Stori ya kusisimua - Taxi

Stori ya kusisimua - Taxi

Jamani, mambo mengine humu ni utanii tu, just to be socially connected, so don't take it serious... Msinigombanishe na poti wangu the_legend maana naona sasa inageuka kuwa kama Simba na Yanga...

NB: Litro ‍🦱
Mkagombane.. kisa dem wa mitandaoni..
maskhara hayo aisee...

Naamini wote Shuu...wewe bishop na Legend...mnafaham vyema kuwa ni furahisha barza tu hii...!
Sema labda kama matani huyawezi.

Afu wengine wameunga trela humu..hawajui tumeanzia kuleee
mbali!

We sema maji yamezidi unga!

Na mpaka udondoshe choziiii...
 
Dada'angu, siwezi na wala sifikirii kuwa na IDs zaidi ya hii ninayotumia. For what? Ninachokifanya ni kwamba, Litro ni mtu wangu wa karibu sana na nilikuwa sijui kama humu JF anatumia ID hii. Tangu nilipogundua nimeamua kufanya fujo...

NB: Litro ‍🦱
Dah!...kwa hili sikurusha jiwe kwako mkuu... ..kabisa nakwambia!

Limetua sipo sory..mkuu..

Na ili nisikusumbue nitajitahidi nipunguze matani...ila Legend hana shida kabisa anajua ni matani ya kawaida...

NB
MIMI SI DADA NITAKE RADHI..

Furaha yangu iliyobaki ni hii..kucheka basi!..

Usijali mkuu...kama nakukwaza basi niwie radhi!
Nitaacha kutania.. .
 
Mine eyes,
Mbona dizaini fulani kama umepanic hivi. Nimepitia posti zako sioni hata moja inayoashiria utani zaidi ya kutuletea mjadala wa nani zaidi kati ya legend na bishop. Usitake kutuharibia uzi wetu kwa mambo ya kipuuzi. Unaposema wengine wameunga trela humu, hebu angalia mwaka niliojiunga halafu ujifananishe na wewe, utapata jibu aliyeunga trela nani.

Kama wewe ni mwanaume basi elewa kuwa mwanaume huwa haongei mara mbili, nadhani nimeeleweka.

CC Bishop Hiluka & the_legend
 
huba wake shunnie njoo basi utushushie mzgo mkuu maana arosto imeshaanza kupanda
 
M'bongo, Pole sana...

Siwezi na sitaweza kupanic kwa vitu vidogo namna hii...

Kama matani sikuanza kwenye uzi huu ...kwa wanaojua..yalianza mda mno kwenye riwaya nyengine ... ...
na ndio maana nikaongea haya.

Kuhusu kuunga trela..kama ni hilo ndio limekufanya kuandika hivi ..nasema tena pole sana ..maana sikukutaja, halijakuhusu na sikudhani kama wewe unaweza kuzungumza hili!
Hakuna sehemu yoyote nimetaja hata kwa matani neno M'bongo!
Siharibu na sitaharibu uzi... mwenye uzi nilishamjibu juu... ... na kanielewa

lini nimejiunga kwa jina hili si kigezo kwamba nipo juzi au mwaka juzi...

kuna sababu nyingi tu za kubadili jina tena za maanana inatokea sana tu.

Namalizia.... ..

Mwanamme huwa anaongea kiume tena kwa yanayo muhusu tu!
Nimelazimika kukujibu maana kama ni panic ni wazi inaonesha ipo kwa nani kwa mujibu wa ulichoandika!

Nafunga mjadala..kwa maana ya kufunga!

Hapa tunasoma riwaya tu ...ndio kubwa .. ..

samahani sana kwa kukwazika na yasiyo kuhusu!

Nitakuwa msomaji wa kimya ili..kuepuka haya... kweli kila mtu na ufahamu wake!

Bishop...

Nisamehe sana kwa haya yanayotokea!.

Lete:riwaya..tujiliwaze.. ...twende kazi mkuu... ... tufurahi sote!
 
Taxi - (123)

ILIPOISHIA

“Hakuna haja ya kumfuata, ngoja tuone nani mwingine atatoka humo ndani,” mwanamume mwingine aliyekuwa kwenye usukani alisema. “Tunachotakiwa kujua ni nani anashirikiana naye, basi!”

