STORY: NAKUPENDA JK
MTUNZI : JK
EPISODE YA 15
★★★★★★★★★★★★★★
Wakati nikiwa na Nira nje tunamsubiri Dr.Mwinyi afanye yake, simu yangu ikaita, alikuwa Rukia, yule dada wa kule Same, wakala wa Vodacom..
"Hey! Jk, Miss you..uko Tanga?"
"Mic yu too..yaap nko Tanga Rukia, za siku?"
"Poa tu, nko njiani nakuja huko tuna tamasha hapo Mkwakwani leo"
"Ok, karibu sana,"
Nilijibu kifupi sana kisha nikakata simu ili kumalizana na hli zito la hapa kwnza..lakini nikijua fika kuwa Rukia leo ni wa kulala nae tu!!.
Hapa nilianza kuumiza kichwa ni jinsi gani nifanye ili nisiwe na Jessie usiku wa leo..
Licha ya kuwa nilikua sijui hatma ya Jessie itakuaje, lakini akili yangu ilisharuka kwa Rukia, nikitamani kumtafuna na yeye ili nimjue utamu wake..
Kunipigia simu na kunieleza kuwa anakuja kwenye tamasha Mkwakwani kwangu ilikua ni ishara tosha kabisa kuwa alitaka nipige mambo yangu..
Kichwa kinauma..nikaanza kufikiria jinsi gani Jessca atalala, wapi atalala, na itakuaje endapo sitalala nae.. Nilichokua naamini tangu nianze mapenzi ni kuwa kunapotokea kitu kipya, basi cha zamani uluchokizoea unakifanya namba mbili..na hata baada ya hili zoezi, sitakua na hamu na Jessca tena kutokana na hali yake itakavyokua..
Baada ya kutafakari kwa kina sana..nikaamua kumpigia simu tena Rukia ili kumuuliza kuwa atakuepo Tanga siku ngapi.? Yeye akanijibu kuwa leo watalala, tamasha linafanyika kesho..then keshokutwa ndio wataondoka..lakini muda mzuri zaidi wa kuonana na mimi ni leo kwani ndio atakua free..kesho atakua bize sana mpaka jioni..na keshokutwa wataondoka alfajiri kurudi Same.. Nikaitikia poa kisha nikakata simu. Sikutaka kukubali kuwa nitaikosa hii nyama ya bure kabisa..mtoto aliyekuwa mrembo zaidi ya Jessca ambaye amebeba mimba yangu!!
****
Tulikaa pale hospital tukimsubiri Dr Mwinyi kwa zaidi ya saa nzima sasa..Hakuna mtu aliyetoka wala kuingia chumba alichokuepo Dr Mwinyi..na hakukua na majibu yoyote mpaka dakika hii..Nilianza kupatwa na wasiwasi, Nira akiwa hataki kuongea chochote juu ya jambo lile, sikujua alikua anawaza nini..
Nikaanza kufikiria endapo kama Jessca amekufa pale hospital kwa kutoa mimba..ni vipi nitaweza kukabiliana na hili jambo? Niliifikiria sana 'future' yangu, nikaona nimeangamia..nimejiingiza kwenye shimo kubwa ambalo sidhani kama itakua rahisi kutoka..
Nilikaa pale na mawazo, ikapita nusu saa nyingine, hapa tumbo lilishaanza kuniuma.. Nikanyanyuka kuufuata mlango ule, Nira ambaye alikua ameinamisha kichwa wakati huu akanyanyua kichwa chake na kuniangalia..Unataka kufanya nini? Aliniuliza Nira wakati nimeshapiga hatua tatu kuuelekea mlango ule.
Nataka kwenda kugonga pale mlangoni Nilimjibu.
Acha ujinga, kaa hapa..mwanaume gani unakua na mawazo mgando kiasi hicho? Be strong acha ujinga! Nira alinikazia..Nikanywea, tena nikawa mpole sana.
Baada ya robo saa nyingine, mlango ule ulifunguliwa, Dokta Mwinyi akatoa kichwa kuchungulia..kisha baadae akaufungua wote akasimama pale nje..ni kama mtu ambaye amechanganyikiwa..mikono yake aliyovaa 'gloves' nyeupe, ilikua imetapakaa damu..Akaangalia kushoto na kulia..kisha akatupa jicho pale tulipokuwa tumekaaa..akarudi ndani na kuufunga tena mlango.
