Story: Mahusiano

Story: Mahusiano

Ninayo imani ya kutosha kwa Honey Money Penny . Vishawishi sijui vya 80 milioni ama 3sumCum na kadhalika havimsumbua Honey Money Penny .

Endelea kushusha utamu Money Penny .
Thubutuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!! Jina lenyewe tu linasadifu pesa pesaaaa
Hahaha nimekupenda bure honey
Basi Kuanzia Leo mimi na wewe tuwe ma honey kama Smart911 na mahondaw unasemaje

Kila sehemu unanitag
Tihtihtihtihi niache basiii dadadeki mbavu zanguuuuu mwenzio!!



Cc Smart911
 
C. MAPICHA PICHA HAYAJAWAHI KUMWACHA MTU SALAMA




Baada ya lile tukio buana la wale majingas kujamiiana wakiwa kwenye team ya watu wa 3 nikaamua kupumzisha akili yangu maana ilinasaaa


shukuru Mungu wiki hio ilikuwa wiki ya sikukuu za nanenane na sikukuu za idi zikaongozana kuanzia alhamisi mpaka j3 kwahiyo kazini ikawa jumanne


Baada ya kupata ule mkanda mzima kuwa Anita nae ndio wale wale, nikamuaga sista nasafiri kidogo we kaa na huyu Bi-Lucifer naenda kujipumzisha Arusha kazini narudi jumanne akiniulizia mdanganye mwambie nimeitwa na wazee Arusha


Sister hakunielewa ila akiwa hanielewi elewi anaona mapicha mapicha kwangu anajua lazima naenda kuwasha moto sehemu akaniambia Mungu akutangulie usijali huyu bishetani nitakaa nae tu


Kabla sijaondoka nikapita ATM nikazikuta zile Milion 80, nikachomoa mil 1 kwanza zikakubali

nikahamia ATM nyingine nikavuta mil 1 ingine

Nikahamia ATM nyingine Masaki nikavuta Mil 1 ikakubali

Nikahamia mwenge nikavuta Mil 1 ingine ikagoma, nikasema tobaaa nishakamatwa ... nikaenda kupanda bus ubungo nimebeba milion 3 pesa nyingi sana kwa mwaka 1995...nikadondoka Arusha mojaa kwenye hotel ya hadhi kubwa ...nikaomba chumba Expensive sana sana sana nikalipia...nikakaa pale siku ya kwanza alhamisi chakula naletewa chumbani naumiza kichwa nawaza naangalia DSTV labda nipate maujanja lakini wapi doh akili imeganda sikuelewa kunanini nikaanza kusali sali na wewe hapo saa 10 jioni akili imesimama kinoma mara nikapata simu ya Papaa.. sikuipokea akapiga mara ya 1... akapiga mara 2... akapiga mara 3 ya 4 ya 5 kimya siipokei akaacha


ikapita kama dk 10 nikaja kugongewa mlango kufungua hotel manager binti salama? kuna simu yako naomba uje, nikashangaa nani ananipigia tenaa, kwenda kupokea ni Papaa


Papaa: we mama unataka kuifunga akaunt yangu ya bank au mbona unachukua pesa ovyo ovyo?


Money Penny: kuna kingine?


Papaa: Arusha unafanya nini?


Money Penny: Nambwato


Papaa: doh ahahahaha, sawa naomba hela toa vizuri mimi nashangaa napigiwa simu naulizwa hizi hela unatumia kwenye nini


Money Penny: nikakata simu mxiiuuuu nikamwambia Manager sitapokea tena simu yeyote na wala sitegemei kupata mgeni msinisumbuee


kabla sijamaliza kuongea na Manager naskia makelele kuna binti anakuja anagooomba kweli kweli sijui alikuwa nani yule?

kuangalia namwona binti anakuja anamfokea mhudumu yupo very rude nikamshangaa huyu demu wa wapi alafu sasa mshamba kavaa kiajabu lakini ana command balaa!


akafika pale reception kaniona nimesimama kaja kanisogelea akanikanyaga na mibuti yake ya kishumundu, sikuondoa mguu nikamwambia kwa upole tu anti unanikanyaga


Binti: akanifokea kwenda zako nimekukanyaga wapi?


