SEHEMU YA 1
A. MWANZO MGUMU
POSTA MPYA DAR ES SALAAM:
Nikaonekana nakimbia kuelekea kwenye gari, ungeniona nadhani ungenihurumia
Stilleto mkononi, pochi kwenye kwapa, natokea Kempinski naelekea Azania Front Kanisani, nilipopaki gari,
Hapo nimemtoroka mtu nimeaga naenda chooni kumbe nawahi kideti kingine (nilichagua kuto date mwanaume mmoja mpaka moyo wangu utakapotulia, sababu ya kuvurugwaaaa, nikaamua kwenda nao double double kama sio triple)
Hapo saa 2 nanusu usiku, nina appointment saa 3 kamili usiku na kaka mmoja anaitwa TAAJIRI!
Taajiri mwenyewe mzungu hatari, saa 3 juu ya alama ameshafika!
Sina hili wala lile simu nimeizima huyu wa Kempinski asinipigie, nipo buzy nakimbia kimbia mara naona gari limekuja na kunisimamia miguuni kwangu, ah nikaliangalia sioni mtu, nikalipotezea nikapita zangu nakimbia!
Nazidi kukimbia, mara gari likaanza kunifuata, roho inaniuma najisemesha leo nafwaaaa, dinner za watu nimekula, lakini machine sitoi, kwani kuna mtu kaleta mahari nyumbani labda?! Si wameninunulia wenyewe?!, wasinichoshe mimi, hapo nipo buzy najongea Azania Front
Ile nakaribia Azania Front, gari ikanipakia mbele tena, kidogo inigonge miguu!
Nahema juu juu najisemea huyu mbuzi gani tena ananigasi gasi tu, like what the hell?! Mara Akafungua kioo, kuangalia ni Edo!
EDO: We mrembo upoo! usiku huu unakimbia kimbia nini?! Au umefumaniwa?!
Money Penny: nikiwa nahema, heee Edooo upoo?! Maamboo?!, kucheka nacheka na kupaliwa juu, hehehe, cough cough! we unafanyaje huku sa hivi?!
Edo: naenda home natokea job njiani nikaona mtu kama namjua kuangalia vizuri kumbe ni wewe dadangu,
Money Penny: Yani we acha tu, huku nahema, hapa kuna mtu namuwahi hapo Moven Pick, mzima lakini huku nataka kuondoka!
Edo: mmh Moven Pick?! Unamfuata nani?! Au TAAJIRI?!
Money Penny: nikashtuka, nikajikausha moyoni lakini nikajikausha, Taajiri ndo nani? !
Edo: ivi Penny unadhani me sikufahamu? !
Money Penny: Bwana we unanichelewesha tutaongea, uje nyumbani, rafkiako amerudi likizo uje umsalimie
Edo: namba yangu hauna lakini?!
Money Penny: nitachukua kwa mdogowangu, au nisubiri hapo hapo usiondoke, natoa gari ndani fasta muda umeisha!
Nikakimbia fasta kutoa gari, kurudi edo hayupoo. Nikapotezea, Nikakimbiza mchuma wangu mpaka Moven Pick mojaaa hapo saa 3 kasoro dk 10 usiku
Nikapaki fasta, jipulizia ma perfume ya Tom Ford kama dawa ya mbu, maana sio kwa jasho lile.... ujue kuna ka mwendo toka Kempinski Hotel paka Azania Front Church, hapo jasho kweli, nikashuka fasta mpaka chooni, nikajirekebisha weeee saa 3 kamili nishapoa poa na a/c ya chooni kiroho safi, simu ikaingia ya Taajiri!
Taajiri: mrembo sikuoni huku restaurant, wapi rakini? !
Money Penny: nakuja nilikuwa wash room! Nikatoka!
Kufika kwa Taajiri kama kawaida ananishangaaa, umependeeza na masifa kibao, kama ame invest kwenye Chochote nilichovaa, stupid Man!
Nikamsikiliza pale anachanganya maneno, herufi R na L
Unajua mulembo mimi nakupenda kweri kweri yani tangu niripokuona pare Sea Criff moyo wangu urishituka sana
Money Penny: kimoyo moyo tobaaaa, Mungu na Maria, hii lugha vepee!
Waiter akaja nikaagiza fasta fasta, huku Taajiri anajielezea yupo buzy hajali cha waiter wala nini,
Mimi sasa hapo ni kucheka nataka, kununa nataka, naskiaje aibu, kulia nataka, i was like what the ****?!
Mrembo kama mimi nakuwaje na mwanaume hata kiswahili ni 0 namna hii?!
Tukaongea weee, me nakupenda na blah blah blah kibaaaao! Nataka kuwa mupenzi wako, si unajua tena maneno yao wanaume ni yale yale, hawanaga mapya!
Money Penny: nikachoka, nikamstopisha, ivi Taajiri Utaniweza au unataka kunichosha tu me nataka kwenda kulala?!
Taajiri: kwanini mulembo, mbona unanitisha! Nisikuweze kwa nini?!
