moneytalk
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 7,701
- 16,418
G... KILIO CHA MTU MZIMA
Bonge akakamatwa na watu asiowajua, wakamfunga macho, mikono, miguu wakampiga weee afu wakamtupa kwenye shimo reeeefu Bonge akashtukaaaa kuangalia saa saa 11 asbh kumbe alikuwa anaota akainuka kumwangalia mtoto wake amelala shwari, mume hayupoo dah akachoka akawa amekaa tu kitandani anawaza na kuwazua hajui ndoto ina maana gan, akaamua kumpandia hewani Matusi hapatikani
Akampandia mfuasi wake hapatikani, akampigia his right hand man hapatikani mmmh asbh ikawa ngumu
Akaamua kujiandaa hata job hakwendaa akaenda kumcheki Matusi, kufika nyumbani mwake kufungua ni madamu kibaooo watu wamekufa kiroho mbayaaa, hapo saa 12 asbh, akasogea kuangalia akakutana na kichwa cha Matusi kimekatwa, chini kuna karatasi imeandikwa you are next
Akakimbia mpaka kurudi home saa 1 asbh, akamwelezea maza yake, maza akaanza kuingia na wasiwasi akasema ngoja nimwulize mtu, kumpandia hewan big poppa che hapatikani wala nene,
Akampandia hewan msaidizi wake akamwambia ametekwa nyara hata wao wanamtafuta ila wanahisi kafichwa mikoani mistuni, mama bonge akachokaaa, akiangalia imevakia wiki 1 kuitwa mahakamani,
Mama Bonge: hajakuachia mzigo wangu wowote kabla hajapatwa na majanga?!
Msaidizi: ndio hata sisi twashangaa hata zile evidence zote zimepotea hazipo nadhan wamezichukuaa wale waliomteka Big Poppa yani mama hapa tumechanganyikiwa hatuelewi
Mama Bonge: kwani nyie hamna maadui zenu ambao mnahisi labda wanachukiana na Big Poppa
Msaidizi: tunae, anaitwa Matusi, sasa tumeenda kumcheki
Tumekuta keshauawa na kichwa kakatwa chini kuna karatasi imeandikwa you are next tukaondoka tusijekutwa na polisi hapo
Mama bonge akakosa pozi sasa maana hajui cha kufanya hajui afanyaje yani ni sheedah akakata simu akaendelea kuonge ana Bonge wanapanga juu ya usalama wao kesi wiki ijayo usalama wao mbovu hawajui cha kufanya dah hii ngoma ngumu
Wakiww wanaendelea kuumiza kichwa Mama Bonge akamkumbuka yule baba aliekuwa anampigia simu anamwimbia ila kwa namba ya private no
Akaenda tigo na voda kuulizia hawana msaada akaenda polisi kulalamika wakamwambia hii namba mbona haipo hewan ila ilikuwa inamilikiwa na babu mmoja akamtajaaa mama bonge akamkumbuka, akauliza kama anaweza pata current no yake, polisi wakamsaidia, kuna lingine au unataka tumkamate?!
Mama bonge: ngoja kwanza nitarudi afande ngoja niongee nae kwanza alafu ntakupigia kama mwingie kazini au la mama bonge akaondoka kufika job kazi haziendi akamwibukia hewani yule babu mzee akapokea
Mama bonge: eh vepee baba za masiku?!
Babu Mzee: salama, nani mwenzangu?!
Mama bonge: me fulani bin fulan
Babu mzee akaganda kama sekunde 5 akamwuliza enhe unataka nini kwangu?!
Mama bonge: nataka tuongee, napenda nikurudishe kazini najua haukuondoka vizuri, tafadhali naomba tuongee
Babu mzee: wapi tuongee sasa?!
Mama bonge: naomba tukutane sehemu flan, leo saa 10 jioni
Babu Mzee: sina nauli mama labda unifadhili
Mama bonge: ntakurushia elfu 30 uchukue taxi hapo uje fasta sawa
Babu Mzee: sawa mama asante, simu ikakatwaaa
Babu Mzee akampandia hewani
Gigi, mama nimepigiwa simu na mama bonge anataka kuongea na mimi
Keshatuma na hela hapa naona imeingia anataka kunirudisha kazini, niende au?!
Gigi: ulienda atakumaliza, ichukue hio hela we panda boat njoo pemba fanya fasta kabla hajakuletea watu kukumaliza
Babu Mzee: sawa mama akakata simu, akawa anakusanya kila chake, aondoke,ila anatoka tu mapolisi hao
Babu mzee upo chini ya ulinzi kwa kosa la kutishia amani ya mama bonge
Babu wa watu kawekwa pingu polisi moja
Saa 8 mama bonge akatia timu polisi, kumcheki mfanya kazi wake wa zamani anamwuliza me nawewe tumekoseana nini na tumekosana wap mpaka kuniletea majambazi nyumbani kwangu
Babu Mzee: me sina jambazi niliemleta mbonaa, unanisingizia embu liambie jeshi la polisi ukweli mama acha kuniweka kwenye wakati mgumu... babu kajitetea pale na nene lakini wapi
Huko Pemba nako Gigi akawa amepata wasiwasi akamweleza Marion, kuhusu yule Babu mzee me nahisi kuna kitu kibaya kinaendelea pale
Marion akampandia hewani ofisa wake, vepee natmatuta mtu anaitwa flan flan,
Ofisa: tunae ameletwa leo anashtakiwa na mama mmoja kibopa
Marion: ana kosa gan na dhaman gan?!
Ofisa: ana koss la kutishia amani ya huyu mama na dhamana yake dau mil 5, huyu ataozea jela
Marion: nikitoa mil 5.5 unaweza mtoa?!
Ofisa: sawa hamba shida mkuu
Simu ikakatwa
Marion akatuma kijaja wake amalipia dhamana, saa 10 dhamana akapewa akaondoka kijana wa Marion na Mzee mpaka Pemba, babu mzee anashangaa kitu kama movie vile
Kufika Pemba anashangaa anapokelewa na Gigi, he mama upo huku?
Umefikaje?!
Gigi: long story usijali, ilimradi upo salama hamna neno! Wakaingia ndani kupiga story, usiku wakala, wakanywa, wakacheka, wakachezaa wakalala
Asbh kukakucha, mama bonge akaamkia polisi saa 4 asbh, kufika anaambiwa mtu wako ametoka kwa dhamana ya mil 5.5 na mtu asiejulikana katuma kijana wake akamtoaa
Sie tumepokea maana dhamana uliweka wewe sio sisi
Mama bonge akachokaaa, dah! Nani huyu mshenz anafanya hivi jamaa! Akachoka akaamua kukaa chini kabisa sakafuni, machozi yanamtoka, kichwa kinamwuuumaaa
Ukiona mtu mzima analia, ujue kuna jambooooo!
Tuonane j5 saa 4 usiku
santeeeeee