Yule aliyekuwa ameketi kwenye usukani alikuwa ni Victor na alikuwa ameshika kamera ndogo akipiga picha eneo lile kwa tahadhari. Mara wakamwona Tom akitoka ndani ya lile jengo na kupiga hatua zake haraka haraka huku akitazama chini, kisha akazama kwenye gari moja na kuondoka zake.

Wale watu waliokuwemo kwenye gari walimtazama kwa makini wakaonekana kumtambua, wakajikuta wakitabasamu.

“Dah! Nilihisi kitu kama hiki kutokea, hatimaye tumepata jibu. Sasa ni Tom na Tunu!” Victor alisema kisha akaangua kicheko hafifu kilichokuwa kimebeba uchungu na hasira huku akimtazama mwenzake aliyekuwa amekaa kando. “Nadhani sasa umenielewa, siyo?”

“Ulikuwa sahihi, Victor!” yule mwingine alisema huku akishusha pumzi ndefu.

“Nilikwambia tuliza kimuhemuhe kila kitu kitajulikana...” Victor alisema na kuwasha gari lake, wakaondoka.

* * * * *

Jitihada za madaktari na wauguzi hatimaye zilikuwa zimezaa matunda, Joyce alikuwa amezinduka na alishangaa sana kuona akiwa katika chumba chenye mitambo mingi pamoja na computer, yeye akiwa amelala kitandani amevishwa mitambo maalumu ya kumsaidia kupumua. Alizungusha macho yake huku na kule na kuwaona wauguzi wawili wakiwa katika harakati za kuchunguza hiki na kile ndani ya chumba kile.

ENDELEA...

Aliutazama mkono wake wa kulia uliokuwa umechomekwa sindano yenye mrija ambao ulipeleka damu kwenye mishipa yake ya damu, akashusha pumzi za ndani kwa ndani na kufumba macho yake kwa kitambo kifupi. Alipoyafumbua tena yalitua moja kwa moja kwenye uso wa muuguzi mmoja ambaye alikuwa amesimama jirani yake akirekebisha mwendo wa matone ya damu yaliyokuwa yakidondokea kwenye mrija uliopeleka damu kwenye mshipa wake wa damu.

Joyce alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akiminya midomo yake. Alikuwa akiuhisi mwili kama si wake. Yule mhudumu aliyekuwa akimhudumia alipogundua kuwa Joyce alikuwa amezinduka aliachia tabasamu. Joyce alitaka kutabasamu lakini hakuweza, akayahamisha macho yake kumtazama muuguzi mwingine ambaye alikuwa amekaa mbele ya kioo kikubwa cha computer iliyokuwa ikionesha mwenendo wa mapigo ya moyo.

Alimtazama yule muuguzi kwa makini kwa kitambo kifupi kisha aliyaondosha macho yake na kuyarudisha tena kwa yule muuguzi wa kwanza ambaye sasa alikuwa amesimama akimwangalia kwa upole, machozi ya huruma na furaha yalikuwa yakimlengalenga machoni.

“Pole sana, Mungu atakusaidia dada’angu, utapona tu. Kwa kuwa umeamka ngoja niwaite ndugu zako!” yule muuguzi alisema akimwambia Joyce kwa sauti ya upole kisha akatoka kuelekea nje huku macho ya Joyce yakimsindikiza nyuma yake.

Kule nje ya kile chumba yule muuguzi aliwakuta Madame Norah na Bi. Pamela wakiwa wameketi kwenye benchi, walionekana wenye sura za uchovu na simanzi na hawakujua hatma ya hali ya Joyce. Walishtuka kumwona yule muuguzi akiwajia huku amepambwa na uso wa tabasamu, kasha akawapa taarifa kuwa Joyce alikuwa ameamka.

Wote waliinuka, wakakimbilia ndani. Madame Norah alikuwa wa kwanza kuingia mle wodini, akafuatiwa na Bi. Pamela aliyekuwa nyuma yake, wote walikuwa wana shauku ya kumwona Joyce na kuisikia sauti yake. Joyce alimwona Madame Norah, kabla hajajua afanye nini akamwona Bi. Pamela akiwa nyuma yake, akapatwa na mshangao mkubwa. Aliwatazama wote wawili kwa zamu huku akionekana kuwa na maswali mengi kichwani kwake.