Money Penny: kwa hasira nikakasirika nikampiga ngumi ya shavu puuuuu akaanguka chini... wahudumu sasa wamegoma kuja kumsaidia manager kachanganyikiwa anajaribu kumnyanyua anakataaa asishikiliwe nikawa namsubiria sasa aje nimwongeze ya pili maana akili yangu ilishavurugwaa


Binti: we dada wa wapi unanipiga unanijua? nikamuongeza nyingine ya pua akawa anatoka damu akaanza kulia hotel manager akaja akaamulia pale yeye anadai anaita polisi mimi namwangalia tu mshamba mkubwa



Binti akalia pale akanyamazishwa mimi nimesharudi chumbani nawaza,

mara naskia hodi, kuja kufungua namwona hotel manager na yule binti



Hotel Manager: oh samahani madam hiki chumba ni cha huyu dada ulipewa kimakosa,



Money Penny: makosa hayo vepe? kwani anaitwa Money Penny kama mimi?



Hotel Manager: anaitwa Money Stars



Money Penny: kwahiyo?



Hotel Manager: aliekupokea amesema ulipotaja money akajua ndio yeye kwahiyo naomba umpishe huyu dada maana hata yeye analipiaga kwa gharama kubwa sana



Money Penny: wewe nyau na huyu mbuzi mtajua pa kumweka huyu ushuzi mimi hapa sitoki, labda kama kuna chumba kingine mkamweke huyu mavi sitoki


Hotel Manager akachoka, kweli kwa upande wao wanamakosa we unaona jina Money una assume ndio huyu kwanini haukuulizia vizuri nikafunga mlango nikarudi kulala


Baada ya dk 30 naskia hodi kufungua ni yule kichaa binti niliempa ngumi


Money Penny: nikamuangalia like what's up?


Money Stars: am sorry my dia kwa yaliyotokea pale chini but mimi sina hotel ya kwenda hotel zote tumejaribu zimejaa na sina pa kulala, plz naomba nilale hapa kwako, sikuoni kama ni mtu mbaya ndio maana nimekuja kuongea na wewe, plz my dia nitakulipa nusu gharama ya chumba... miaka yangu yote nakuja kwenye hii hotel sijawahi kukikosa hiki chumba plz naomba nisadie


Money Penny: nikamuangaliaaaaa nikamwambia kamwite manager aje na karatasi uandike ulichoandika na kitambulisho chako kiwe attached ndio nitakukubalia


akafanya kama nilivyomwelekeza, akaenda kweli akaja na Manager wake nawaangalia wanaandika hapo mara akapewa kitambulisho akaenda kutoa kopi nikaona huu msala sasa nimekuja kukaa mwenyewe naletewa masumbufu dah, kazi kweli kweli


baada ya barua na viambatanisho na kopi kutolewa akaja akanipa nusu hela ya chumba nikaweka nikamwambia upande wake huu wangu huu situmii tv na staki makelele ya mziki unaishi kwa rules zangu


Money Stars: sawa mama hamna neno akatua pochi akaenda kuoga hotel manager ananishukuru mara mia mia maana angemshitaki kibarua hanaaa.. akaondoka baba wa watu nikarudi kukaa kitandani nawaza na kuwazua wee lakini wapi hainiji kila nachopanga kinanasa, uuuwi Penny nimenaaasaaa.. mara bibie akatoka uchi anatafuta taulo kwenye sanduku lake doh


Money Penny: we mama unanikalia uchi kwani nimekwambia mimi msagaji?


Money Stars: oh sorry unajua nimezoea pekeyangu sorry mama nachukua taulo fasta


Money Penny: namwangalia namshangaa huyu demu vepee?


akavaa nguo zake pale me namwangalia tu, ila kila nikimwangalia naona anafanana na Anita kwa kila kitu, mwili, shape, sura, sikuelewa nikamwuliza

unaitwa nani?


Money Stars: Money Stars


Money Penny: namaanisha jina lako la kweli sio la usanii


Money Stars: ndio hilo hilo akatoa kitambulisho kumbe kweli doh nilichoka tumekuwa ma twin saa ngapi?


Money Penny: unaishi wapi unafanya kazi wapi?


