Stori ya kusisimua - Taxi

Stori ya kusisimua - Taxi

Wakuu, kwanza niombe radhi kwa ukimya wangu, ni kwa vile sipo buheri. Nimeshauriwa kupumzika kwa siku kadhaa baada ya kupatwa na uchovu mkali uliosababisha nipoteze fahamu juzi jioni... Hata hivyo tupo pamoja...

NB: Litro

Pole. Mkuu. Afya Ni muhimu sana. Jitahidi kuheshimu maalekezo na ushauri wa madaktari. Speedy recovery.
 
Bishop unaendeleaje...pole sana ukijiskia kusoshalaizi karibu jukwaani kubadilishana mawili matatu japo taxi nayo ni nzuri sana
 
Pole sana Bishop Hiluka, Mungu akufanyie wepesi katika ugonjwa upone Haraka
Pole sana bro
Pole sana
Pole sana
Uwiiii pole sana jaman bishop
Pole sana mkuu.
Pole Sana Askofu
Pole sana mkuu, Mungu akufanyie wepesi
Pole sana mkuu
Pole sana Bushop
Pole sana Bishop
Pole sana tulipata wasiwasi
Mungu atakuponya inshallah karibu sana mkuu
Pole. Mkuu. Afya Ni muhimu sana. Jitahidi kuheshimu maalekezo na ushauri wa madaktari. Speedy recovery.
Bishop unaendeleaje...pole sana ukijiskia kusoshalaizi karibu jukwaani kubadilishana mawili matatu japo taxi nayo ni nzuri sana
Pole sana mkuu bishop
Pole sana mkuu Bishop, wishing you quick recovery!!
Thanks a lot, wapendwa... Leo najihisi buheri wa afya. Nitarudi baadaye ili niwasusie kufidia siku ambazo sikupatikana...

NB: Litro 👩
 
Taxi - (138)

ILIPOISHIA

Basi waliendelea kupimana ubavu, Tunu alikuwa anajipindua na kurusha mateke kwa haraka sana, kisha alimgeuzia mgongo Victor na kupaa juu na kujigeuza huku akiwa ametanua miguu yake na kuutanguliza mguu wake wa kulia kwa nguvu huku ukifuatiwa na mguu wa kushoto. Victor akafanya jitihada za kujikinga na shambulizi hilo huku akiwa tayari amechomoa kisu toka kwenye mguu wake na kukishika vyema mkononi.

Tunu alipotua chini akatahamaki kisu kikipita na kuuchana mguu wake wa kulia, damu ikaanza kumtoka. Tunu hakujali, akaruka hewani na kuganda ukutani huku mguu mmoja ukiwa umegota upande mmoja wa ukuta na mguu wake mwingine upande mwingine wa ukuta wa korido ile, kisha akajibetua na kuruka hewani huku akitua mbele ya Victor, na wakati huohuo akimtupia pigo moja matata la teke kifuani kwake lililomfanya apepesuke na kugugumia kwa maumivu,

Kuona hivyo, Victor akarusha kisu, lakini Tunu alikikwepa na kuruka hewani kisha akamshindilia Victor ngumi tatu mfululizo za mbavuni na kuzivunja. Victor akashika mbavu zake akiugulia huku akitema damu. Alikuwa anahisi maumivu makali sana. Hakuweza tena kuhimili kwani ngumi zile zilimfanya kuwa mdhaifu sana katika kupambana na Tunu.

Tunu aliruka tena hewani na alipotua aliachia teke mauti lililopoteza kabisa fahamu za Victor, teke jingine lilipotua Victor hakujua maumivu yake kwani tayari alikuwa amezirai.

SASA ENDELEA...

Kwa sekunde kadhaa Tunu alibaki amesimama pale akimtazama Victor huku akitweta ovyo na kijasho chepesi kilikuwa kikimtoka usoni. Japokuwa hakuwa amepata upinzani mkubwa sana kama alivyokuwa ametarajia baada ya kuwa amechomoka na ushindi rahisi katika pambano lile, lakini hakuamini kabisa kuwa Victor alikuwa peke yake eneo lile.
Hakutaka kupoteza muda, kwa harakaharaka alianza kumpekua mifukoni na maeneo mengine ya mwili lakini hakupata kitu chochote cha maana zaidi ya magazine moja ya bastola iliyojaa risasi na kifaa maalumu cha kuepeleka mawasiliano kwa wenzake.

Tunu aliichukua ile magazine ya bastola iliyojaa risasi na kisha kile kifaa maalumu cha mawasiliano alikiharibu kwa kukikanyagakanyaga kwa mguu wake pale sakafuni. Kisha alijitazama jinsi alivyokuwa amechafuka kwa damu iliyotokana na lile jeraha la kisu mguuni kwake. Aliokota kile kisu na kulichana shati la Victor, akajifunga pale kwenye jeraha ili kuzuia damu isiendelee kutoka.

Sasa alijua kuwa hakuwa na muda zaidi wa kuendelea kupoteza katika eneo lile kwa kuamini kuwa yote yaliyotokea wenzake Victor walikuwa wakiyasikia na sasa wangepatwa na wasiwasi zaidi baada ya mawasiliano kati yao na Victor kukatika ghafla. Hivyo, haraka akaanza kuitafuta bastola yake iliyokuwa imeanguka gizani.

Alitoa kurunzi yake ndogo ya kijasusi toka mfukoni na kuanza kumulika kule alikodhani ilikuwa imeangukia. Ndani ya muda mfupi akawa amefanikiwa kuipata ile bastola yake na kuirudisha tena kwenye himaya yake, akaiokota na ile bastola ya Victor na kuelekea moja kwa moja chumbani kwake ili kuchukua begi lake. Kama alivyokuwa ametarajia, mlango wa chumbani kwake ulikuwa wazi.

Tunu alisita kidogo na kuyatega vyema masikio yake kusikiliza, hakukuwa na sauti yoyote iliyomtia shaka. Akaingia taratibu huku akitamani sana kuwasha taa ya mle chumbani lakini nafsi yake ilimuonya kuwa kwa kufanya vile angeweza kuyavuta macho ya adui ambayo yangekuwa jirani na eneo lile. Akaamua kuingia hivyo hivyo huku akitembea kwa kunyata, alimulika kwa kutumia ile kurunzi yake ndogo.

Alichokiona mle ndani kilimzidishia hasira na kumfanya ahisi mapigo ya moyo wake yakisimama kwa muda na yalipoanza tena moyo ukaanza kwenda mbio isivyo kawaida.

Aligundua kuwa upekuzi wa ovyo ulikuwa umefanyika ndani ya chumba chake, kabati kubwa la ukutani lilikuwa limefunguliwa na kuachwa wazi. Nguo zake chache zilizokuwemo humo zilikuwa zimetupwatupwa ovyo sakafuni na vitu vyake vilipekuliwa na kutawanywa ovyo. Droo za ndani za lile kabati zilikuwa zimevunjwa na vitu vilivyokuwa mle ndani vilikuwa vimetawanywa ovyo kila mahali. Godoro katika kitanda chake pia lilikuwa limevurugwa na kuinuliwa.

Tunu alishuka pumzi za ndani kwa ndani huku akimeza mate ya uchungu kutowesha koo lake lililokauka kwa hasira, kisha akaelekea moja kwa moja kwenye mlango wa chumba kidogo cha maliwato na kuingia mle ndani kwa tahadhari kubwa huku akimulika kwa utulivu. Aliyapeleka macho yake kutazama juu ya dari kwenye gypsum ambako kulikuwa na mlango mdogo wa siri wa kumruhusu mtu kupanda na kuingia ndani ya paa la ile nyumba.

Alitazama kwa makini na kuachia tabasamu baada ya kuuona uzi mwembemba mweupe uliokuwa umegundishwa kwa umakini sehemu ya ule mlango wa siri. Tunu alikuwa ameutegesha ule uzi kwa umakini wa hali ya juu ili endapo mtu yeyote angeufungua ule mlango mdogo wa siri wa kuelekea kule juu basi ule uzi ungekatika.

Hali ile ilikuwa ni ishara kuwa sehemu ile ilikuwa haijafikiwa na mtu mwingine yeyote na hivyo kudhihirisha kuwa vitu vyake muhimu vilikuwa salama. Tunu akajisogeza na kupanda juu ya sinki la maji, kisha akajivuta na kuusukuma ule mlango wa siri na kupeleka mkono wake ndani, vidole vyake vikagusa begi lake dogo la safari. Akashusha pumzi za ahueni na kulivuta lile begi ili kulishusha.

Lilikuwa ni lile begi lake la safafri alilokuja nalo toka jijini Mwanza likiwa na nguo zake chache na vifaa vyake vya kazi, ikiwemo laptop yake yenye program zote muhimu kwa ajili ya kazi za kishushushu, kisu maalumu kitumiwacho na majasusi (Butterfly Knife) na vifaa vingine. Begi lilikuwa vilevile kama alivyokuwa ameliacha siku iliyotangulia siku hiyo.

Tunu aliivua ile suti yake ya bluu aliyokuwa ameivaa tangu asubuhi ya siku ile na kujisafisha kwa maji harakaharaka akijaribu kuiondoa damu miguuni kwake kisha akavaa suruali ya blue ya jeans na t-shirt nyeusi. Miguuni alivaa raba za simpo nyeusi.
Alipomaliza akatoka haraka kule bafuni na kuingia chumbani huku akiipachika bastola yake kiunoni, kisha akalifungua lile begi na kutoa begi lenye laptop, akachukua vifaa vyake vyote vya kazi, ile magazine ya bastola iliyojaa risasi na bastola ya Victor na kuviweka haraka kwenye lile begi la laptop kisha akaanza kupiga hatua kwa tahadhari kuelekea nje.

Kabla hajatoka alichungulia sebuleni na kumulika kwa kutumia ile kurunzi yake ndogo ya kishushushu, hakushangaa kuona kuwa hata kule sebuleni pia walikuwa wamepekua na kutawanya ovyo vitu vyake wakivitupatupa huku na kule. Kwa kuwa Tunu alikuwa amepata vitu vyake muhimu, sasa akili yake ilikuwa mbali, alikuwa anawaza jinsi atakavyoufunga ukurasa wa kesi ile na kuimaliza kabisa jeuri ya Mr. Oduya baada ya kushindwa kuikamilisha kazi hiyo miaka mitatu iliyokuwa imepita.

Wakati akitoka nje kupitia mlango wa jikoni mara akahisi kusikia vishindo hafifu vya watu waliokuwa wakiizunguka ile nyumba kuelekea kwenye mlango wa kuingilia mle ndani. Tunu alishtuka na kuondoka haraka eneo lile kwa mwendo wa kunyata, alikwenda kujibanza nyuma ya mti mkubwa wa kivuli.

Inaendelea...

CC the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater Bigjahman moneytalk marybaby nipo2 ram kisukari Smart911 Madame S carbamazepine Astelia culture gal Prisoner of hope Mine eyes kuku mweus Thad hearly Shunie Tumosa Mine eyes Kudo swahiba92 ludist Toyota escudo Clkey macson3 boga la kiangazi LEGE Smart911 Richard irakunda skfull popie Krizy Beat hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Mlenge Kacheda mjasiliamali Laki Si Pesa cocochanel kinusikwetu big jambo mludego Shupavu Kacheda mjasiliamali Mweweso Songa Heri esiankiki mnadhimu mkuu wa jf red apple the-sniper MR KUO dan oseko Jackal kuku mweus mtugani wa wapi huyo chiqutitta ndukulusudicho

NB: Litro 👩
 
Taxi - (139)

Kutokea pale aliweza kuwaona wanaume wawili waliovaa nguo nyeusi zilizowafanya wawe kama vivuli, walikuwa wakitembea kwa tahadhari pasipo kutoa kishindo na kuelekea ndani ya ile nyumba, kisha akamsikia mmoja wao akiita kwa wasiwasi kwa sauti ya chini yenye wasiwasi, “Victor! Victor!”

Tunu hakuwa na muda wa kupambana nao, alitumia mbinu yake ya kijasusi kuupanda ukuta haraka na kurukia nje pasipo kutoa kishindo. Mara tu alipotoka nje ya ile nyuma akakumbuka kuitazama saa yake ya mkononi na hapo akagundua kuwa alikuwa amepoteza takriban dakika therathini, kwani ilishatimia saa mbili za usiku.

Hakutaka kuelekea moja kwa moja barabara na kwenda kule alikokubaliana kukutana na kina Bob, hivyo akashika uelekeo wa upande wa kulia ili kumpoteza mtu yeyote ambaye angejitia kumfuatilia. Kutokea pale akaingia kwenye kichochoro kimoja na kuanza kutembea kwa tahadhari kwenye kile kichochoro huku mara kwa mara akigeuka na kutazama nyuma yake ili kuona kama kulikuwa na mtu yeyote aliyekuwa akimfuatilia. Hakumwona.

Alipofika mwisho wa kile kichochoro alisimama na kutathmini hali ya usalama wa eneo lile na aliporidhika akachepuka na kuvuka barabara ya mtaa ule wa nyuma kisha akaelekea upande wa pili. Akiwa upande wa pili wa ile barabara akaendelea kutembea haraka haraka na kwa tahadhari kubwa chini ya miti iliyokuwa pembeni ya barabara ile kando kando ya nyumba za makazi ya watu.

Ule mtaa ulikuwa ni wenye pilikapilika nyingi za watu kutokana na uwepo baa mbili tatu. Tunu alizidi kusonga mbele pasipo kuwajali wanaume waliokuwa wakigeuza shingo zao kumtazama na wengine kumwita, akaingia kwenye kichochoro kingine kilichompeleka katika mtaa wa pili kisha akashika uelekea mwingine uliompeleka hadi alipokwenda kutokea katika barabara ya Mtatiele.

Alipofika pale alisonga mbele zaidi hadi eneo alipokubaliana kuwakuta kina Bob wakimsubiri lakini hakuliona lile gari aina ya Nissan Patrol la rangi ya bluu wala dalili za kuwepo kina Bob, akaangaza macho yake huku na huko lakini hakukuwa na dalili zozote za uwepo wao. Tunu akatweta na kuchukua simu yake akitaka kupiga lakini akajionya kuwa huenda angeweza kuingia kwenye mtego.

Sasa hakuwa na namna nyingine ya kumfanya kuondoka haraka eneo lile isipokuwa kutafuta usafiri mwingine. Alianza kutembea huku akitupa macho yake huku na kule kutafuta usafiri wowote ambao ungemtoa eneo lile, mara akaiona taxi moja ikija kufuata uelekeo wake kwa mwendo wa kawaida.

Tunu akampungia mkono dereva wa ile taxi ambaye alipomfikia alisimama na kumfungulia mlango wa mbele lakini Tunu hakutaka kuketi mbele, akaufunga ule mlango na kufungua mlango wa nyuma kisha akaingia na kumweleza dereva ampeleke Ubungo. Yule dereva alikubali, lakini badala ya kuondoa gari alishuka na kuzunguka nyuma akiyatazama magurudumu kuona kama yangekuwa na hitilafu yoyote. Aliporidhika aliingia ndani ya gari lake na kutulia kwenye siti yake akionekana kama aliyekuwa anachunguza kuona kama kulikuwa tatizo mle ndani ya lile gari lake.

Tunu alianza kuingia na wasiwasi, alipotaka kumuuliza kama kulikuwa na shida au kitu chochote kilichokuwa kinaendelea pale akashtuka kuona mlango mmoja wa nyuma na mwingine wa mbele kushoto kwa dereva ikifunguliwa na wale watu wawili wanaume wakaingia haraka ndani ya gari na kuketi.

Tunu aligeuza shingo yake kuwatazama wale wanaume haraka haraka mmoja baada ya mwingine, wote wawili walikuwa wakimtazama kwa tabasamu lililojaa kejeli. Zilikuwa ni sura zilizopambwa na tabasamu la kinafiki lenye tafsiri halisi ya ushindi na macho yao yalimwonesha Tunu jambo moja tu, kwamba alikuwa “amepatikana”.

Akiwa ameshikwa na mshtuko wa hali ya juu, Tunu alianza kuyatembeza macho yake taratibu akizikagua vizuri sura za wale watu kisha akaweka kituo akimtazama yule dereva ambaye pia alikuwa anatabasamu. Tunu alijitahidi kuumeza mshtuko aliokuwa nao moyoni, akajifanya kuachia tabasamu kidogo kujifariji na kuitowesha hasira iliyokuwa imeanza kuchemka moyoni mwake.

Yule mwanamume aliyeketi siti ya mbele kushoto kwa dereva alikuwa mrefu na mweusi kama mjaluo, alikuwa na mwili ulioshiba na alivaa suti maridadi nyeusi. Macho yake yalikuwa makubwa mekundu yenye kila dalili za unyama. Tunu hakumtambua, akayahamisha macho yake kumtazama kumtazama mwanamume wa pili aliyeketi kule nyuma pamoja na Tunu na kumtambua.

“Spoiler!” Tunu alinong’ona kwa mshtuko. Alijikuta akiingiwa na hofu kubwa sana ingawa hakutaka kuionesha. Hapo hapo akili yake ikafanya kazi haraka sana, aliupeleka mkono wake kiunoni kwake kwa uficho ili kutoa bastola yake lakini akawa amechelewa, aliuona mtutu wa bastola aina ya FNX 45 Tactical yenye kiwambo cha kuzuia sauti toka kwa yule mwanamume aliyeketi mbele kushoto kwa dereva ukimwelekea usoni kwake. Akanywea.

“Tulia hivyo hivyo kama unanyolewa,” sauti tulivu ya yule mwanamume aliyeshiba ikapenya kwenye ngoma ya masikio yake huku bastola yake ikichukuliwa na Spoiler, “Kama hautakuwa mjinga basi utaendelea kuwa hai japo kwa saa kadhaa.” Yule mwanamume alifoka huku akiikoki ile bastola.

“Kwani shida yenu nini, mbona sielewi?” Tunu aliuliza huku akijitahidi kuifanya sauti yake ionekane ya kawaida.
“Haipendezi kuuliza swali ambalo jibu lake unalijua vyema,” Spoiler alimwambia Tunu kisha akamtazama yule dereva wa taxi. “Chuku ondoa gari uelekee Kinondoni.”

“Basi kama shida yenu ni mimi mmeshanipata, naomba nipake lipstick yangu ili tuelewane,” Tunu alisema na kuchukua kibomba kidogo cha rangi ya dhahabu kilichokuwa kinafanana sana na rangi ya mdomo, alipotaka kukifungua Spoiler akamdaka mkono wake na kumpoka kibomba hicho.

Kibomba kile kwa macho ya kawaida kilionekana kama kibomba cha kawaida cha rangi ya mdomo lakini kiuhalisia ilikuwa ni bastola hatari sana ya kijasusi (lipstick gun) iliyotengenezwa kwa mfano wa rangi ya mdomo. Kwa kukizungusha tu risasi ingeweza kutoka na kuua.

inaendelea...

NB: Litro 👩
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom