Taxi - (148)
ILIPOISHIA
“Mr. Oduya,
you are not serious, brother! Unadhani utaua wangapi?” yule kigogo wa polisi alisema huku akimtazama Mr. Oduya kwa mshangao. Kisha kikaibuka kitambo kifupi cha ukimya, kila mmoja alionekana kufikiria kwa muda na kushusha pumzi.
“Sioni namna nyingine ya kufanya ili kuepuka janga hili, kumbuka kuwa akizidi kuchimba kiundani basi hata wewe huwezi kukwepa kwenye hili, ndiyo maana nadhani kuwa yeyote atakayekaa mbele yetu anapaswa kunyamazishwa haraka!” Mr. Oduya alisema baada ya kitambo kile cha ukimya.
“Hapana, sidhani kama kuua litakuwa jambo jema, kwani hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwako kuliko hata kwangu!” yule kigogo wa polisi alishauri.
“Sasa tutafanyaje wakati naona maji yanaanza kuzidi unga?” Mr. Oduya aliuliza kwa sauti yenye mchanganyiko wa hasira na wasiwasi.
Yule kigogo wa polisi aliwaza kidogo kisha akasema, “Wacha niende, hadi nikifika ofisini kwangu nitakuwa nimeshapata jibu!” yule kigogo wa polisi alisema kisha akaangalia huku na kule ili kuhakikisha hakuna mtu aliyemwona, akashuka haraka toka ndani ya gari la Mr. Oduya na kuondoka.
Muda huohuo simu ya Mr. Oduya ikaanza kuita. Mr. Oduya aliitazama kwa makini na kuliona jina la Spoiler. Akaipokea ile simu mara moja na kuipeleka kwenye sikio lake. ”Niambie!” alisema kwa sauti tulivu huku akiilamba midomo yake iliyoanza kukauka.
“Nimekamilisha kila kitu, mzee. Casmir amekufa,” Spoiler alisema kwenye simu kwa sauti ya ushindi.
“Una uhakika?” Mr. Oduya aliuliza kwa sauti iliyoonesha kutoamini kile alichokuwa akiambiwa.
“Ninao uhakika, mzee... daktari aliyekuwa anamhudumia ndiye ameifanya kazi hiyo kwa umakini na amenihakikishia. Nimetoka kuongea naye sasa hivi kwenye simu, ameniambia kuwa Inspekta Abel amechanganyikiwa kwelikweli baada ya kuambiwa kuhusu kifo cha Casmir!” Spoiler alisema huku akiachia kicheko hafifu.
ENDELEA...
“Okay, hiyo ni habari nzuri. Sasa nataka na yule binti anayejiita mpelelezi wa kimataifa naye afuate njia hiyo hiyo. Hakikisha anapatikana kabla jua halijatua,” Mr. Oduya alisema kisha simu ikakatwa. Aliwaza kidogo na kutafuta namba ya Robert Kamau kwenye simu yake, alipoipata akapiga simu na kuiweka sikioni. Ile simu ikaita mara tatu na kupokelewa.
“Rob, upo wapi?” Mr. Oduya aliuliza pasipo hata salamu.
“Bado nipo hapa hotelini
Udzungwa Beach Resort, nipo na Tom, mkuu,” Job alijibu.
“Naona sasa kazi imekushinda! Umeamua kulala tu, hujui hiyo fedha unayolipwa inatokana na kazi gani?” Mr. Oduya aliuliza kwa hasira na kumfanya Job aduwae kidogo.
“Najua, mkuu,” Robert alijibu kwa sauti tulivu.
“
Okay, mwambie Tom ninawahitaji haraka sana hapa
Paradise Club, mkifika getini jitambulisheni kuwa ni wageni wa
PC.008.19, hakikisheni mnafika hapa ndani ya dakika tano tu, hatuna muda wa kupoteza,” Mr. Oduya aliongea na kukata simu.
* * * * *
Saa tatu asubuhi, kwenye sebule kubwa ya kifahari iliyo katika mazingira ya upweke, eneo la Kinyerezi, sebule yote ilikuwa imetulia sana na wanaume watatu walikuwa wakimwangalia Tunu kwa mshangao mkubwa. Macho yao yalikuwa yametulia yakimtazama usoni. Tunu alikuwa ameketi kwenye sofa akiwa amekunja nne na mikono yake ikiwa imepakata
laptop yake.
Japo Tunu alikuwa akiwaangalia kwa tabasamu na mwili wake ukiwa umetulia kwenye sofa, lakini moyo wake ulikuwa unakita kwa nguvu kifuani kwake na akili yake ilikuwa mbali sana. Akili yake ilikuwa nje ya zile kuta nne za ile sebule.
Hali hii ilikuwa imejitokeza baada ya wote kushuhudia mambo ya kutisha kwenye ile
memory card baada ya kupachikwa kwenye
laptop ya Tunu.
Walikuwa wamesikiliza mazungumzo ya simu kati ya Mr. Oduya na kigogo mmoja wa jeshi la polisi, waliokuwa wanapanga mikakati ya jinsi ya kumteka nyara Jaji Lutego kwa kumtumia mwanadada Lisa, na kisha kutekeleza mauaji yake. Yule kigogo wa polisi alibainisha kuwa alikwishaandaa mipango yote na alikuwa na uhakika Jaji Lutego angenasa kwenye mtego.
“
Jesus Christ!” Bob alijikuta akiropoka kwa mshangao mkubwa baada ya kuyasikia yale mazungumzo. “Una hakika kabisa zile sauti ni za Mr. Oduya na Kamishna Omalla, Mkuu wa Kamisheni ya Intelijensia wa Jeshi la Polisi? Siyo kwamba kuna watu wametumia teknolojia wakatengeneza sauti zinazofanana na zao?”
“Hiki si kitu cha kutengeneza, Bob. Hizi ni sauti zao za kweli. Niliyanasa mazungumzo yao mimi mwenyewe kwa kutumia simu yangu,” Tunu alisema huku akiachia tabasamu.
“Dah! Nimeishiwa kabisa nguvu!” Bob alisema huku akipiga mluzi mdogo, mshangao ulikuwa bado haujamtoka usoni.
Baada ya yale mazungumzo ya simu kati ya Mr. Oduya na kigogo wa jeshi la polisi, Tunu aliwawekea video iliyomwonesha Jaji Lutego akipata mateso makali na baadaye kuuawa kinyama. Katika video hiyo, Mr. Oduya alionekana katika picha ndogo akiwasiliana kwa mfumo wa
Videotelephony na watu aliowapa kazi ya kuua, waliokuwa katika eneo ambalo halikujulikana.
Mr. Oduya ambaye hakuwa katika eneo la tukio alionekana akitaka kujionea kwa macho yake jinsi jaji huyo alivyokuwa akiteswa kabla ya kifo chake. Alimsomea Jaji Lutego mashtaka yake kama aliyekuwa mahakamani akihukumu kesi, kisha akawaamuru watu wake kummaliza. Dulla na Uledi wakamwelekezea Jaji Lutego bastola zao, wakammiminia risasi nyingi mwilini na walipohakikisha amekufa wakamwekwa kwenye mfuko na kumpakia kwenye buti la gari aina ya Cadillac DeVille lenye muundo wa kizamani. Haikueleweka mwili wake waliupeleka wapi ule.
Video ile iliishia pale Mr. Oduya mwenye furaha alipotamka, “
Good bye, my dear judge. This is a die-or-survive world!”
“Na hii video, una uhakika si ya kutengeneza?” Tom aliuliza huku akizidi kushangaa.
“Ndiyo,” Tunu alisema kwa utulivu huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.
“Mimi sina mengi sana ya kutaka kujua isipokuwa hili moja tu... uliwezaje kuyarekodi matukio hayo yote pasipo kushtukiwa?” Tom aliuliza huku akimimina mvinyo aina ya
Madeira kwenye bilauri ya Tunu iliyokuwa tupu.
Tunu alimwangalia Tom kwa makini na kuachia tabasamu pana, kisha akawaelezea kisa kizima aliporudi toka Israel na kupata taarifa za mauaji ya rafiki yake Layla, waliyesoma darasa moja katika Shule ya Jangwani, alivyoumia sana kujiingiza kufanya uchunguzi baada ya kuhisi polisi hawakutaka kujishughulisha na kesi hiyo kwa kuwa aliyefanya hivyo alikuwa mtoto wa bilionea.
Alieleza alivyojipenyeza na baadaye kuajiriwa kwenye kampuni ya Mr. Oduya na baadaye kuhamishiwa makao makuu ya kampuni ya
The Splendid Group kama mkuu wa kitengo cha ‘
tehama’ kutokana na taaluma yake ya
Computer System Analysis.
Kwa kutumia
laptop yake iliyokuwa na mfumo maalumu wa udukuzi wa taarifa, Tunu aliweza kutengeneza kirusi maalumu aina ya
Trojans alichokituma kuiba taarifa za siri za kampuni hiyo baada ya kukituma kwenye kompyuta alizozichagua za kampuni hiyo kikiwa kama
keyloggers na
RAT (
Remote Administration Tools), na aliweza kupata taarifa baada ya mtu kubonyeza kwenye
keyboard yake, na bila kujua akawa amekiingiza kwenye mfumo bila kujua na kutuma taarifa zote nyeti kwenye laptop ya Tunu.
Inaendelea...
CC
the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater Bigjahman moneytalk marybaby nipo2 ram kisukari Smart911 Madame S carbamazepine Astelia culture gal Prisoner of hope Mine eyes kuku mweus Thad hearly Shunie Tumosa Mine eyes Kudo swahiba92 ludist Toyota escudo Clkey macson3 boga la kiangazi LEGE Smart911 Richard irakunda skfull popie Krizy Beat hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Mlenge Kacheda mjasiliamali Laki Si Pesa cocochanel kinusikwetu big jambo mludego Shupavu Kacheda mjasiliamali Mweweso Songa Heri esiankiki mnadhimu mkuu wa jf red apple the-sniper MR KUO dan oseko Jackal kuku mweus mtugani wa wapi huyo chiqutitta ndukulusudicho ADK aggyd BAHARI J
NB:
Litro 👩