Money Penny: (Nikamdanganya) Mimi mtoto wa kishua, nimezaliwa na silver spoon mdomoni (kijiko cha silver), nimeshazoea kudekezwaaa, kupendwaaa kupetiwa petiwaaa, nimekuwa spoiled miaka yote 24, kwetu nimezaliwa msichana peke yangu, kuna kitu gani labda ambacho unacho, utanishawishi mimi nikukubali?! (Basi tu namdanganya si sijampendaaa na yeye kaning'ang'ania, si unajua Watu wanasema mtu use mpenda bora ujipaishe aone hawezi aondoke, lakini huyu TAAJIRI mwenzangu naona nilikuwa na twanga maji kwenye kinu
Kumbuka hapo me nimetoka kuvurugwaaaa kwenye mahusianooooo, wanaume wote nawaona kama nyanya za sokoni, dyudyu haikuwa swala la msingi saaana kwangu maana hapo nilikuwa na pending penis kibaooo nimezikataa na kila siku zinanipigia simu, baby ooo baby aaa baby weee baby wuuuu, nyimbo kibao utadhani mimi studio!
Pia sikutaka tena mwanaume yeyote wa kunichezesha dimba mjini, niliadhimia nikajipanga na Mungu nikamuweka sawa ktk maombi kuwa sasa hamna kupenda ni kupiga tu wanaume mpaka uchungu na maumivu moyoni na rohoni mwangu yaishe,
Kumbuka hapo nina hofu, umri ushaenda nina 24, saaa ndio inagongaaaa, bado miaka 6 niwe na 30 kwaiyo ujinga ujinga wa wanaume na sikuutaka kabisaa
Taajiri: mimi nitakuletea standard ya maisha ya juu sana, hata nyumbani kwenu haujawahi ona! Hakuna utakachokosa kwangu, kuanzia mahitaji ya kila siku mpaka ya kuzidi,
Money Penny: kwa shughuli gani ambayo unaifanya mjini labda?! nikamsonya hapo hapo simkopeshi, Mxiiiiuuuuu! Usikute unapanga magogo vijijini na barabara za kwenda mikoani huko na kuibia watu alafu ukishanioa uanze kunisumbua mimi na familia yangu, kifupi unataka kunilenga mimi ili usijedorora kimaisha, pole weee na uzee wako, kwanza una umri gani maana sio kwa makunyanzi yako, ujana ule na nani uzee uje umalize kwangu?!
Tajiri: mimi sio jambazi wala madawa siuzi, me nakupenda mulembo, nina miaka 40
Money Penny: tobaaaa, babu kijana, una uhakika hauna ukimwi wewe?! Maana najua kidudu icho umekitembezaaa weee sasa unataka kuniletea gasi na shombo za kizee kwangu, nikataka kuamka niondoke akanizuia,
akaendelea kunitongoza hapo weee na kuzichanganya herufi r na L hapo ananiboa hakuna mfano!
Nikaamua kuoda tu msosi, baada ha dk 20 ukaja nikawa nakula huku namsikiliza anavyopiga debe utadhani daladala za kwenda mwenge posta!
Nikamaliza kula sijamjibu neno hata 1, nikamshukuru asante kwa msosi, naenda nyumbani si unajua bado naishi na wazazi na mwisho wangu ni saa 4 na sasa ni saa 5 usiku
Kwanza hapa sijui kama nitaruhusiwa kuingia nyumbani, na hivi mlinzi mnoko na niki lala nje ndio balaaa...
Itabidi unipe laki 1 nikampoze mlinzi pale anifungulie! Sawa?!
Taajiri: ah baby jamani, aya bwana, akaingiza mkono mfukoni anasema hilo tu, au kuna lingine?!
Money Penny: nikakinga mkono na makeup yangu ya kwa glam madam nimependezaje Sasa!
Taajiri akatoa laki 3, nyingine nitakumarizia kesho bebi,
Money Penny: nikainuka, asante mimi nakwenda!
Taajiri: ah subiri basi mbona una haraka sana
Money Penny: bwana sina muda nishachelewa, ujue nimekuheshimu sana hata kukaaa mpaka saa 5, kwaheri nikaondoka, kufika nje si nakutana na Mshefa
Mshefa ndio yule niliemkimbia Kempinski, anaingia na demu mwengine, mmh nikaamua kukimbilia chooni.
Taajiri nae akawa ananikimbilia, kuja wa nakutana na Mshefa uso kwa uso mara namwona demu wa Mshefa anakuja chooni, nikakimbilia ndani chooni kabisaa
Demu alipoingia ndani ya choo mimi nikatokaa, nikajipozisha kwenye kiooo, demu akatoka akanisalimia.
Demu: mambo
Money Penny: poa
Demu: nimependa viatu vyako
Money Penny: asante, hata mimi nimempenda vyako,
Demu: asante, nimepewa zawadi leo na boyfriend wangu,
Money Penny: kimoyo moyo na sema wabongo bwana, hata sijamwuliza ameshaanza kujielezea, nikaamua kumng'onga kwa kuzidi kumsifia; dah shem anajua kuchagua! (kumbe viatu vyenyewe vibayaaa)
Demu: akajaa mwenyewe anacheka cheka, si unajua mademu wa kibongo walivyo?! Ukiwasifia wanatanuuuukaaa mabichwa na midomo inaviiiimba
Demu: asante, mamiii,
Money Penny: i wish ningekuwa na boy friend anaejua kuchangua classical stuffs, sijui mnawapataga wapi wenzetu?!
Demu: mmh kwani wewe upo single?!
Money Penny: yah single kwa muda mrefu sana,
Demu: mmmh! Mrembo kama weee?!how?! Kwa muda gani upo single?!
Money Penny: miaka 3
Demu: duuu pole sana, inaelekea ulivurugwa ee?!
Money Penny: acha tu, huku narekebisha lipstic yangu,...Ila ningependa u nisaidie na kunipa tips za kupata mabwana classy kama wako, niwe naenda wapi?!
Demu: mmh me kama huyu, nilipataga Mikadi Beach, alikuwa na marafiki zake tena mwengine amekuja kuonana nae hapa nimewaacha wanaongea hapo nje, ni kaka mzuri hana shida
Money Penny: Ur lucky my dia, utakuwa umepata bonge la bwana
Demu: hamna bwana huyu ni bank manager nadhani analipwa vizuri ofsini kwake
Money Penny: nikajifanya simu inaita, hallo eh nipo washroom nakuja, nikampungia demu ndukiiii, kutoka nakutana uso kwa uso na Taajiri na Mshefa,
Taajiri asishangae sasa, eh Mpenzi bado upo?! Nilidhani umeondoka?!
Money Penny: bado nipo, unajua kile chakula nimekula, hakijanipenda kabisa, nimekaa sana washroom,
Mshefa: pole dada, habari yako
Money Penny: nzuri za kwako ( hapo uso mkavu kama hatujuani)
Taajiri: ah samahani Mshefa, huyu ndio shemeji yako mtarajiwa, anaitwa money penny,
Money penny huyu ni rafkiangu sana anaitwa Mshefa
Money Penny: hapo nina confidence kama nene, si nishajua Mshefa kanidanganya kumbe ana mtu! Nikamsalimia mambo Kaka, nimefurahi kukufahamu shem,
Taajiri mimi naenda sasa, nikamkumbatia na kumchum mdomoni kwa juu juu,
Tajiri Alishtuka, maana hakutegemea
Mshefa anatuangalia anatamani kulia, me na buy time hapo yule demu atoke, basi nimemaliza tu kumchum mdomoni Taajiri, Demu nae huyooo, oh Mshefa bado mpo hapa!
Mshefa: yah nilikuwa nakusubiria usije ukapotea bure na simu yako kumbe ninayo
Taajiri: ah Mshefa huyu ndio shemeji yangu sio?! Habari shemeji
Mshefa: demu huyu rafkiangu anaitwa Taajiri, wakasalimiana na demu pale, mimi nacheka kimoyo moyo! Leo nimembamba mwizi wangu shenzy type!
Nahisi nilimchanganya Taajiri na ile chum, akaamua kunitambulisha kwa Demu wa Mshefa, na huyu ni Mchumba wangu anaitwa Money Penny!
Demu: ah! Akaanza kucheka huku ananigonga mkono kwenye Bega, weee weeee, kumbe unae handsome wako bwana, hongera sana, nimekutana na mchumba wako washroom tukawa tunaongea aka...., ile hajamalizia, nikajifanya nimepokea simu, nikamfanyia demu shhh! Dk 1, huku naongea nambie boss, nikampungia Taajiri bye huyooo nikaondoka!
Kufika parking nakutana na Edo!
Money Penny: we nawe kama mchawi, tena upo hapa?!
Edo: nilikwambia nataka kuongea na wewe
Money Penny: nilienda kuchukua gari kutoka haupooo! Sasa ulitaka nifanyaje dogo?!
Edo: ushaonana na Taajiri?!
Money penny: ndio tena ngoja tusepe asije akanikuta hapa!
Edo: mmmh chukua namba yangu tutaongea
Money Penny: tukabadilishana namba pale, haya me naenda dogoo langu
Edo: ila huyu mwanaume sio mzuri kwako
Money Penny: Mwanaume yupi sio mzuri?!
Edo: Taajiri
Money Penny: na Mshefa je?!
Edo: mimi namwongelea taajiri,
Money Penny: Mshefa je?! Au kwasababu haumjui Mshefa? !
Edo: saa 5 nanusu nenda kwenu, tutaongea ukiwa serious, ila huyu mtu sio mzuri, mpotezee asije akakuumiza kama alivyokuumiza aliyepita
Money penny: ohooo! we nawe ushakuwa my guardian Angel, usiku mwema bwana ngoja niwahi home
Edo: usisahau kunicheki sawa kabla haijawa too late!
Money penny: boy bye!
Nikaondoka, kufik home saa 6 usiku, watu wote wameshalala, nikafunguliwa na mlinzi nikamwachia elfu 10 asinizoee, hela iliobaki nikatia ndani
TUONANE TAR 3 JAN 2018 SAA 7 MCHANA YA TANZANIA