Money Stars: naishi Arusha, London, USA Arusha... mimi ni ARUSHA sitokagi ndani ya ARUSHA... nafanya biashara zangu tu mwenyewe nilishamalizaga shule wmaka juzi nikaamua kufanya biashara nina hotel.. na hii hotel ninamiliki hisa 61... pia nina maduka ya nguo Arusha... kwanini?


Money Penny: akili ikanifunguka, mmmh! kwenu umezaliwa pekeyako?


Money Stars: hapana tulizaliwa mapacha! ila doto mwenzangu mama aliniambia alipotea aliibiwa tukiwa wachanga... kuna majambazi walikuja nyumbani wakamteka nyara doto mpaka leo hajafanikiwa kurudi


Money Penny: Uuuuwi Money Penny nikapata nguvu kuliko maelezo like hii safari ya Arusha nililetwa na Mungu mwenyewe... Yeeesu na Maaariaaa na Yooooseeefuuu uuuwiiii!


nikazidi kumwuliza maswali akaniambia


Money Stars: Baadae wazazi wake walizaa watoto 2 wakiume so wakike akabaki mwenyewe wazazi wake wanahisi doto alishakufa na wale majambazi hawakukamatwaa tena si unajua Tz yetu tena wameamua kuachilia tu


Money Penny: oh poleni sana... na wewe haujaangaika kumtafuta pacha wako?


Money Stars: nitamjuaje sasa huenda alikufa kweli


Money Penny: ok


nikamuacha anaendelea kujiandaa akamaliza akapiga simu wakamletea chakula akaja akakaa anakula, alipomaliza ananiuliza we mbona hauongei?


Money Penny: sikuja kuongea nimekwambia nimekuja kuwa alone mama


Money Stars: awkay sorry ma! akachukua simu yake akaweka headphones masikioni anasikiliza huku anaangalia dirishani,


Money Penny nikaingia kulala, asbh nikashtuka namwona Money Stars anakunywa chai kucheki saa saa 4 asbh , nikajiandaa kama kawa nikaamua kwenda restaurant kunywa chai maana bi kiwingu keshakuja


nilipomaliza chai nikaenda kukaa swimming nachezea maji Money Penny natunga sheria ya jinsi ya kumuunganisha Money stars na Anita na je nikifanya itanisaidia nini? maana wanaonekana wote hawana shukrani ila lazima nimwonyeshe Papaa mimi ni dume jike vile vile mjinga sana!


huku namwazia Aloyce, Aloyce akijua kuwa Anita ana pacha wake si atakufa moyo?! uuuwi ni sheedah hii Arusha imenipendaaa! nikaingia nikapiga maji weee akili ikanijaaa... nikarudi Restaurant nikaagiza chakula ile nasubiri namwona Money Stars anakuja hee best umekaa hapa ngoja nijiunge na wewe!


akakaa tukaongea vitu vingi nikajua kuwa Money Stars ni Kipanga kichwani kweli kweli ina maana na Anita lazima atakuwa kipanga tu alikuwa ananichezea akili!



Pia nikajua kuwa Money Stars alikuwa kwenye mahusiano na mtu lakini kavurugwaa! sasa hapo ndipo nilikuwa napataka mimi



Money Stars: are you in any relationship?



Money Penny: hapana mimi nipo single kabisaa



Money Stars: du unawezaje kukaa mwenyewe na umri huo



Money Penny: shit happened, now nipo likizo



Money Stars: hata mimi my dia wanaume watu wa ajabu sana, ila ndio hivyo hivyo nimeamua kupambana



akanielezea jinsi alikuwa kwenye mahusiano na kaka mmoja, walianza vizuri tu wakakaa kwenye mahusiano miaka 2 mwanaume akaanza kumbadilikia hakujua kwanini, kila kitu walikuwa wanafanya na wanafanya pamoja hakuna siku aliwahi kumzuilia kwenye mapenzi lakini mwanaume mwenyewe sijui ndio kipara kile hata sielewi ni nini hajisomi kipara kikiwaka moto anabadilika anamletea mapicha mapicha mara tuachane kipara kikipoa anataka turudiane



kwahiyo nikaamua nikae pembeni siwasiliani nae akawa anapiga simu wee sipokei, mpaka leo nina miezi 6 sijawasiliana nae nafanya mambo yangu



Money Penny: pole sana wajina pole, huyo shemeji anaishi Arusha



Money Stars: hapana anaishi kwenu Dar, anafanya biashara zake mwenyewe yupo vizuri nilimfundisha biashara sasa hivi anahela ameanza kunidharau nimeona niachane nae



Money Penny: oh jaman pole sana



Money Stars: na wewe what happen nimekuona wewe sio mwongeaji sana kama mimi..



