuwa tulikuwa wote zaidi ya magari 25. Ilibidi nifungue kioo ili kumuelimisha yule Polisi akawa mkali kama mbogo. Ilibidi na mimi nipandishe sauti kwa kumkosoa kikanuni na watu wengine wakaingilia kumsakama yule Polisi mpaka akasalimu amri.

Ndipo ikabidi asimamishe magari ya kutoka Kimara kwanza ili sisi wa kutoka mjini tugeuze tena kurudi nyuma mbele ya lango la kutokea UBT ili tuendelee na safari yetu kupitia njia ya kawaida pembezoni mwa kiwanda cha Kibuku. Yaani kutoka eneo la Kiwanda cha Kibuku mpaka nafika Ubungo mataa nilitumia muda usiopungua dakika 50.

Kwa kweli niliboreka sana na hiyo njia mpaka nikaapa kutoitumia tena mpaka hapo ujenzi utakapokamilika.
Kweli hili ndio Janga la TAIFA??
 
kampuni hii wanafanya kazi vizuri sana tusipende vitu vya haraka alafu havina ubora jamaa wameaminiwa na serikali ndio maana ata bara bara kuu ya tanga-kilimanjaro pia wanatengeneza
my take; tusiwe na haraka tuwaache wapige kazi.
 
Je tukisema wewe ndio umekosea tutakua tumekosea??
Nadhani watu wengi humu ndani hatuchambui vizuri nini mleta mada ameleta hapa. Hakua mtu aliyehoji uwezo wa hawa jamaa bali uzembe katika utendaji kazi upo dhahiri.

Kwa mtu yeyote mwenye uelewa wa kandarasi za barabara, atakuwa anaelewa kwamba wakati wa ujenzi utatakiwa kuchonga njia ya muda ya watumiaji wengine au at least diversion yenye maelekezo yanayoonekana kutokea mbali wakati utakapokuwa unashughulikia kipande cha barabara fulani.

Kwa hawa jamaa hata sehemu wanapochimba ni sehemu chache sana utakuta alama za tahadhari, kila sehemu wamechimba bila sababu ya msingi. KERO MPAKA BASI
 
Je tukisema wewe ndio umekosea tutakua tumekosea??
Huo ni mtazamo wako wewe. Ingekuwa vizuri kama wewe na wenzako mkajifunza kutoka kwa kandarasi anayejenga barabara ya Mwenge-Tegeta. Pamoja na kuwa moja kati ya barabara zenye madaraja mengi tena makubwa lakini wanafanya kazi kwa mfumo mzuri sana.
 
je kazi ya mwenge tegeta na kimara-kivukoni zinalingana??kwanza mwenge-tegeta ni 4 WAYS while kimara-kivukoni ni 4WAYS plus 2 CONCRETE ENFORCED BUS LANES......msiwe wepesi kulaumu
 
je kazi ya mwenge tegeta na kimara-kivukoni zinalingana??kwanza mwenge-tegeta ni 4 WAYS while kimara-kivukoni ni 4WAYS plus 2 CONCRETE ENFORCED BUS LANES......msiwe wepesi kulaumu
Kwani kanuni na taratibu za Kidaktari zinatofautiana katika kutibu mtu mwenye ugonjwa wa muda mrefu na yule wa muda mfupi?

Kinachongelewa hapa ni mapungufu katika kufuata usalama na usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara wakati wote wa ujenzi.
 
hayo yote ulioelezea hapo juu yanategemea uzito wa kazi.......tena mshukuru mnapita kwa shida otherwise hio barabara ingefungwa kabisa mzunguke mandela road......usifananishe kujenga simple 4 lanes za mwenge-tegeta na kujenga 4 lanes plus 4 complicated bus lane reinforced with concrete,special bus stops,pedestrian flyovers,complex intersections.....hata angekuja mkandarasi kutoka MARS lazima usumbufu uwepo.....u cant have ur cake and eat it.....either u eat it or u have it.....so tujenge tupate usumbufu au tusijenge tupite kwa "raha".....kwa sisi wapanda daladala tunaomba wajenge tu itatusaidia sana.
 
Kaka taratibu ndo mwendo ....ikianza kuwa na NDITA..aka..MAKUNYANZI utarudi tena jamvini na kuwakandia...upande mmoja ukibinuka kuliko mwingine hukawiii kunena

Wanapata shida kwa sababu miundo mbinu ya maji masafi, taka, umeme, simu, mkonga wa taifa, yote ipo eneo la barabara haijahamishwa kupisha ujenzi...WEZI wanahujumu vitendea kazi

Wana vifaa vya Kutosheleza, wanastahili pongezi 😛lane:
 
hayo yote ulioelezea hapo juu yanategemea uzito wa kazi.......tena mshukuru mnapita kwa shida otherwise hio barabara ingefungwa kabisa mzunguke mandela road......usifananishe kujenga simple 4 lanes za mwenge-tegeta na kujenga 4 lanes plus 4 complicated bus lane reinforced with concrete,special bus stops,pedestrian flyovers,complex intersections.....hata angekuja mkandarasi kutoka MARS lazima usumbufu uwepo.....u cant have ur cake and eat it.....either u eat it or u have it.....so tujenge tupate usumbufu au tusijenge tupite kwa "raha".....kwa sisi wapanda daladala tunaomba wajenge tu itatusaidia sana.
Sasa mimi nimesema nini na wewe unaongelea nini? Hao watu wako unaowasifia sijui kwa kazi kubwa ni heri wangefanya busara kufunga kabisa hiyo njia mpaka hapo watakapo maliza ili watumiaji wengine wa barabara wakajua moja, kuliko wanavyofanya ina maana hata madaladala ambayo wewe umesema unapanda yangeweza ku-diverge na hata abiria nao wangejua waende wapi ili kupata usafiri wa kuwapeleka wanakoelekea kwa urahisi na usalama zaidi.

Sasa kwa hali kama hiyo daladala linalazimika kukaa kwenye foleni masaa kadhaa kwa kipande kifupi tu cha umbali na likijaribu kuchepuka barabara nyingine Traffic Police wanalikamata. Wamiliki wa vyombo vya usafiri tunaumia sana mkiongezewa nauli kidogo tu makelele mengiii.
 
Back
Top Bottom