A
Anonymous
Guest
Wakuu, naomba nitoe kilio cha wananchi kuhusu hali ya barabara ya kuanzia Chelesi hadi Kisiwani (Kibedange).
Barabara hii imeharibika sana kwa sasa kiasi kwamba magari na bajaji yanapita kwa shida kubwa.
Hali hii inasababisha wananchi kushindwa kuwa huru katika shughuli zao za kila siku kutokana na usafiri kuwa mgumu. Mvua ikinyesha hali inakuwa mbaya zaidi, kwani barabara inakuwa haipitiki kabisa.
Kuna kipindi wananchi waliwahi kujitolea kuifanyia marekebisho hasa karibu na daraja, lakini kwa sasa hali imekuwa kama awali tena. Maji yanatuama, mashimo yanaongezeka siku hadi siku, na hatari kwa watumiaji wa barabara inaendelea kuongezeka.
Tunaomba mamlaka husika walione hili kwa jicho la huruma na wachukue hatua stahiki ili kurejesha hali ya barabara hii kwa maslahi ya wananchi wote Maana Mamlaka Zimetusahau.
Asanteni.