Money Penny: mwanaume niliempenda alimpenda rafiki yangu zaidi



Money Stars: oh jaman pole, unajua sijawahi kumfumania ex wangu so sijui jinsi ya kukusaidia wewe pole sana

anyway ngoja nikuonyeshe ex wangu



akatoa wallet yake akaniaonyesha, Mungu waaangu weee kuangalia ile picha nikachoka mpenzi msomaji

Ile picha buana ulikuwa picha ya Aloyce! Aloyce rafiki yangu aliekuja kuniambia anamtaka Anita, nilichokaaa! sikueleewaaa kuna nini?! Aloyce kama ana mahusiano na bimdashi stars alikuwa anataka nini kwa Anita akili ikanigomaaaa



nikabaki nimeduwaa kwenye picha mbona wiki hii imekuwa ngumuu?!



Money Stars: Penny, we Penny, twin mbona umeduwaa unamjua au?



Money Penny: hapana simjui nimemfananisha labda na mtu mchumbaako handsome jaman sasa kwanini msirudiane jaman



Money Stars: hapana kwakweli ameni traumatize vya kutosha

nimeamua kubaki mwenyewe



Basi tukaongea wee hapo na nini, tukarudi chumbani kulala, nikawa namwuliza kwahiyo tangu Aloyce aondoke kwenye maisha yako haja zako za kimwili anakutimizia nani au kuna shuga daddy umempata?


Money Stars: akacheka sana akanyamaza basi mimi nikapanda kitandani nikalala, yeye akawa amekaa tu anakula mziki
lakini nikawa nawaza haya mapicha pichaaa nimekutana nayo mbona yamezidi kuwa mengi?

nikawaza je haya mapichaa yataniacha salama kweli?



TUONANE TAR 21 MARCH 2018 SAA 1 USIKU YA TZ



Money Penny kwa jinsi ulivyo laini hizo ngumi umerushaje? Si angekuchakaza dimples hizo...

Money Star ni pacha wa Anita. Money Star alikua ex wa Aloyce. Aloyce sasa hivi anamtaka Anita. Duu...

Na Subira ane atakua ex wa nani?


Cc: mahondaw
 
Honey Money Penny . Akina mahondaw na Smart911 watasubiri sana. Kimsingi, they will eventually come to borrow a leaf from us. Sio kwa maujanja haya Honey Money Penny

Endelea kuongeza sukari, moto wa episode ijayo haupimiki. Nakuamini Honey Money Penny


haaaaaaaa Smart911 ' s empire sio ya nchi hii... haina mapepe haina papara... inajiamini kupita maelezo.... as you can see you borrowed a leaf from us hili lipo uchiii kabisa halina kufichaa .. dat is just an intro

Money Penny huyo tunamnunua kabisa mbona wee subiri... huyo mtwangio na wallet kwisha habari yake
 
Uzuri Honey Money Penny ni mwelewa. Uchokozi huu wa mahondaw nitauacha upite kwa sasa. Seriously. Huko tuendako uchokozi huu ukiendelea nitajua namna ya kumweka sawa Honey Money Penny . Smart911 mkanye laazizi wako mapema. Akianza kukubadilikia usinilaumu.

Honey Money Penny usikonde moyo sweetheart, natania tu 😎 😎😎
Nibadilike?????? Thubutuuuuuuuuu labda sio kwa Smart911.. Vile nampenda huyu mwanaume wee acha tu. Kwa smart papa akasome tena awali.... Smart ninambaaaaaaaaa ledada mwenyewe ashamuelewa Kitambooo aliomba walau 3sum nani akubali sasa???
 
Back
Top Bottom