★★★★★★★★★★★★★★★★
Baada ya kukata simu ya Feisal..Nuro alimpigia simu Mndeme..ambaye siku zote huwa anamwita 'Mama watoto'.
Yes mama watoto, mambo vipi?
Mndeme, naomba sana achana na Feisal..utaniudhi..tafaadhali sana.. Nuro wala hakutaka kujibu salamu ya Mndeme.. Moja kwa moja alipanda kwenye 'point'.
Hahhahhhaaa..sijawahi kufikiria kuwa Nuro waweza kuwa mjinga kiasi hicho, unataka mimi baba wa watoto wako unione sina maana kuliko huyo mpuuzi wako?!
Mimi sijui hayo, ninachotaka usinifuatilie, niache na Feisal wangu..endelea na Vero wako plzz..usije ukasababisha tukafikia mbali..wewe ni mtu mzima jiheshimu..hivi unavyofanya ni vitu vya kitoto..kwani ni kipi hasa cha ajabu? Ilipokua zamu yako si nilikuachia mpaka tukazaa hawa watoto? Sasa nini kinakufanya ubabaike mwanaume? Au unataka mimi nisiwe na mume wangu ninayempenda wakati wewe una ndoa yako? Jiheshimu banaa Mndeme.. Nuro aliongea kwa hisia, maneno haya yalimchoma sana Mndeme.. Akakata simu na kuanza kujilaumu kwa kitendo cha kijinga alichofanya cha kumpigia simu Feisal..akajiona mwehu haswaa..
Usijali hubby, kila kitu kiko poa..wala hatakusumbua tena Nuro alimtoa uoga Feisal baada ya kumpigia simu kwa mara nyingine, ambaye alionekana wazi kuwa alihofia sana kitendo cha kupigiwa simu na Mndeme.
Ok sawa baby..nimekuelewa.. Aliitikia Feisal kwa sauti ya kinyonge sana.
Enhee..niambie, umefikia wapi ile michakato yako ya kuleta barua? Nuro aliuliza baada ya kuona Feisal ameridhika..
Naomba iwe suprise.. Ndivyo alivyojibu Feisal na kuendelea na maongezi mengine mengi kuhusu harusi yao na jinsi gani watakavyoishi. Nuro alionekana kuwa na furaha zaidi kuliko hata muoaji..Furaha hii ilisababishwa na jambo kuu moja tu, Nuro alikua anaamini kuwa sasa anaenda kuishi na mtu ampendaye..akiwa na roho safi kabisa.
★★★★★★★★★★★★★★★★
Uko wapi Jk? Mi nataka nikuone now Sikujua nilijibu vipi swali hili la Rukia..nikabaki na kigugumizi..
Daah..nina kazi kidooogo hapa home, nitakujulisha baada ya muda kidogo Niliamua kudanganya..pamoja na mawazo niliyokuwa nayo kuhusu hatma ya Jessca lakini bado nilimtamani sana Rukia..alishanivutia, na hivi anavyoendelea kupigapiga simu anazidi kuivuruga akili yangu. Baada ya kumwambia hivi alinielewa akinambia atanicheki tena baada ya dakika 30.
Mara tu baada ya kukata simu yake, Dokta Mwinyi alifungua tena mlango..safari hii akaja moja kwa moja mpaka pale tulipokaa tena kwa mwendo wa haraka..Nilimgusa Nira ambaye alikua amejiinamia..akashtuka na sote tukawa tumemkodolea macho..gloves zake zilizojaa damu bado zilikua mikononi mwake.
Vipi dokta, umefanikisha zoezi? Nilishindwa kumuacha Dokta Mwinyi aanze kuongea yeye..nilihisi anachelewa.
Hapana, kuna tatizo Ndivyo alivyonijibu Dokta Mwinyi na kunifanya nihamishie mikono yangu yote miwili kichwani.
★★★★★★★★★★★★★★★★
Don't Miss Episode O16
Maoni👉+255718274130
Kwa story zingine tamu zaidi..Follow instagram now.. 🏃🏃@jk.stories