Alitamani sana kujua ni kwa nini alikuwa amelazwa ndani ya chumba kile chenye mitambo maalumu? Kwani ni nini hasa kilikuwa kimemtokea? Alijaribu kufikiria lakini akawa hakumbuki chochote. Madame Norah na Bi. Pamela walikuwa wamesimama hukuwakimwangalia kwa macho yenye upole yaliyojaa machozi ya furaha.

Waliendelea kumtazama kwa makini kisha wakaangaliana na kushusha pumzi za ndani kwa ndani na kuinua mikono yao juu kumshukuru Mungu.

Joyce alikuwa bado ana maswali lukuki kichwani, hakujua Sammy alikuwa wapi muda huo! Hakuwa amemtia machoni kabisa! Alijikuta akiingiwa na wasiwasi mkubwa. Alitaka kuinuka lakini akahisi maumivu makali sana eneo la kifuani na sehemu ya mgongoni. Madame Norah, kwa kushirikiana na yule muuguzi walimuwahi, wakamshika na kumzuia asiinuke.

Joyce alitii na kutulia huku akiendelea kuwaangalia Madame Norah na Bi. Pamela kwa zamu. Akalazimisha tabasamu na kufumba macho yake.

Wakiwa bado wamesimama pale wakamwona Daktari Mshana akiingia haraka, sura yake ilikuwa imesawajika kidogo na alikuwa anahema kwa nguvu. Alisimama, akawaangalia watu wote waliokuwemo mle ndani kisha macho yake yakatua kwa Joyce. Akaonekana kusita sana.

“Madame!” Daktari Mshana alimwita Madame Norah, uso wake ulikuwa na wasiwasi.

“Vipi dokta, kuna tatizo lolote?” Madame Norah aliuliza huku akiyatuliza macho yake kwenye uso wa Daktari Mshana.

“Samahani kwa usumbufu, naomba tuongee kidogo hapo nje,” yule daktari alisema kwa wasiwasi kisha akatoka nje bila kusubiri jibu la Madame Norah.

Madame Norah na Bi. Pamela wakaangaliana kwa mshangao na Madame Norah akanyanyua mabega yake juu na kuyashusha papo hapo, kisha akashusha pumzi na kutoka nje kumfuata yule daktari.

“Sijui umepata taarifa kuhusiana na shambulio lililotokea mchana huu?” yule daktari alimuuliza Madame Norah huku akimtulizia macho yake.

“Shambulio?” Madame Norah aliuliza kwa mshangao. “Shambulio gani, dokta?”

“Ina maana hamjapata taarifa zozote za kuhusiana na shambulio lililotokea muda mfupi uliopita?” yule daktari akauliza tena huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Hapana hatuna taarifa zozote. Ni shambulio gani tena hilo?” Madame Norah alizidi kushangaa. Sasa alihisi jasho jepesi likianza kumtoka sehemu mbalimbali za mwili wake na mapigo ya moyo wake yakibadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida!

“Nyumba ya mume wa huyo mgonjwa wenu imeshambuliwa kwa bomu na watu wasiojulikana muda mfupi uliopita...” yule daktari alisema huku akifuta jasho usoni kwake kwa kitambaa.

Oh my God!” Madame Norah aling’aka kwa mshtuko mkubwa, “Ilikuwaje? Vipi watu wamesalimika kweli?” aliuliza huku akihisi ubaridi mkali wa woga ukimtambaa mwilini. Midomo yake ilikuwa inamchezacheza.

“Mmoja hali yake ni mahututi, kiukweli kama ataweza kufika kesho asubuhi basi atapona, na hivi nilivyokuja kwako kuna utaratibu unafanywa apelekwe Muhimbili haraka...” yule daktari alisema, “Ila mwingine hali yake siyo mbaya, ana maumivu ya hapa na pale tu lakini hajaumia sana. Ndiye aliyenituma nije kukupa hizi habari.”

Itaendelea...

CC the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater Bigjahman moneytalk marybaby nipo2 ram kisukari Smart911 Madame S carbamazepine Astelia culture gal Prisoner of hope Mine eyes kuku mweus Thad hearly Shunie Tumosa Mine eyes Kudo swahiba92 ludist Toyota escudo Clkey macson3 boga la kiangazi LEGE Smart911 Richard irakunda skfull popie Krizy Beat hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Mlenge Kacheda mjasiliamali Laki Si Pesa cocochanel kinusikwetu big jambo mludego Shupavu Kacheda mjasiliamali Mweweso Songa Heri esiankiki mnadhimu mkuu wa jf red apple the-sniper MR KUO dan oseko Jackal kuku mweus

NB: Litro 👩‍🦱
 
Taxi - (124)

Madame Norah alishindwa aseme nini tena, aliweka mikono yake kichwani huku michirizi ya machozi ikianza kuonekana kwenye macho yake. Alibaki kimya kwa kitambo kifupi akionekana kuwa mbali sana kifikra kisha akamwashiria yule daktari amsubiri palepale. Akafuta machozi na kuingia ndani huku akijitahidi kutokuonesha hisia zozote za majonzi ingawa uso wake ulisindwa kuficha ile hali ya kunyong’onyea. Mikono alikuwa ameikunjia kifuani.

“Vipi, dada, kuna nini kimetokea?” Bi. Pamela alimuuliza Madame Norah huku akimtazama kwa makini.

Madame Norah alimtupia jicho Joyce ambaye pia alikuwa anamtazama usoni, akashusha pumzi na kulazimisha tabasamu ingawa bado tabasamu lake halikuweza kuiondoa hisia ya majonzi usoni kwake. Alibaki amesimama akiwa kimya huku akionekana kutafuta neno la kumwambia Bi. Pamela kwani hakutaka kuongea mbele ya Joyce kwa kuhofia kumsababishia matatizo mengine.

“Kuna nini?” Bi. Pamela aliuliza tena.

“Kuna matatizo fulani yametokea ofisini kwangu, nahitajika kwenda mara moja kuyashughulikia. Sasa njoo tuongee mara moja,” Madame Norah alimwambia Bi. Pamela aliinuka na kumfuata, wakatoka nje ambako walimkuta Daktari Mshana akisubiri.

“Sasa sikiliza, naomba uwe jasiri kwa hiki ninachokwenda kukwambia, sawa...” Madame Norah alianza kusema, “Nyumba ya mkweo Sammy imeshambuliwa na watu wasiojulikana wakati wao wakiwamo ndani...” Madame Norah alisema kwa sauti ya kumtetemeka.

“Mungu wangu! Wamesalimika kweli?” Bi. Pamela aliuliza kwa huku akihisi mwili wake ukiishiwa nguvu.

“Nimeambiwa mmoja wao yupo mahututi na mwingine kaumia kidogo tu, sasa sijajua ni nani aliye mahututi na nani hajaumia sana...” Madame Norah alisema huku akishindwa kuzuia machozi. Bi. Pamela naye hakuvumilia, akaanza kulia.

Daktari Mshari aliwataka wamfuate, wakaondoka hadi kwenye chumba kimoja ambako walimkuta Jengo akiwa amepumzishwa, mwili wake ulikuwa umelowa damu na alikuwa amefungwa bandeji kichwani na kwenye jeraha katika mkono wake wa kulia lililokuwa linatoa damu. Mwili wake wote ulikuwa unamteteteka kwa hofu ya kile alichokuwa amekishuhudia siku hiyo.

Madame Norah na Bi. Pamela walimtazama kwa mshangao mkubwa, kisha wakaangalia kwa kitambo pasipo kuongea chochote. Sammy hakuwemo katika chumba hicho. Kisha Madame Norah aliyarudisha macho yake kumwangalia Jengo huku mwili wake ukitetemeka. Machozi yalianza kububujika machoni na midomo yake ilishindwa kutulia, alikuwa anatetemeka japo alijitahidi kubana meno yake lakini bado haikusaidia.

Moyo wake ulikuwa umevunjika, hakutegemea kabisa kama siku ile ingegeuka kuwa ya huzuni kiasi kile badala ya kuwa siku ya furaha, furaha ya kumpata binti yake waliyepotezana kwa miaka therathini na mbili. Moyo wake sasa ulikuwa kama unaovuja damu ndani kwa ndani. Japo amewahi kupita katika mapito magumu sana lakini hakuwahi kuhisi hisia kama hizo hapo nyuma. Hakuwahi kuhisi namna ile tangu kuzaliwa kwake, hisia mchanganyiko wa hasira, uchungu na mfadhaiko kwa pamoja! Alitamani kupiga yowe kali kwa ghadhabu lakini hakuweza.

“Mkwe wangu yuko wapi, mbona simuoni hapa?” Bi. Pamela alimudu kuuliza baada ya kimya kirefu kutamalaki mle ndani.

“Hali yake ni mbaya sana, tulichohitaji ni kuwapa taarifa kuwa anapelekwa moja kwa moja Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, tayari taratibu zingine zote zimeshafanyika,” Daktari Mshana alisema huku akiangalia saa yake ya mkononi.

“Kwa hiyo dokta, huyu mwingine hajaumia mahala kokote?” Bi. Pamela alimuuliza Daktari Mshana huku akimtazama Jengo kwa namna ya kumkagua.

“Hata sijielewi elewi. Najihisi kama mtu niliyekufa,” Jengo alijibu huku akijitazama kwa namna ya kujikagua.

“Usiseme hivyo, hujafa. Bado unaishi...” Bi. Pamela alisema huku machozi yakimlengalenga machoni, kisha akaongeza, “Kwani hakuna sehemu yoyote inauma?”

“Ninasikia maumivu makali hapa katika mkono wa kulia labda kidogo kichwani na chini ya mguu wa kushoto,” Jengo alisema huku akionesha maeneo yenye maumivu.

“Pole sana,” Bi. Pamela alisema kwa upole huku akijifuta machozi.

Wakati hayo yanaendelea Madame Norah alikuwa bado amezama kwenye dunia yake, dunia ya kisasi. Sasa alikuwa anahisi kifua chake kikiwaka moto utadhani alikuwa anataka kulipuka! Aliapa kushughulika na yeyote aliyefanya hivyo. Donge la hasira lilikuwa limemkaba kooni na alikuwa anapumua kwa shida kama mgonjwa anayepigania pumzi ya mwisho.

Alichokumbuka kuongea muda huo ilikuwa kuomba ruhusa ya kumwona Sammy kabla hajapelekwa Muhimbili. Wote waliongozana hadi nje walikolikuta gari la wagonjwa likiwa tayari kuondoka. Sammy alikuwa kalala kwenye kitanda maalumu hajitambui, alikuwa kama mfu akiwa anapumua kwa msaada wa mashine maalumu ya kumsaidia kupumua na alitundikiwa chupa maalumu ya maji aina ya Normal Saline yaliyowekwa dawa maalumu ndani yake ili kusaidia kuyafanya mapigo ya moyo yasishuke.

Wote walishindwa kuyazuia machozi, walijikuta wakilia kwa uchungu huku wakimwangalia Sammy ambaye alikuwa ametulia, hatingishiki. Madame Norah alimwita Sammy huku akibubujikwa na machozi kana kwamba ni mama aliyempoteza mwanawe wa pekee kwenye shimo refu sana, alimwita huku akilia kilio cha uchungu.

asante sana bishop barikiwa kwa kazi nzuri..huu utamu wa simulizi hatari sana 🙄 🙄 🙄 kama vile wakati wa kiangazi jangwani ukapata pepsi ya baridi kale karadha murua utakachokapata ndo huu uzii sio wa mchezo mchezo
 
Pole sana...

Siwezi na sitaweza kupanic kwa vitu vidogo namna hii...

Kama matani sikuanza kwenye uzi huu ...kwa wanaojua..yalianza mda mno kwenye riwaya nyengine ... ...
na ndio maana nikaongea haya.

Kuhusu kuunga trela..kama ni hilo ndio limekufanya kuandika hivi ..nasema tena pole sana ..maana sikukutaja, halijakuhusu na sikudhani kama wewe unaweza kuzungumza hili!
Hakuna sehemu yoyote nimetaja hata kwa matani neno M'bongo!
Siharibu na sitaharibu uzi... mwenye uzi nilishamjibu juu... ... na kanielewa

lini nimejiunga kwa jina hili si kigezo kwamba nipo juzi au mwaka juzi...

kuna sababu nyingi tu za kubadili jina tena za maanana inatokea sana tu.

Namalizia.... ..

Mwanamme huwa anaongea kiume tena kwa yanayo muhusu tu!
Nimelazimika kukujibu maana kama ni panic ni wazi inaonesha ipo kwa nani kwa mujibu wa ulichoandika!

Nafunga mjadala..kwa maana ya kufunga!

Hapa tunasoma riwaya tu ...ndio kubwa .. ..

samahani sana kwa kukwazika na yasiyo kuhusu!

Nitakuwa msomaji wa kimya ili..kuepuka haya... kweli kila mtu na ufahamu wake!

Bishop...

Nisamehe sana kwa haya yanayotokea!.

Lete:riwaya..tujiliwaze.. ...twende kazi mkuu... ... tufurahi sote!
Jamani tumefikia huku tumshinde huyu shetani
 
Maskini
Taxi - (124)

Madame Norah alishindwa aseme nini tena, aliweka mikono yake kichwani huku michirizi ya machozi ikianza kuonekana kwenye macho yake. Alibaki kimya kwa kitambo kifupi akionekana kuwa mbali sana kifikra kisha akamwashiria yule daktari amsubiri palepale. Akafuta machozi na kuingia ndani huku akijitahidi kutokuonesha hisia zozote za majonzi ingawa uso wake ulisindwa kuficha ile hali ya kunyong’onyea. Mikono alikuwa ameikunjia kifuani.

“Vipi, dada, kuna nini kimetokea?” Bi. Pamela alimuuliza Madame Norah huku akimtazama kwa makini.

Madame Norah alimtupia jicho Joyce ambaye pia alikuwa anamtazama usoni, akashusha pumzi na kulazimisha tabasamu ingawa bado tabasamu lake halikuweza kuiondoa hisia ya majonzi usoni kwake. Alibaki amesimama akiwa kimya huku akionekana kutafuta neno la kumwambia Bi. Pamela kwani hakutaka kuongea mbele ya Joyce kwa kuhofia kumsababishia matatizo mengine.

“Kuna nini?” Bi. Pamela aliuliza tena.

“Kuna matatizo fulani yametokea ofisini kwangu, nahitajika kwenda mara moja kuyashughulikia. Sasa njoo tuongee mara moja,” Madame Norah alimwambia Bi. Pamela aliinuka na kumfuata, wakatoka nje ambako walimkuta Daktari Mshana akisubiri.

“Sasa sikiliza, naomba uwe jasiri kwa hiki ninachokwenda kukwambia, sawa...” Madame Norah alianza kusema, “Nyumba ya mkweo Sammy imeshambuliwa na watu wasiojulikana wakati wao wakiwamo ndani...” Madame Norah alisema kwa sauti ya kumtetemeka.

“Mungu wangu! Wamesalimika kweli?” Bi. Pamela aliuliza kwa huku akihisi mwili wake ukiishiwa nguvu.

“Nimeambiwa mmoja wao yupo mahututi na mwingine kaumia kidogo tu, sasa sijajua ni nani aliye mahututi na nani hajaumia sana...” Madame Norah alisema huku akishindwa kuzuia machozi. Bi. Pamela naye hakuvumilia, akaanza kulia.

Daktari Mshari aliwataka wamfuate, wakaondoka hadi kwenye chumba kimoja ambako walimkuta Jengo akiwa amepumzishwa, mwili wake ulikuwa umelowa damu na alikuwa amefungwa bandeji kichwani na kwenye jeraha katika mkono wake wa kulia lililokuwa linatoa damu. Mwili wake wote ulikuwa unamteteteka kwa hofu ya kile alichokuwa amekishuhudia siku hiyo.

Madame Norah na Bi. Pamela walimtazama kwa mshangao mkubwa, kisha wakaangalia kwa kitambo pasipo kuongea chochote. Sammy hakuwemo katika chumba hicho. Kisha Madame Norah aliyarudisha macho yake kumwangalia Jengo huku mwili wake ukitetemeka. Machozi yalianza kububujika machoni na midomo yake ilishindwa kutulia, alikuwa anatetemeka japo alijitahidi kubana meno yake lakini bado haikusaidia.

Moyo wake ulikuwa umevunjika, hakutegemea kabisa kama siku ile ingegeuka kuwa ya huzuni kiasi kile badala ya kuwa siku ya furaha, furaha ya kumpata binti yake waliyepotezana kwa miaka therathini na mbili. Moyo wake sasa ulikuwa kama unaovuja damu ndani kwa ndani. Japo amewahi kupita katika mapito magumu sana lakini hakuwahi kuhisi hisia kama hizo hapo nyuma. Hakuwahi kuhisi namna ile tangu kuzaliwa kwake, hisia mchanganyiko wa hasira, uchungu na mfadhaiko kwa pamoja! Alitamani kupiga yowe kali kwa ghadhabu lakini hakuweza.

“Mkwe wangu yuko wapi, mbona simuoni hapa?” Bi. Pamela alimudu kuuliza baada ya kimya kirefu kutamalaki mle ndani.

“Hali yake ni mbaya sana, tulichohitaji ni kuwapa taarifa kuwa anapelekwa moja kwa moja Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, tayari taratibu zingine zote zimeshafanyika,” Daktari Mshana alisema huku akiangalia saa yake ya mkononi.

“Kwa hiyo dokta, huyu mwingine hajaumia mahala kokote?” Bi. Pamela alimuuliza Daktari Mshana huku akimtazama Jengo kwa namna ya kumkagua.

“Hata sijielewi elewi. Najihisi kama mtu niliyekufa,” Jengo alijibu huku akijitazama kwa namna ya kujikagua.

“Usiseme hivyo, hujafa. Bado unaishi...” Bi. Pamela alisema huku machozi yakimlengalenga machoni, kisha akaongeza, “Kwani hakuna sehemu yoyote inauma?”

“Ninasikia maumivu makali hapa katika mkono wa kulia labda kidogo kichwani na chini ya mguu wa kushoto,” Jengo alisema huku akionesha maeneo yenye maumivu.

“Pole sana,” Bi. Pamela alisema kwa upole huku akijifuta machozi.

Wakati hayo yanaendelea Madame Norah alikuwa bado amezama kwenye dunia yake, dunia ya kisasi. Sasa alikuwa anahisi kifua chake kikiwaka moto utadhani alikuwa anataka kulipuka! Aliapa kushughulika na yeyote aliyefanya hivyo. Donge la hasira lilikuwa limemkaba kooni na alikuwa anapumua kwa shida kama mgonjwa anayepigania pumzi ya mwisho.

Alichokumbuka kuongea muda huo ilikuwa kuomba ruhusa ya kumwona Sammy kabla hajapelekwa Muhimbili. Wote waliongozana hadi nje walikolikuta gari la wagonjwa likiwa tayari kuondoka. Sammy alikuwa kalala kwenye kitanda maalumu hajitambui, alikuwa kama mfu akiwa anapumua kwa msaada wa mashine maalumu ya kumsaidia kupumua na alitundikiwa chupa maalumu ya maji aina ya Normal Saline yaliyowekwa dawa maalumu ndani yake ili kusaidia kuyafanya mapigo ya moyo yasishuke.

Wote walishindwa kuyazuia machozi, walijikuta wakilia kwa uchungu huku wakimwangalia Sammy ambaye alikuwa ametulia, hatingishiki. Madame Norah alimwita Sammy huku akibubujikwa na machozi kana kwamba ni mama aliyempoteza mwanawe wa pekee kwenye shimo refu sana, alimwita huku akilia kilio cha uchungu.

Itaendelea...

NB: Litro 👩‍🦱
Maskini samY

ki
 
Usiache ulimi wako ukafuata macho yako kwa kueleza aibu za wengine, kumbuka kuwa hata hao watu wengine nao wana macho na ulimi kama wewe. Pia kumbuka kuwa: BUSARA moja ya UKIMYA ni kwamba UTAEPUKA kusema AMBAYO hukutarajia KUYASEMA...

Nawatakia siku njema...

NB: Litro
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom