Taxi - (120)
ILIPOISHIA
“Ninahisi gari hili limewekwa
GPS device ili kuni-
track waweze kujua kila ninapokwenda,” Tunu alisema.
Wale wanaume wakaanza kulikagua gari wakianzia kwenye sehemu za ndani ambazo magurudumu hufungwa kuona kama vifaa vya
GPS vilikuwa vimepachikwa lakini hawakuona kitu, inaaminika kuwa kwa vyovyote mtu mtaalamu wa mambo hayo asingeweza kufunga kifaa kama hicho sehemu hiyo.
Wakafungua boneti la gari na kuchunguza kila sehemu kwa uangalifu sana, walikagua injini nzima kwa kutumia kioo maalumu na tochi lakini hawakuona chochote. Wakachunguza chini ya gari wakiiangalia injini kutokea chini hadi juu lakini hakukuwa na kifaa chochote cha GPS. Wakafungua siti za gari na kuangalia chini, pia hakukuwa na chochote.
Walipokosa maeneo yote hayo wakaondoa redio kwenye dashbodi na kuchunguza kwa ndani na kila sehemu, hakukuwa na kitu. Kisha wakaondoa paneli za milango na kava za spika na kuchunguza. Walipokosa wakaangalia kwenye mikono ya milango (
handles) na kwenye vifungo vyake, wakakiona kifaa kimoja cha GPS kilichokuwa kimewekwa kitaalamu sana kwenye kifungo cha mkono wa mlango wa kushoto, kiasi cha kumfanya mtu asiye mjuzi wa mambo hayo asiweze kugundua.
SASA ENDELEA...
Tunu na Tom wakaangaliana, macho yao yaliweza kuongea mengi kuliko ambavyo wangeweza kuongea kwa midomo yao kisha Tunu akashusha pumzi za ndani kwa ndani.
“
You were right! Ulikuwa umechezewa mchezo ili waweze kujua kila unapokwenda,” Tom akasema huku akiweka mikono yote miwili kwenye kiuno chake. Alikuwa anatweta.
“
I dont believe this, Victor ndiyo kaamua kunichezea mchezo, siyo?
I knew it!” Tunu alisema kwa sauti tulivu lakini iliyobeba hasira ndani yake huku akimtazama Tom. Aliuma midomo yake na kushusha pumzi kisha akabetua kichwa chake huku akijitahidi kudhibiti hasira zake.
“Hivi huyu ni Victor yupi?” Tom akauliza huku akimtazama Tunu kwa makini.
“Nitakuelezea baadaye,
I truted the guy lakini kumbe ni nyoka! Hata sijui kwa nini roho yangu ilikuwa nzito sana kumweleza chochote kuhusiana na mambo haya japo alikuwa ananiuliza maswali mengi sana yaliyonifanya kuanza kuwa na shaka kidogo!” Tunu akasema na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.
Wale wanaume wa kazi walimaliza kazi yao kulikagua lile gari kwa makini katika kila sehemu waliyodhani kungeweza kufichwa kifaa cha GPS na hakuona kifaa kingine. Wakampatia Tunu kile kifaa walichoking’amua, Tunu akakitazama kwa makini na kuachia tabasamu la uchungu, kisha akabana taya zake na kuanza kukereza meno yake huku akizuia hasira zilizoanza kumpanda.
“Sasa nitawafanyia uhuni ambao hawajawahi kufanyiwa, ninakwenda kukitelekeza hiki kifaa
Central Police, hapo ndipo watakapofurahi na roho yao!” Tunu alisema kisha wote wakaangua kicheko. Alitoka nje na kuwaacha wanaendelea kurudishia vitu vyote kwenye gari kwa usimamizi wa Tom, yeye akakodi pikipiki na kuelekea moja kwa moja Kituo Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam.
* * * * *
Magari mawili ya zimamoto na ving’ora vya magari ya polisi yalionekana yakielekea katika mtaa ilipokuwa nyumba ya Sammy, eneo la Tabata Chang’ombe yakiwa katika mwendo wa kasi. Yalipofika kazi ya kuuzima moto ilianza harakaharaka ili kuzuia moto ule usiweze kusambaa katika nyumba za jirani na kusababisha maafa zaidi na baada ya muda mfupi juhudi zao kuuzima moto huo zikaonekana kufanikiwa.
Nyumba ya Sammy ilikuwa imebomoka na kubaki kama gofu huku gari lake aina ya Cadillac DeVille likiwa limeteketea kabisa na kubakichuma chakavu.
Ndani ya muda mfupi barabara zote za kuingia na kutoka katika mtaa ule zilikuwa zimewekwa kizuizi cha askari na eneo la nyumba ya Sammy likazungushiwa utepe maalumu wa njano maarufu kama
Barricade tape wenye maandishi ya “
Police Line Do Not Cross”. Kila mtu aliyetaka kupita eneo lile alisimamishwa, akahojiwa na kama alionekana hahusiki basi alizuiwa kupita.
Dakika zilizofuata eneo lote lilijaa magari, yakiwemo ya polisi, mawili ya jeshi la wananchi na magari mawili ya wagonjwa yaliyokuwa yameegeshwa kandokando ya barabara kulizunguka eneo lile huku askari wenye silaha wakishika doria kulinda iwapo kungetokea vibaka waliotaka kupora. Askari wale walikuwa makini sana wakizungusha macgo yao pembe zote. Pia walikuwepo wataalamu wa mabomu toka jeshini waliokuwa wakikagua eneo lote kuona kama kulikuwa na mabomu mengine ambayo hayajalipuka.
Makundi mbalimbali ya watu yalikuwa yamekusanyika katika eneo lile, watu hao, wakubwa kwa wadogo, walikuwa wanashangaa na wengine wakisimuliana jinsi walivyoshuhudia mlipuko mkubwa ulioliteketeza kabisa gari la Sammy na kubomoa ile nyumba. Hakuna kati yao aliyekuwa anaruhusiwa kusogea karibu na eneo ambalo mlipuko huo au kuvuka uzio uliokuwa umewekwa kwa hofu kuwa huenda kulikuwa bado na masalia ya mabomu mengine.
Kati ya watu waliokuwepo eneo lile wakionekana kushangaa ni mwanamume mmoja mrefu mwenye ndevu nyingi aliyekuwa amevaa suti nzuri ya rangi ya hudhurungi na viatu vyenye rangi hiyo hiyo. Alitembea kwa hatua za wastani, macho yake yakilenga zaidi kuangalia kwenye kifusi cha nyumba kuona kama kulikuwa na majeruhi yeyote wa lile tukio. Alipobakiza kama hatua mbili kuufikia ule uzio wa njano wenye maandishi ya “
Police Line Do Not Cross” alijitoa katika kundi la watu wengine, akajiegemeza ukutani mwa duka moja la Mangi.
Alisimama pale akawa anashangaa huku akijaribu kuuliza kama kuna mtu yeyote aliyeokolewa kwenye lile tukio akiwa hai. Hakuna aliyejishughulisha naye kwani wote aliokuwa akiwauliza na wao walikuwa wamefika hapo muda mfupi tu kabla yake, akatoa sigara yake na kuwasha kisha akawa anavuta taratibu huku akiangaza macho yake pembe zote, kisha akayatuliza kwa wanajeshi wa kutegua mabomu na askari wa uokoaji ambao walikuwa wanafukua kifusi kuona kama kulikuwa na mtu yeyote aliye hai.
Muda huohuo gari la Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam likaingia. Naibu Kamishna Ramon Mamboleo akashuka haraka toka kwenye gari lake na kuanza kutembea kwa ukakamavu huku akiangaza macho yake pembe zote kama aliyekuwa anachunguza kitu. Alikuwa askari makini sana na mkakamavu asiyeruhusu makosa ya kipumbavu yaliyoashiria uzembe yatokee awapo kazini.
Kabla ya kupandishwa kuwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna Mamboleo alikuwa Mkuu wa Upepelezi. Hakuwa na mzaha kabisa awapo kazi, angeweza kumfuatilia hata shetani katika harakati zake za kuharibu Amani au maadili mema ya wana wa Mungu na akamtia mbaroni kisha akamburuza mahakamani, tena peke yake.
Itaendelea...
CC
the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater Bigjahman moneytalk marybaby nipo2 ram kisukari Smart911 Madame S carbamazepine Astelia culture gal Prisoner of hope Mine eyes kuku mweus Thad hearly Shunie Tumosa Mine eyes Kudo swahiba92 ludist Toyota escudo Clkey macson3 boga la kiangazi LEGE Smart911 Richard irakunda skfull popie Krizy Beat hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Mlenge Kacheda mjasiliamali Laki Si Pesa cocochanel kinusikwetu big jambo mludego Shupavu Kacheda mjasiliamali Mweweso Songa Heri esiankiki mnadhimu mkuu wa jf red apple the-sniper MR KUO dan oseko Jackal kuku mweus
NB:
Litro 👩🦱